Mwezi utakuwa jirani na Sayari tano alfajiri

Umeweza kutambua Sayari ngapi kati ya tano hizi?

  • Mustarii (Jupiter)

    Votes: 2 66.7%
  • Mirihi (Mars)

    Votes: 3 100.0%
  • Zohali (Saturn)

    Votes: 3 100.0%
  • Zuhura (Venus)

    Votes: 2 66.7%
  • Zebaki (Mercury)

    Votes: 2 66.7%
  • Sikuweza kutambua hata moja

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    3
  • Poll closed .

njiwaji

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
285
206
Katika siku zijazo kuanzia sasa hadi tarehe 7 Februari Mwezi utakuwa jirani na Sayari tanzo tunazoweza kuziona kwa macho moja kwa moja. (Angalia picha ya anga ya alfajiri iliyoambtishwa)

- Mwezi upo jirani na Mustarii (Jupiter) leo usiku hadi alfajiri.

- Baada ya siku chache, alfajiri ya Februari 1 na 2, Mwezi utakuwa jirani na Mirhi (Mars)

- Februrari 3 na 4 Mwezi utakuwa jirani na Zohali (Saturn)

- Na mwisho, siku za Februrari 6 na 7 alfajiri Mwezi utakuwa jirani na Zuhura na Zebaki ambazo zipo jirani na upeo wa mashariki kabla ya Jua kuchomoza.

Tumia nafasi hii kuweza kutambua Sayari mbali mbali kwa kutumia nafazi zake zitakapokuwa jirani na Mwezi katika siku zijazo wakati wa alfajiri. Fuata picha iliyambatishwa kurahisisha utambulizi wa Sayari za Musharii (Jupiter), Mirihi (Mars), Zohali (Saturn), Zuhura (Venus) na Zebaki (Mercury).

Mustarii na Zuhura zinan'gaa kuwa uangavu mkali kwa hiyo hutakosa kuzitambua.

Mirihi hun'gaa kwa mwanga mwekundu. Lakini kuwa macho kuna nyota angavu jirani na Zohali iitwayo Antares, ambayo inang'aa kwa uwekundu kama Mirihi.

Sayari hutaofautiana na nyota za kawaida kwa kutofautiana kun'gaa kwa vile Sayari hun'gaa bila kumeremeta wakati nyota humeremeta. Kwa hiyo utaweza kutofautisha kati ya Sayari na nyota kawaida.

Mwezi jirani na sayari tano alfajiri siku zijazo.png

Ukiangalia mandhari hii angani mwenyewe kwa macho yako, utatambua kuwa Sayari zote zimejipanga angani kwa mstari mmoja. Na hata Mwezi husogea angani kwa kufuata msatari huo.

Hii itawashangaza watu, lakini inaelezeka kwa kuelewa kwamba Sayari zote na Mwezi zipo katika bapa moja nyembaba ambayo huunda Mfumo wa Jua. Kwa hiyo kwa wakati unaziangalia Sayari na Mwezi kutoka hapa kwetu Duniani, bapa hiyo ya Mfumo wa Jua umejiweka wima anagani na Sayari na Mwezi zipo katika bapa hiyo.
 
Unamaanisha sitahitaji telescope kuziona?
Ndiyo. Zile angavu sana kama Mushtarii (Jupiter) na Zuhura (Venus) utazitambua kwa urahisi. Mirihi inauwekundu. Kwa kutumia nafasi za Mwezi angani siku hadi siku utaweza kutambua Sayari zote tano zinaoonekana kwa macho tupu.

Na kwa ujumla Syari zinan'gaa moja kwa moja bila kumeremeta kwa hiyo utaweza kutofautisha na nyota za kawaida zinazomeremeta.
 
View attachment 319864

Ukiangalia mandhari hii angani mwenyewe kwa macho yako, utatambua kuwa Sayari zote zimejipanga angani kwa mstari mmoja. Na hata Mwezi husogea angani kwa kufuata msatari huo.

Hii itawashangaza watu, lakini inaelezeka kwa kuelewa kwamba Sayari zote na Mwezi zipo katika bapa moja nyembaba ambayo huunda Mfumo wa Jua. Kwa hiyo kwa wakati unaziangalia Sayari na Mwezi kutoka hapa kwetu Duniani, bapa hiyo ya Mfumo wa Jua umejiweka wima anagani na Sayari na Mwezi zipo katika bapa hiyo.
Hichi ni kipindi kizuri kuomba dua yoyote ile mbaya au nzuri itakuwa tu. Elimu yangu hiyo umeipata wapi mkuu?
 
Ndiyo. Zile angavu sana kama Mushtarii (Jupiter) na Zuhura (Venus) utazitambua kwa urahisi. Mirihi inauwekundu. Kwa kutumia nafasi za Mwezi angani siku hadi siku utaweza kutambua Sayari zote tano zinaoonekana kwa macho tupu.

Na kwa ujumla Syari zinan'gaa moja kwa moja bila kumeremeta kwa hiyo utaweza kutofautisha na nyota za kawaida zinazomeremeta.
Nashukuru sana kwa ufafanuzi.Leo nimekesha nikiisubiri alfajiri.Nimebahatika kuiona Jupiter karibu na Mwezi kwenye saa kumi na robo hivi. Mwanga wake ulikuwa mkali kuliko nyota zilizokuwapo karibu na pia ilionekana kubwa kuliko nyota na mwanga wake haukuwa ukicheza. Nimefurahi sana.
 
Mkuu .... kuna kifaa chochote kinachoweza kutumika kuangalia kwa ufasaha au zinaonekana vizuri with bare eyes
 
Najiuliza maswali mengi Dunia duara pakuingilia wapi. Jua nyote na mwezi ziko wapi na mengine mengi nisaidie simple geography book nijikumbushe kufuta giza
 
Back
Top Bottom