Mwigulu Nchemba ateuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Tizeba apelekwa Kilimo na Mifugo

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Rais John Pombe Magufuli leo tarehe 11 June 2016, amemteua Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi. Mhe. Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Charles Muhangwa Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Wakati huo huo rais amemteua mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na uvuvi, nafasi iliyokua ikishikiliwa na Mhe. Nchemba.

Wateuliwa wataapishwa siku ya Juma tatu majira ya saa 3:00 asubuhi Ikulu.


image.jpeg
 
Nampa Hongera Mwigulu. Lakini pia ni Pigo kwa Wizara ya Kilimo

Sitaki kusema pia uteuzi umefanyika muda huu ili kupoteza mijadala na attention dhidi ya Bajeti Mbovu ya Serikali

Ni kweli nampa Hongera Mwigulu Nchemba kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya Ndani.Naamini utaweza kusimama kishujaa kama ulivyosimama na kwenda kinyume na Wenzako kwenye sakata la ESCROW Bungeni

Wizara hii ngumu hujapewa kwa bahati mbaya.Kama lengo ni kukumaliza kisiasa basi silaha yako kubwa ni Watanzania endapo utasimama kwa haki na Uaminifu utashinda mitego yote

Naamini unao uwezo wa kutofuata nyayo za watangulizi wako na kusimama kwa taaluma,busara na weledi kama ulivyosimama kwenye ESCROW na pia ulivyowatahadharisha wenzako ndani ya chama katika Bunge la Katiba kuwa mchakato ule ungekwama na hivyo kulaumiwa kwa kutumia fedha nyingi.Yote yalitokea

Na sasa simama kuhakikisha unarejesha imani ya vyombo vilivyo chini ya Wizara yako kama Polisi kurejesha uhusiano mzuri na Raia

Jeshi la Polisi linahitaji kufumuliwa na kuwa chombo cha huduma kwa Raia na Mali zao yaani Police Service

Ufanisi hauwezi kuwepo ikiwa kuna uadui kati ya Polisi na Raia au Polisi wanatumika kisiasa


Wizara hii ni wizara ngumu sana lakini kama utafanya kazi kwa Uaminifu kama alivyowahi kufanya Augustine Lyatonga Mrema enzi za Utawala wa awamu ya Pili basi Utakuwa umewapa watanzania zawadi

Usifuate nyayo za watangulizi wako akina Omar Ramadhani Mapuri, Nahodha au Nchimbi na Akina Kitwanga

Kuhusishwa kwako na njama za kuangamiza CHADEMA ukiwa naibu Katibu Mkuu CCM ni wakati na fursa kwako sasa kuhakikisha vyombo vilivyopo chini yako vinatenda kwa haki na havitumiki kisiasa.Hiyo itakua baraka kwako kisiasa

Usiliache suala la Lugumi likaenda na Ulevi wa Kitwanga

Fufua Vita ya Madawa ya Kulevya aliyoianzisha kijana Mwenzetu Amina Chifupa(Apumzike Kwa Amani)

Waliotajwa kwenye Ripoti ya Jaji Maneto kwenye Mauaji ya Mwanahabari David Mwangosi bado hawajakamatwa wote na wengine wapo ofisini kwa kupandishwa vyeo

Hakikisha haki za binadamu zinalindwa ndani ya magereza

Komesha Mauaji ya Raia wasio na hatia na pia yale ya Kisiasa .Ni fursa ya kufufua waliohujumu mikutano ya kisiasa na kusababisha mauaji kule Arusha .Ni Fursa ya kumaliza chuki kati ya Raia na Jeshi la Polisi

Simama kwa uaminifu dhidi ya Rushwa kwa askari Wetu

Boresha Maslahi ya Askari Wetu

Kwa bahati Mbaya unaenda kuongoza Wizara ambayo bajeti yake hukuiandaa Wewe

Nakutakia Kila la Kheri
 
Hii nchi hapa ndio huwa sielewi,mtu mmoja kuhamishwa Wizara kutoka hii kwenda hii sasa hatujaanza kuona mafanikio au performance ya Mwigulu katika Wizara ya Kilimo pamoja na kuwa na Mwanzo Mzuri mara kahamishwa Wizara sasa kule anaenda kuanza Upya kuanzia mipango hadi Utekelezaji,muda mwingine huwa naona Serikali huwa inajirudisha nyuma kwa hatua zake yenyewe inayochukua
 
Hii nchi hapa ndio huwa sielewi,mtu mmoja kuhamishwa Wizara kutoka hii kwenda hii sasa hatujaanza kuona mafanikio au performance ya Mwigulu katika Wizara ya Kilimo pamoja na kuwa na Mwanzo Mzuri mara kahamishwa Wizara sasa kule anaenda kuanza Upya kuanzia mipango hadi Utekelezaji,muda mwingine huwa naona Serikali huwa inajirudisha nyuma kwa hatua zake yenyewe inayochukua
kwa kweli
 
Back
Top Bottom