Mwigulu wako kawaweka pabaya Polisi kwa unyama wake..angalia wanavyoteseka kutoa majibu mepesi
Jeshi la Polisi limeendeleza ngonjera katika tukio la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda (pichani), baada ya kushindwa kutaja watuhumiwa wa tukio hilo la kinyama kama lilivyokuwa limeahidi awali.
Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu, akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, alishindwa kutaja majina ya watu waliohusika katika matukio mbalimbali likiwamo la Kibanda ingawa alisema uchunguzi wake umeanza muda mrefu.
Mngulu akizungumzia tukio la kutekwa na kuteswa kwa Kibanda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka, alisema uchunguzi wa matukio hayo bado unaendelea.
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema amesema upelelezi wa kesi ya kutekwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka bado haujakamilika.
Mbali na Dk. Ulimboka, IGP alisema kesi nyingine zote za aina hiyo pamoja na za mauaji ya watu mbalimbali, akiwemo Padri wa Kanisa Katoliki la Minara Miwili lililopo Mji Mkongwe Zanzibar, Evaristus Mushi (56), uchunguzi wake unaendelea.