ukwelinauwazi
Member
- Nov 24, 2014
- 71
- 91

Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Rais wa Vietnam NdgTruong Tan Sang mapema hii leo walipokutana kwaajili ya mazungumzo kuhusu fursa zilizopo katika kilimo,mifugo na uvuvi katika nchi mbili hizi rafiki

Katika mazungumzo ya pamoja kati ya Rais wa Vietnam na Mh.Mwigulu Nchemba na ujumbe wake,Pande hizi mbili zimekubaliana kushirikiana kwenye uzalishaji wa mbegu bora za mazao na uzalishaji wa samaki hapa nchini,Mbali zaidi wamekubaliana kufungua fursa zaidi kwa wafanyabiashara wa nchi hizi mbili kuwekeza kwenye kilimo,mifugo na uvuvi.

