FirstLady1
JF-Expert Member
- Jul 29, 2009
- 16,789
- 5,420
Waswahili wanasema Mtu akipata Pesa ndo utamjua vizuri, ukipata matatizo ndo utamjua mwenzi wako vizuri lakini pia mwenzi wako akipata matatizo ndo unapata fursa ya kumjua vizuri kwa namna atakavyokabiliana na tatizo lake.
Sasa je ikitokea mwenzako kapata matatizo ya kikazi,kifedha, kifamilia,ugonjwa alafu ukagundua kwamba anaamini sana ushirikina na ndo kimbilio lake la kwanza kutafuta utatuzi wa tatizo lake utafanyaje?! Hapo ni baada ya kuishi ama kuwa kwenye mahusiano kwa muda mrefu miaka miwili na hukuwahi kujua msimamo wake kuhusu hayo maswala.
mafame Lizzy Upo jamani miaka mingi imepita sikuoni hapa ndani