Mwenziyo unanikosha!

[QUOTE=Yakuonea;4019268]

Beti nilimtumia, kumpa yeye nasaha
Hekima nikajazia, aepuke ya karaha
Awache kung'ang'ania, ajenge yake staha
CHOVEKI ANISHANGAZA, KWA PENZI KUNG'ANG'ANIA

Beti zangu hakujibu, sijui hata kwa nini
Labda ni zake ghadhabu, kwa vile bado kuwini
Au kashikwa aibu, binti kutomthamini
CHOVEKI ANISHANGAZA, KWA PENZI KUNG'ANG'ANIA

Na hataki shaurika, eti mrembo ni wake
siku nazo zakatika, aishi kivyake vyake
uzee utamfika, bila hata ya mwenzake
CHOVEKI ANISHANGAZA, KWA PENZI KUNG'ANG'ANIA

SINDANO MWANA WA GANZI (SMG)
KIJIJINI TONGOLEANI
[/QUOTE]

Nzi kufia dondani!

Nzi kufia dondani, msemo waujulia?
Narudi kwako mtani, wahenga kukumbushia
Mapenzi ni upofuni, kupenda kweli wajua?
Halali nakujulia, nzi kufia dondani!

Ni mengi umeyahoji, na hapo nikajulia
Ki mapenzi si mwnyeji, mtani nimegundua
Hunacho pia kipaji, mapenzi kufahamia
Halali nakujulia, nzi kufia dondani!

Zaidi ya maradufu, kwa kina kuelezea

Nahisi wewe kipofu, mapenzi kujionea
Umpendaye hukifu, kwa dhati nakuminyia
Halali nakujulia, nzi kufia dondani!

Kigumu kwako ni kipi, mtani ninashangaa
Mgongo kweli simpi, spidi naongezea
Ladhaye yashinda pipi, mapenzi nasubiria
Halali nakujulia, nzi kufia dondani!

Tano zilizo kamili, ni beti namalizia
Bibie nina mjali, hakuna afanania
Ya kwanza, siyo ya pili, nambari ashikilia
Halali nakujulia, nzi kufia dondani!

Kijana Bin M'bichi

Nzi kufia dondani!

Nzi kufia dondani, msemo waujulia?
Narudi kwako mtani, wahenga kukumbushia
Mapenzi ni upofuni, kupenda kweli wajua?
Halali nakujulia, nzi kufia dondani!

Ni mengi umeyahoji, na hapo nikajulia
Ki mapenzi si mwnyeji, mtani nimegundua
Hunacho pia kipaji, mapenzi kufahamia
Halali nakujulia, nzi kufia dondani!

Kijana Bin M'bichi

Mtani nitarudi.....
 
PENZI TATA KWELI TATA

Choveki mtani wangu, kwako ninarudi tena
Si mpya mada yangu, ulosema nayakana
Mimi mjuzi wa tangu, mapenzini si wajana
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Mapenzi kweli ajali, ajali iso na kinga
Hata wale marijali, waweza patwa ujinga
Duni ikawa akili, penye hoja wakapinga
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Waonyesha limbukeni, mapenzi bado kujua
Tena kwako ni mageni, na sasa yakusumbua
Hali yako iko duni, moyoni unaugua
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Ni lini utazinduka, kwa mola nakuombea
Ona ulivyo dhofika, mapenzi yakuchezea
Tatizo la kwako kaka, binti wamshobokea
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Na kwangu sio mageni, mapenzi ninakwambia
Ninae wangu mwandani, wa pwani kwa asilia
Si mtu wa kisirani, upole yake tabia
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Kutwa kuchwa twapeana, sasa nakusimulia
Twajua kuridhishana, kwa mia asilimia
Si usiku si mchana, penzi twalifurahia
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Mtani upo ta'buni, kweli nakuhurumia
Tatizo lako huoni, na sifa wamiminia
Binti yule nuksani, mbeleni utaja jutia
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Na wacha kudanganyia, ladhae yashinda pipi
Penzi hajakupatia, watulaghai kwa lipi?
Mtani wajisumbua, pale penzi halilipi
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Wazidi kutushangaza, hujui usipopendwa
Kwa mema unamjaza, ila bado unatendwa
Fanya hebu kutangaza, "penzile" umelishindwa
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Penzi tata penzi gani, ona hizo hati hati
Umebaki ujivuni, binti apaishwa chati
Shida yote hiyo nini, yeye kwako hana dhati
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Na wengi tumeshauri, ila hutaki sikia
Umejawa na kiburi, ya kwetu wapuuzia
Kaa chini tafakari, muda utaujutia
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Kwa hoja tunazojenga, vipi hutaki kuona
Ni vyema ukamtenga, sema mwambie hapana
Binti huyo wa kuringa, kaka mtaja shindwana
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Na hapa nasimamia, ila hoja zingatia
Lengo si kukusakama, ni mema nadhamiria
Nae mola wa rehema, akupe yaso kadhia

...

Roulette, nafikiri shairi zuri. unaweza kutumia kunipa mifano nilikuuliza kwenye thread yako
 
Last edited by a moderator:
PENZI TATA KWELI TATA

Choveki mtani wangu, kwako ninarudi tena
Si mpya mada yangu, ulosema nayakana
Mimi mjuzi wa tangu, mapenzini si wajana
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

Mapenzi kweli ajali, ajali iso na kinga
Hata wale marijali, waweza patwa ujinga
Duni ikawa akili, penye hoja wakapinga
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

…….
Na hapa nasimamia, ila hoja zingatia
Lengo si kukusakama, ni mema nadhamiria
Nae mola wa rehema, akupe yaso kadhia
PENZI TATA KWELI TATA, NI LINI UTAZINDUKA

SINDANO MWANA WA GANZI (SMG)
KIJIJINI TONGOLEANI

Mpendwa Yakuonea (Mtani),

Kwako weye penzi tata, kwangu miye nimependa
Nahisia hujapata, ambaye unampenda
Kwangu miye siyo tata, mtani nimeshapenda
Kwako weye penzi tata, kwangu miye nimependa!

Mtani unanihoji, mapenzi hujajulia?
Sihataji hata jaji, mpenzi kumjulia
Kupenda kama kipaji, mwenyezi anajalia
Kwako weye penzi tata, kwangu miye nimependa!

Mapenzi kama ajali, mtani umeshanena
kupenda tena muhali, kimapenzi mi mtwana
kwangu miye kama zali, kwa huyu wangu kimwana
Kwako weye penzi tata, kwangu miye nimependa!

Ningali ninasubiri, ujuwe wangu mtani
Ashika tena nambari, amenijaa kichwani
nasema siyo stori, ukweli wangu moyoni
Kwako weye penzi tata, kwangu miye nimependa!

Wakatabahu tamati, sijampata mwengine
Sihitajii kamati, juweni nanyi wengine
Maneno mengi siteti, sitompenda mwengine
Kwako weye penzi tata, kwangu miye nimependa!

Wakatabahu waraka,

Kijana Bin M-bichi
 
Mpendwa mwana Fulani,

Kumbuka kuna korona;

Nanianzia salamu, binti mwana Fulani

Ingawa nina ugumu, ungali mwangu moyoni

Kwangu weye ni muhimu, hujatoka akilini

Kumbuka kuna korona, utulizane nyumbani

Kipindi hichi kigumu, tulia mwana fulani

Utoke kama muhimu, vinginevyo kaa ndani

Unitafute kwa simu, nitakuwa mlangoni

Kumbuka kuna korona, utulizane nyumbani

Najuwa kuna ugumu, muda wote kuwa ndani

Sitaki upate sumu, Korona ni mtihani

Kama kutoka kwa zamu, kumbuka wangu mwandani

Kumbuka kuna korona, utulizane nyumbani

Kukuona nina hamu, ninaumia moyoni

Lakini kuna ugumu, sipendi utoke ndani

Ni wako miye fahamu, hujatoka akilini

Kumbuka kuna korona, utulizane nyumbani

Tamati natoa humu, ungali mwangu moyoni

Kwangu miye we muhimu, kumbuka mwana Fulani

Ninaupata ugumu, kukuagia moyoni

Kumbuka kuna korona, utulizane nyumbani

Wakatabahu,

Kijana Bin M’bichi

Mei , 2020

(Mwaka wa Korona)
 
Mpendwa,

Ilikuwa Aprili, tarehe naikumbuka

Kukujuza sina hali, kwako weye nimefika

Nikaomba ufadhili, kwa dhati nikatamka

Ilikuwa Aprili, ningali ninakumbuka!

Kwa kina nilikujuza, kwako weye nimefika

Na tena sikujikuza, kwa dhati niliandika

Na lugha nikaiuza, kutaka kueleweka

Ilikuwa Aprili, ningali ninakumbuka!

Nilitoa ya moyoni, wakati nikiandika

Sikuuleta utani, kwako uliyeumbika

Kwa lugha ilo laini, yenye hadhi na mipaka

Ilikuwa Aprili, ningali ninakumbuka!

Ningali nasubiria, tena pia sijachoka

Pia tena sijaoa, ungali wasubirika

Wazazi wanaumia, ni lini nitafunguka?

Ilikuwa Aprili, ningali ninakumbuka!

Tano nasema tamati, kwa leo ninatamka

Nasubiria bahati, barua utaamdika?

Ningali ni mahututi, kimapenzi natamka

Ilikuwa Aprili, ningali ninakumbuka!

Wakatabahu.

Akupendaye,

Kijana Bin M bichi
 
Wapata tabu ya nini?

1.Salamu natanguliza,kwa barubaru choveki
Hakika utajiponza, simulizi zitabaki
Wapata tabu ya nini?

2.Wazee umewachosha,hebu kaa tafakari
Wajukuu wangetosha,kuwapa yao fahari
Wapata tabu ya nini?

3.Keshasema hakutaki,lipi sasa wasubiri
Wapo malaki malaki,wanashindana uzuri
Wapata tabu ya nini?

4.Tena wapo mabanati,nawajua kwelikweli
Ungeipata bahati,ukathibiti kauli
Wapata tabu ya nini?

5.Mwenzako anae wake,alomshika kauli
Asemapo jambo lake,tayari kata kibali
Wapata tabu ya nini?

6.Subira yavuta heri,ila si kwa jambo hili
Hacheleweshi kahari,panapo jambo la kweli
Wapata tabu ya nini?

7.Machweo yanaingia,ujana unatamati
Yakupasa kutambua,huu ndo wako wakati
Wapata tabu ya nini?

8.Uzee ni mkakati,kuvuna ulichopanda
Usije kutahamaki,mebaki peke kitanda
Wapata tabu ya nini?

9.Beti kenda nimepanga,uchukue tahadhari
Ni wakati wa kujenga,na si kuleta stori
Wapata tabu ya nini?

Swahibu Mlokole
Tabata Dar es salaam
09/12/2022.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom