Mwigulu afyeka vigogo waliolamba Bilion 5.7. Sasa kupandishwa kizimbani

ukwelinauwazi

Member
Nov 24, 2014
71
91
1937162_453755028160064_4068537352430988619_n.jpg
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi akiwasili kwenye mradi uliodumaa wa Ujenzi wa machinjio ya kisasa wa ranchi ya Ruvu mapema hii leo.
12508993_453755078160059_4660145398233805944_n.jpg
Sehemu ya jingo lililobaki kama Gofu mara baada ya kutelekezwa na Uongozi wa Bodi ya ranchi za Taifa(NARCO)
12508843_453755034826730_2024804202422212096_n.jpg
Mwigulu Nchemba akishangaa namna mali hii ya Umma ilivyotekelezwa.
12508820_453755104826723_8954297844331159293_n.jpg
Mwigulu akiwa na jopo la wataalam wakiendelea kutathimini hasara iliyojitokeza kutokana na ujenzi mbovu wa machinjio ya kisasa hapa Ruvu.
1510846_453755131493387_1363546417355435493_n.jpg
Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Chalinze Mh.Ridhiwani wakisikiliza kwa makini sababu zilizopekea jingo hilo kutelekezwa.Anayetoa maelezo wa mwisho kushoto ni msimamizi wa ranchi hiyo Ngd.Bwire.

12508948_453755071493393_1263240942465636249_n.jpg
Sehemu ya jingo ikiwa imetelekezwa bila kuendelezwa kiujenzi.
12509693_453755114826722_5912636982326832694_n.jpg
Hii ni sehemu ya ukuta wa jingo hilo ambao umekatika kutokana na kukaa muda mrefu bila kuendelezwa.
12494821_453755171493383_1654150081091013370_n.jpg
Mwigulu Nchemba akiendelea kupewa maelezo ya kina kuhusu ubadhilifu uliojitokeza kwenye ujenzi huu.
1422436_453755341493366_4758037396091756872_n.jpg
Mh.Ridhiwani kikwete Mbunge wa Chalinze akitoa malalamiko yake kwa Waziri.Mwigulu Nchemba kuhusu kukosekana kwa mahusiano mazuri kati ya wamiliki wa ranchi na wananchi wanaozunguka ranchi ya Ruvu.
12439217_453755348160032_5274315773359029135_n.jpg
Kwa mbali hili ndio jengo la machinjio ya kisasa lililokuwa linajengwa na hatimaye kutelekezwa bila kuendelezwa tangu mwaka 2010.
12417961_453755598160007_6181672878037564076_n.jpg
Mh:Mwigulu Nchemba akiteta jambo na viongozi wanaohusika na kulinda baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa kwaajili ya ranchi hiyo ya kisasa.
10151378_453755404826693_6806684662362983672_n.jpg
Mh;Mwigulu Nchemba akioneshwa baadhi ya Ng'ombe wanaopatikana kwenye ranchi hiyo.
1929109_453755451493355_3260270447424066333_n.jpg
12509642_453755468160020_7367273123481285543_n.jpg
Mwigulu Nchemba akiwa kazini kwenye shamba la Mifugo la Ruvu hii leo.
12509036_453755504826683_6556331783109551281_n.jpg
11237217_453755581493342_8296334689626737052_n.jpg
Mwigulu Nchemba akidadisi utunzaji wa maji ya Mifugo inayopatikana ndani ya ranchi ya Ruvu.



Wakati Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya Rais.J.P.Magufuli kwa speed yake ya uchapa kazi,Mawaziri wake pia wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli za maendeleo ya Nchi yetu.

Hii leo,Mh:Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi amefanya ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua ujenzi wa majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.

Katika hali ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu,Mwigulu Nchemba amekutana na ubadhilifu wa Bilioni 5.7 ambazo zilitolewa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo,Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama ilivyokusidiwa.

Waziri huyo wa kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010 bila kuendelezwa,Sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa ni kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO(kampuni ya usimamizi wa ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mh:Mwigulu Nchemba ambaye baada ya kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi hiyo aliamua ifuatavyo.

Kwanza,Mwigulu Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo la ranchi ya ruvu.

Pili,Mwigulu Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi mkuu wa ranchi za Tiafa kwa kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake.

Pia,waziri huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria,wahusika wote walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo usifanikiwe wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.

Mwisho,Nchemba amewaagiza wataalam wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7 wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na fedha zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.

Sambamba na hatua hizo,Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya nchi yetu,Mbali na hapo,serikali ya Magufuli haitakuwa tayari kuona mali ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna watanzania wanaweza kusimamia mali hizo na kuziendeleza.
 
Mbona ya bandari yalimshinda?

Waliokuwa na dhamana ya kujenga uwanja wa Ally Hassan Mwinyi kule Tabora nao wanachukuliwa hatua gani?
Watu wapo na ranchi ya taifa wewe unaleta mambo ya uwanja wa ccm,kama huna hoja vema ukae kimya kamanda watu wapo kazini wewe unakodoa mimacho kutafuta makosa ambayo huyapati unaishia kulazimisha
 
Ndugu zangu UKAWA na CDM mm juzi nilitofautiana sana na wenzangu eti hawajaona alichokifanya Mh. Rais au serikali yake hadi sasa, nikawaambia, sio kila jambo ni kupinga au kudhihaki hata kama ni jambo jema, huo sio upinzani bwana, akifanya vizuri mpongeze, akikosea mkosoe...!! sasa kupinga kila kitu ndo nini sasa?

mm ni CDM ila nakubaliana na utendaji huu wa serikali maana mm binafsi ndio niliokuwa nautarajia...
 
Ndugu zangu UKAWA na CDM mm juzi nilitofautiana sana na wenzangu eti hawajaona alichokifanya Mh. Rais au serikali yake hadi sasa, nikawaambia, sio kila jambo ni kupinga au kudhihaki hata kama ni jambo jema, huo sio upinzani bwana, akifanya vizuri mpongeze, akikosea mkosoe...!! sasa kupinga kila kitu ndo nini sasa?

mm ni CDM ila nakubaliana na utendaji huu wa serikali maana mm binafsi ndio niliokuwa nautarajia...
chadema hapo katokea wapi?
 
Ile kamati ya bunge iliyoenda pale wakati ile kwa mbwembwe nyingi ripoti yake iko wapi? Au nao waliondoka na bahasha???
 
kwakweli nchi hii ina uozo sana. nasikitishwa na wanaodai eti kufukuzafukuza watumishi jwa jpm na mawaziri wake ni kukurupuka!!

tujiulize watu wamesababisha ufujaji wa mafedhaa kibaoo na bado wapo tu wamerelax!! makontena yametoroshwa lakini wao kama wahusika walipiga kimyaaa!! kwa maana wanajua na wameridhika watimuliwe ili wajue wameleta umaaikini nchini bilioni 5 kupotea kwa uzembe wa mtu 1, sio kitu kidogo.

ndalichako nakusubiri kwenye elimu waalimu ni jipu zaidi ya wanafunzi
 
Mbona ya bandari yalimshinda?

Waliokuwa na dhamana ya kujenga uwanja wa Ally Hassan Mwinyi kule Tabora nao wanachukuliwa hatua gani?
Ushabiki wa vyama vya siasa kweli umetufanya watanzania kupoteza uzalendo wetu, sasa wewe utaki kukubali anachofanya Mwigulu Nchemba hata kama kina maslahi na taifa kisa yupo CCM.
 
Yap, kwa vile hii ni serikali mpya kabisa, labda si ajabu viongozi wake wakishangaa uzembe uliofanyika awamu iliyopita ambao ni dhahiri kuwa ulifanywa na serikali ambayo haikujali kabisa maslahi ya taifa. Lakini tusishangae pia kama viongozi haohao "wapya" wakatetea kuwa utawala uliopita umelifanyia taifa "mengi mazuri" hivyo inatakiwa kuenziwa! How ironic!

Tulichobakiwa nacho sasa ni kuwa wavumilivu na kuamini kuwa hawa watu sasa "wameokoka"; wamebadilika. Hivyo hiyo shangaa yao kwa madhambi tuliyoyazoea ni halisi (genuine) na kwamba sasa wameamua kwa dhati kabisa kuyashughulikia.
 
Mbona ya bandari yalimshinda?

Waliokuwa na dhamana ya kujenga uwanja wa Ally Hassan Mwinyi kule Tabora nao wanachukuliwa hatua gani?
Wenye CHADEMA walishasema hakuna dhambi kuipongeza serikali kama inafanya vizuri.

Wewe umeendelea kuuvaa ujinga wa unyumbu.

Wenye CHADEMA wameanza kubadilisha gear angani wakati wewe bado unashangaa ardhini.

Badilika!
 
Back
Top Bottom