Siri yangu
JF-Expert Member
- Jul 22, 2023
- 1,847
- 3,746
Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba, ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kushirikiana na sekretalieti ya maadili kutazama sekta zenye vishawishi vya rushwa wajaze fomu za maadili, badala ya kuangalia wanasiasa zaidi kwakuwa wengi wao wanajipatia fedha zisizo halali.
Mwigulu alitoa agizo hilo leo wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Takukuru unaofanyika mjini Morogoro.
Amesema wapo viongozi wa maeneo ambayo yanashawishika kwa vitendo vya rushwa ili nao wajaze fomu za maadili ili kukomesha kabisa tatizo hilo nchini.
“Wapo watumishi wa maeneo hayo yenye ushawishi wa rushwa wamekuwa wakifanya kazi kwa miaka michache tu lakini wanamiliki mali nyingi, nakutaka kutunga kanuni ambazo zitawafanya wajute watakapopokea rushwa.
“Rais Samia Suluhu Hassan, amekuwa akichukia sana viongozi wa serikali wanaojihusisha na rushwa na ndio maana anapobaini hana undugu, urafiki wala ujamaa amekuwa akichukua hatua kwa yoyote yule,” amesema.
Ameagiza Takukuru kuangalia dosari za kikanuni au sheria zinazochangia kutekeleza majukumu yao kuzipitia na kuziwasilisha mara moja ili ziweze kurekebishwa ili kuleta ufanisi katika utendaji wao.
Imeandikwa na Ashton Balaigwa, Morogoro
Haki:
#NipasheMwangaWaJamii #nipashedigital
Swali langu ni kuwa huyo rais tunaeambiwa hapendi wala rushwa ni yupi ndugu zangu , ni huyu Samia au kuna mwingine?
Naomba majibu yako mwanajf