Mwigulu Nchemba aombwa kuongoza majimbo mawili, wananchi wazuia mwenge kwa muda...

Mleta mada ana jinsia gani ? sifa hizi mara nyingi ni za mke kwa mume au mume kwa mke

Tena anaonekana akili yake cyo nzuri, Sisi ni wakazi wa Iramba mwigulu hamna alichokifanya cha maana humu jimboni na asitegemee mwenge eti kupanda kisiasa arudi bungeni! Ni ngum kwake kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano wapambe wanampoteza, eti mchapa kazi angezema mgoni tu au mzinzi.
 
Mleta mada ana jinsia gani ? sifa hizi mara nyingi ni za mke kwa mume au mume kwa mke

Kabla hujauliza ya watu wengine, tangaza kwanza ya kwako hadharani na kutokufanya hivyo inakuwa ni kama unafiki na wivu kihoja.
 
Tena anaonekana akili yake cyo nzuri, Sisi ni wakazi wa Iramba mwigulu hamna alichokifanya cha maana humu jimboni na asitegemee mwenge eti kupanda kisiasa arudi bungeni! Ni ngum kwake kama ngamia kupenya kwenye tundu la sindano wapambe wanampoteza, eti mchapa kazi angezema mgoni tu au mzinzi.

Hii ni haki yako lakini kumbuka hata kwenye vita vya Iraq kulikuwa na mtu aliyekuwa anaitwa Mohammed Saeed al-Sahhaf alikuwa na rhetoric kama unazosema wakati mvua ya mabomu ikinyesha jirani na jengo lake.
 
hongera mwigulu nchemba,chadema lazima muumize kichwa.

hivi inaruhusiwa kuvaa uniform za jeshi la nchi nyingine? Mwigulu hiyo kofia yake ni ya jeshi la china lijulikanalo kama red briged na nashangaa bado hajachukulia hatua!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Lazima wauzuie mwenge Washangae Magari ambayo hawajawahi kuona,Mwigulu anatamani hao watoto wa shule waliomshangilia wawe mafala ivyo hivyo.
 
Mkuu Taswira, heshima kwako mkuu.

Mimi nimefurahi kuona umeleta matukio muhimu ili nasi tuone kilichojiri.

Pamoja na hayo yote, napenda kukupa pole kwa safari zako ukiwa na Mwenge wa Uhuru ingawa kazi yako kubwa naona ni kuripoti vituko vinavyofanywa na Boss wako Mwigulu Nchemba Madelu.

Lakini kuna moja ambalo umesahau kuriripoti, labda ni kuwa umesahau au Boss wako kakukataza kwa sababu limekaa vibaya.

Naomba kuliweka hapa jamvini suala hilo ili nikusaidie kazi zako unazotumwa na wakuu wako wa kazi.

Naamini ulikuwa pamoja na msafara wa Mwenge mpaka ulipofika pale kijiji cha Misigiri. (Kwa wale wasipopajua, Misigiri ipo Singida-Nzega Road. Ukimaliza tu kijiji hiki unaanza kuteremka Mlima maarufu unaoitwa Sekenke, kama unaelekea Mwanza).

Nirudi kwenye mada sasa.

Katika kijiji hiki, kulikuwa na shughuli ya uzinduzi wa Soko la Kuku kama lilivyoitwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba.

Kama ilivyo ada Mwenge ulifika majira ya saa 8 au 9 hivi ndipo kihoja kilipotokea.

Wakati wa kusoma matumizi yaliyofanyika katika ujenzi wa soko hilo, nilipatwa na bumbuwazi na mshangao usio na kifani pale nilipoambiwa kuwa soko hilo limeghaeimu kati ya Million 70 na Million 80 za kitanzania.

Sikuwa na hoja wala swali ila leo imenibidi nitumie weekend yangu kwa kwenda eneo la tukio na kujionea huo ujenzi wa soko kwa gharama zilizotajwa.

Kwanza nilianza kwa kwenda kwenye soko lenyewe na kupata uhalisi kwa macho. Kisha nilianza kuwahoji baadhi ya watu waliokuwepo hapo wakati wa uzinduzi.

Wengi wao wanaonekana kuhoji uhalisia wa jengo la soko hilo na kiasi cha pesa kilichotajwa kujenga jengo hilo. Na pia wamenidokeza kuwa kiasi cha Shilingi Million 8 ni michango yao waliochangishwa na Viongozi wa kijiji waliopita nyumba hadi nyumba. Na wapo waliopelekwa polisi na Mahakama kwa kosa la kutolipa michango hiyo.

Pia wapo wanaolalamika kulazimishwa kufunga biashara zao za Mama Ntilie na Viduka vidogo ili waende kuusubiri Mwenge. Viongozi hao wa Kijiji waliwatisha kuwa kama hawatowenda watatozwa faini ya Shilingi Elfu 5.



Kwa kumalizia kazi yangu ya kupekua jambo hili, nilitafuta chanzo kimoja ili kinipatie picha ili nizilete hapa jamvini. Naamini kuwa humu JF kuna wataalamu wa Civil Engineering na watatupa BOQ inayohusiana na soko hilo. Nimefanikiwa kupata baadhi ya picha.

My Take:

1. Nataka Mkuu Taswira atueleze kwa nini hakuweka pia picha na maelezo ya tukio hili.

2. Kwa sababu Mh. Mwigulu Nchemba yupo humu JF na alikuwepo wakati wa uzinduzi wa Soko hilo na kusikia gharama za soko, basi aje na gharama halisi za soko na atuonyeshe mchanganuo wa fedha hizo zilivyotumika. Hii ni kwa sababu Mwigulu Nchemba anaingia kwenye vikao vya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba na anajua kila kinachoendelea.

3. Pia, baada wa Wataalamu wa Civil Engineering kuja na BOQ ya soko hili, wanajamvi tujadili na tumuangalie kwa jicho la tatu Mh. Mwigulu Nchemba na watendaji wakuu wote wa Wilaya ya Iramba.


Stay Tuned for More Updates.
 
Last edited by a moderator:
uploadfromtaptalk1376272076529.jpg uploadfromtaptalk1376272117843.jpg uploadfromtaptalk1376272154136.jpg uploadfromtaptalk1376272184216.jpg uploadfromtaptalk1376272213187.jpg
 
IRAMBA magharibi wamlilia mbunge wao Mwigulu Mnchemba.
Wanasema ukistaajabu ya Mussa utaona ya Mwigulu,
Wakati mbunge wa Singida magharibi Mhe. Mwigulu Mnchemba anapasua masafa ya nchi wapiga kura wake wanamlilia kweli aende akawasikilize matatizo yao kwani shida zimewakaba hadi shingoni. Wanamstaajabu mbunge wao ambae wakati rais wake anachanja mbuga duniani yeye mbunge anachanja mbuga inchini akiwawakilisha wanainchi ambao hawakumchagua akiwaacha wao katikati ya lindi la matatizo. Nimepita jimboni mwa huyo mbunge wapiga kura wake wakanieleza yafuatayo kwa mdomo wao:-
Shida zinazowakabili-
1. Njaa kali.
Wana uhaba mkubwa wa chakula mvua zilikuwa haba sana ukitilia maanani wenywe wako kwenye bonde la ufa inabidi kupata mvua za kutosha ili wavune mtama (lugugu) wacha mahindi, kwa hiyo wanauhaba mkubwa wa chakula familia nyingi karibu % 90 katika jimbo la Mwigulu wanakula mlo mmoja na huo mlo mmoja hawashibi. Watoto wa shule wanashindwa kwenda shule shauri ya njaa, pia wakirudi nyumbani saa 6 wanalala inje ya nyumba shauri ya njaa kali ndani hamna kitu na wazazi wao hawapo wamekwenda kutafuta vibarua, wengine wanazirahi.
2. Umasikini wa kipato.
Wanaumaskini mkubwa wa kipato wachilia mbali njaa inayowakabili, hawana zao lolote la maana la biashara,ajira wanayoitegemea ingalao kupata kipato ili kutatua matatizo yao ni ombaomba kwenye treni, na biashara za ovyoovyo kwenye treni yakati biashara kama kuuza ujugu, vikapo , vindege, vifilimbi vya miti, ukwaju na ubuyu, ni vibiashara vya kijinga jinga tu, vijana wengi wamekimbia jimbo wasichana kwa wavulana wameenda kutafuta ajira mjini na wengine wameenda kutafuta vibarua vya kulima tumbaku katika vijiji kata ya Igwisi urambo.
3. Ukame mkali.
Kuna ukame wa hali ya juu, ukame unawakabili watu na mifugo, mifugo kuanzia vijiji vya Kintinku, Igose, Makutupora Kirimatinde Salanda, Ulyampiti, Msigili hadi Sherui mifugo wanakunywa mgwao, yaani wanakunywa leo siku inayofuata hawanywi maji.Maji yenyewe wanayapata kwa kuesea kwa kutumia Nkosi,wanadamka usiku kwenda kwenye visima walivyochimba wenyewe ili kuchotelea maji kwa kutumia nkosi na kujaza mrambo ili mchana mifugo waje wanywe, kazi hiyo ni ngumu sana inawafanya vijana wengi kukimbia makazi yao au kuwa ni ajira kwa wenye uwezo, mtu unafanya kazi hiyo ngumu halafu anaishia kupewa chakula tu jioni.
4. Wizi wa mifugo.
Kuna wizi wa mifugo wa hali ya juu, hii ni kutokana na njaa kali, mifugo inaibiwa nyumbani usiku au mchungaji ananyang`anywa mchana kweupe machungani, mifugo inaibiwa kiasi kuna tishio la mifugo kwisha kwa wizi, wengine huiba mbuzi na kwenda kuchinja polini na kuishia kula nyama shauri ya njaa.
5. Magonjwa:
Tunakabiliwa na magonjwa ya kuambikiza, magonjwa yanayotusumbua ni Malaria na kichocho, malaria inatusumbua kwa ajili ya joto hapa jimboni kwa Mwigulu ni bonde la ufa yaani ardhi imetitia chini hivyo joto kweli usiku na mbu ni wengi , kwenye vituo vya kutolea huduma ya afya kama zahanati na vituo vya afya hamana dawa mseto kuna paracetamo tu, pia uwezo wa kukata bima ya afya hatuna kwa sababu ya umasikini wa kipato, Kichocho kinasumbua sana hasa wanafunzi ,shule kama Ndago karibu wanafunzi wote wana kichocho dawa ya Parazenguantel hamana katika vituo vyote hadi hospitali ya mkoa ya Singida, halafu dawa yenyewe ni ghali. Pia jimbo la Iramba magharibi karibu lote linakabiliwa na tatizo la mishoo kwa ajili ya kula nyama mbichi za wizi.
Ushauri kwa Mbunge wa Mwigulu
Aje akae jimboni ili waweze kusaidiana kukabili matatizo haya , huko unakozurula kwani ndiko walio mchagua? Aache kuhangaika na LEMA kwani mbunge huyo hamwezi wanaweza wenyewe waliomchagua. Kupenda ni sehemu ya uhai , kumeambatana na uhai kupenda hakuwezi kwisha mpaka uhai umetoweka kwa hiyo kama Arusha wanampenda mbunge wao Mwigulu hata ufanyeje unajisumbua tu njoo jimboni utusaidie wapiga kura wako tunakwisha. Huyo LEMA unayempiga vita yeye anawapigania wapiga kura wake hadi saa ingine bungeni haendi hadi anafungwa jela mahabusu wewe Mwigulu unazurula tu unatusahau,

Kama mbunge una uwezo kutusaidia kupata dawa hasa za kichocho, kulobe chakula kije jimboni ingalao tutanua, Kwenye jimbo la Tundu Lisu mashuleni wanafunzi wanapata mlo wa mchana kupitia Pragram ya WFP, Mbunge wetu Mwigulu yuko wapi na sisi tupate mpango huu. Njoo tusaidiane kuandaa mkakati wa kukabiliana na wizi wa mifugo, njoo tujipange tuweze kukata bima za afya kwa watendaji wa kata ingalao zituwezeshe kupata matibabu hata hayo kiduchu.
Mbunge wetu Mwigulu njoo jimboni sisi wapiga kura wako tunakulilia kwani hiyo jeuri uliyopewa na Rais kwamba wewe unakabiliana na wapinzani hukimbilii polisi isikuvimbishe kichwa kiasi unasahau wajibu wako. Wacha kujishebedua na mkutano huko Dar. Njo site uone mwenywe serikali ya chama chako ilivyotufanya mbaya kwa kutufanya tuwe maskini wa kutupya, ile kambi ya wakoma ya sukamahela imeanza kujaa tena wengi wa wagonjwa wanatoka wilaya ya Iramba.




 
Eti wananchi waliuzuia mwenge ili wasikie sauti ya Mwigulu.Inamaana huo mwenge ulikuwa unakimbizwa na Mwigulu mpaka wananchi wakapata nafasi ya kuuzuia? Ina maana wananchi wa jimbo lake hawajawahi kusikia sauti ya mbunge wao hata anapotoa michango yake bungeni wao huwa hawaisikii? Inamaana Mwigulu huwa hatembelei jimboni kwake ili awapelekee wananchi sauti yake ambayo wameiona ya maana kwao mpaka asubiri siku ya mwenge ndiyo awapelekee sauti yake?.Pamoja na maneno matam ya kumpamba Mwigulu hamna kitu chochote cha maana hapa.Kinachoonekana ni kwamba wananchi walikuwa kwenye shughuri zao za mapokezi ya mwenge halafu Mwigulu kwa kujipendekeza ana kwenda kujichomeka katikati yao na kuwasalimia ili aonekane kuwa anapendwa sana na kwamba ni mtu muhimu kwao kuliko wengine kumbe hamna lolote na ndiyo maana alimwandaa mpiga picha ili apigwe picha atakazo zitumia kuhadaa watu.
 
hata darasa la vilaza tupu huwa linakuwa na kilaza anayeongoza wenzake!!!Wanaomuona Mwigulu mwigulu ni wa maana ni vilaza.Kisana shule imefungwa kwa kukosa madarasa ya kusomea,wanafunzi wamekua wakisomea chini ya mipama tangu uhuru

Ndio maana Singida ipo nyuma sana kimaendeleo mojawapo ya vyanzo ni hili
 
Huu mtindo wa kujisifia mwenyewe sio mzuri jamani, Pole sana Mwigulu kwa kukosa kiti cha Ubunge 2015. Wananchi wameelimika saiz hata kijijini, Kisana tu CCM hamna chenu tena...!!
 
Back
Top Bottom