Mwigulu Nchemba aamuru afisa ardhi wilaya ya Butiama akamatwe kwa kuuza eneo la mnada

ukwelinauwazi

Member
Nov 24, 2014
71
91
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.Mwigulu Nchemba aagiza afisa ardhi wa wilaya ya Butiama ndg.Clavery Bitabile akamatwe mara moja na vyombo vya dola vichukue hatua kwa kosa la kuuza eneo la mnada wa upili(Mnada wa Mifugo) wa Kirumi uliopo wilaya ya Butiama.

Mbali na kuuza eneo hilo na kutoa hati kwa mtu binafsi wakati tayari eneo hilo la serikali la mnada lilikuwa na hati,Bwana Bitabile amekuwa kinara wa kusababisha migogoro kadha wa kadha katika wilaya ya Butiama na jimbo la msoma vijijini kwa muda mrefu.Moja ya migogoro mikubwa anayotajwa kusababisha ni ule wa shamba la Buhemba(Mikamariro) n.k

Mwigulu Nchemba akitoa agizo hilo,amesisitiza pia vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa haraka ili mnada huo uanze kufanya kazi. Hatua hii ni mwendelezo wa ziara ya Mh.Mwigulu nchemba kukagua maeno mbalimbali yanayohusiana na wizara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Jioni ya leo,Mwigulu atakuwa na mkutano mkubwa wa hadhara Tarime mjini kuzungumza na wananchi kuhusu dira ya wizara yake katika kuimarisha mfumo wa upatikanaji wa pembejeo,ufugaji wa kisasa na uvuvi salama.

mwigulu.jpg

(Picha Mwigulu nchemba akiwa eneo la tukio la mnada wa Upili-Kirumi Butiama.)
 
Makahama ya mafisadi iko wapi?…naanza kuamini polepole Lowasa alisingiziwa kumbe mafisadi wapo hadi level za kijiji
 
Safi pia agizo hilo lifuatiliwe utekelezaji wake...Ila Comrade Mulongo namwamini.
Makahama ya mafisadi iko wapi?…naanza kuamini polepole Lowasa alisingiziwa kumbe mafisadi wapo hadi level za kijiji
ufisadi hausafishwi kwa kukamatwa fisadi mwingine.
 
Safi Sana waziri wangu kwa ufuatiliaji. Lakini sasa mbona Bunda mjini hujaongea na wananchi ulipita tu ukaenda halmashauri ndani ya robo saa ukaondoka.
NJOO UONGEE NA WANACHI WA BUNDA HAWAJATEMBELEWA NA KIONGOZI YEYOTE TOKA MUINGIE MADARAKANI.
 
Mwigulu uje Kilimanjaro kufuta matangazo yako ya kampeni uloandika kwenye Mawe,Miamba,Miti na magari mabovu,Watalii wamepungua sana kwasababu yako,Wanauliza haya mawe ni artificial ndo maana yameandikwa ,njoo futa kabla hatujakuripoti kwa mkuu Wa nchi,
 
wataalam wengi wa ardhi ndio wamekuwa chanzo cha migogoro ya ardhi....

wanawapa mizigo mahakama za ardhi kusikiliza mashauri(case) ambayo mengine yangeweza kutatuliwa na idara ya ardhi.
 
hiyo barabara ya mwanza musoma kuna nyumba ziko maeneo ya kuanzia Lamadi hadi Bunda yamechorwa jina la huyo wazir sijui kama kafuta wakat anapita hapo au kayaacha tu.
 
Hivi kama kimeshauzwa huwa kinarudishwa au inakuaje? Watu kama hawa ni kuwatandika risas mbele ya waandishi wa habari
 
Makahama ya mafisadi iko wapi?…naanza kuamini polepole Lowasa alisingiziwa kumbe mafisadi wapo hadi level za kijiji
Mkuu huko chini ndo kuna madudu makubwa.
Majipu yaliyopitiliza, Matambazi n.k yako huko chini.
Wevyeviti wa Seriakali za vijiji/Mitaa, Watendaji wa kata ni matambazi.
Shida iliyopo hasa vijijini ni kwa wananchi kutokuwa na know how hasa kwenye masuala ya haki zao za Msingi na sheria kwa ujumla. Hivyo baadhi ya watendaji wa serikali katika maeneo haya wamekuwa wakitumia hiyo loophole kuwakandamiza na kuwaonea wananchi. Kuna kisa kilitokea huko Geita mwaka jana kwenye familia moja. Hiyo familia ilitembelewa na mgeni ambaye ni ndugu wa mume wa familia hiyo. Huyo mgeni alikuwa wa jinsia ya kike. Baba wa familia hiyo alikuwa na shughuli zake za uvuvi. Siku moja ameondoka asubuhi kwenda kwenye shughuli zake, huku nyumbani kamuacha mkewe na huyo ndugu yake (mgeni). Majira ya saa saba akarudi nyumbani kwake. Alipofika mkewe kamwambia hapo nyumbani kuna upotevu wa pesa umetokea. zimepotea shilingi laki tatu. Jamaa alipoambiwa hivyo wazo la kwanza ni kususpect huyo ndugu yake mgeni kuwa ndiye atakuwa ameiba hizo pesa. (Kumbuka Mgeni alikuwa na wiki moja hapo nyumbani, na siku zote Mama mwenye nyumba akitoka, walikuwa wakiambatana). Alichokifanya jamaa nikuanza kumuadhibu mgeni kwa tuhuma kuwa yeye ndo kaiba pesa. Alipiga kamvunja mguu then kamchukuwa mpaka ofisi ya mtendaji wa kata baada ya maelezo yake mtendaji wa kata akaamulu awekwe ndani ili asubiri kesho yake kupelekwa polisi. (Note hapo: Mtuhumiwa kapigwa mpaka kavunjwa mguu, bado mtendaji wa Kata kamuweka ndani*). Hii tu inaonyesha jinsi gani mtendaji huyo alivyokuwa incompetent kwani kumpiga tu mtuhumiwa lilikuwa kosa, pili kumvunja mguu kosa jingine. Aliye mtuhumu hakupasa kujichukulia sheria mkononi ya kumpiga na kumvunja mguu. Yeye alimhisi tu kuwa ndo ameiba na hajamkuta na hizo pesa. Tatu kama Mtendaji wa kata angekuwa competent kwenye masuala ya sheria asingeruhusu huyu binti awekwenda kwani alishavunja mguu hivyo angeshauri apelekwe hospitali ili apate matibabu then case ndo iendelee. Pia inawezekana mtendaji wa Kata alikuwa competent ila kapewa rushwa ili amkandamize mtuhumiwa. Kwa jaribu kuangalia namna gani huko chini ndugu zetu wanavyoonewa na watendaji wasio waaminifu. Huku ndo kwenye majipu makubwa makubwa
 
Hivi kama kimeshauzwa huwa kinarudishwa au inakuaje? Watu kama hawa ni kuwatandika risas mbele ya waandishi wa habari
Jiulize hujawahi fanya kosa, ndugu yako, let be specific, baba, mama yako, kaka, dada zako hawajawahi kukosa, wapigwe risasi?
 
Wanapotokea mafisadi zaidi inathibitisha kuwa kumbe hakuwa mmoja jamani CCM no kiwanda kikubwa cha kutoa Mafisadi
 
Back
Top Bottom