kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,252
- 16,171
Nilikerwa na uuzwaji wa nyumba za serikali uliofanywa na Mkapa. Mwaka 2005 nilimchagua Rais Kikwete kwakuwa na yeye alionesha dalili za kukerwa pia na uuzwaji wa nyumba zile. Lakini hadi leo anamaliza urais wake nyumba hazijarudishwa. Mwaka 2015 nimekerwa tena na wizi wa escrow, wakati huu tena Mwigulu anaonyesha dalili za wazi za kukerwa na wizi huu na ametangaza nia ya kugombea urais 2015. Mh. Mwigulu anataka kutuaminisha kuwa kama akiwa rais atayakamata majizi yote ya mali za umma. Safari hii sitaki kuamini tena kama mtu mmoja anaweza kufanikisha jambo ambalo halimo kwenye katiba ya nchi na ambalo ni kinyume na mfumo wa chama chake cha siasa. Sera ya kukamata majizi lazima iwe kwenye katiba na iwe ni sera ya chama sio utashi wa mgombea mmoja mmoja. Ndio maana Kikwete kashindwa kuzirudisha nyumba za serikali hata kama alipenda kwakuwa sio sera ya chama chake. Hata Mwigulu akiwa rais hataweza kukamata majizi kwakuwa sio sera ya chama chake, hivyo hatapata uungwaji mkono ndani ya chama chake kutekeleza kile anachokiamini na kutuahidi. Hivyo basi, nguruwe pita sina mkuki mie mwaka huu, style ile ya 2005 ya Kikwete sintainunua tena 2015.