Ni siku hiyo hiyo ya ijumamosi tarehe 15/6/2013 ambayo ilikuwa siku ya kuitimisha kampeini za marudio ya uchaguzi wa Madiwani ktk kata 4 za jiji la Arusha. Mnamo muda wa saa 5 asubuhi, Mwigulu alipotelemka kwenye gari lake baada ya dereva wake kuliegesha sambamba na lango la kuingilia Naaz restaurant, iliyoko mtaa mashuhuri wa Sokoine mkabala na NMB Banki, alipotelemka na kukatiza barabara kuingia NMB. Ghafla badhi ya watu walimuona na kumtambua, na ndipo walipoanza kumzomea. Zomea zomea hiyo ilivuta watu wengi ambao walianza kukusanyika na kuenea hadi Modern Supermarket. Umati mkubwa ulimsubiria atoke Benki ili waendelee kumzomea.
Askari wa Benki kuepusha tafrani na aibu kwa mkuu walimwambia dereva apeleke gari kwenye lango la kuingilia Benki ali akitoka tu apande kwenye gari na atokomee. Hatua hii ilifanikiwa na alipomaliza shughuli zake alipanda kwenye gari na kuondoka.
Watanzania inatupasa tuwe makini sana , tuachane na ushabiki wa vyama. Wote kwa umoja wetu na kwa ustawi wa amani ya nchi tukatae na tumnyoshee vidole mtu ambaye anataka kutuvuruga na kuipeleka nchi kwenye machafuko.
Nafasi ya kuchaguliwa kwa nafasi yoyote ile huwezi kuwalazimisha watu, eti ni lazima wakuchague wewe tu, wapende wasipende. Hata ikibidi ufanye mchezo mchafu wa kutoa maisha ya binadamu wenzio. Si sahihi na si haki mbele ya Mwenyezi Mungu. Kama watu ni wale wale waliokupa au kukuchagua kwenye hiyo nafasi, ujue kuwa pia wanayo haki vile vile ya kukukataa. Na watakapofanya hivyo si dhambi bali ni haki yao.
Watanzania tukiamini na kuhubiri ktk kukubaliwa na kukataliwa, hakika nchi hii itaendelea kuwa na amani milele. Kinyume chake nchi hii tutaiingiza kwenye machafuko kutokana na upuuzi wa watu wachache wanaofikiri kuwa wana mkataba na Mwenyezi Mungu wa kutawala milele. Kila kitu ktk dunia kina ukomo wake, nami nikiangaza macho yangu mbele naona ukomo wa CCM, kikipisha mfumo mwingine wa utawala, ambao nao utafika mwisho wake na kupisha mwingine huku Tanzania ikiendelea kuwepo. Kwa binadamu aliyezaliwa na mwanamke hawezi kupingana na falsafa hii. Nawasilisha.