Mwenza wa maisha (mume) anahitajika!

Toa specification basi:
Cc ngapi, km, make, model, transimision type nakadhalika.
 
ungesema ulivyo
mnene?
kabila gani?
shepu aina gani?miss tz?miss bantu?miss namba nane?namba tisa?

Nimekuelewa The Boss, unajua kueleza kila kitu inaweza kuwa tabu kidogo, ila kwa aliye na nia hizo sifa tajwa zinaweza kumpa picha na hatimae tukakubaliana tuonane ili kupata uhakika. Karibu kwa mawazo zaidi!
 
Daah! sifa zoote ninazo isipokuwa hapo kwenye kitambi! hebu nipe muda ntarekebisha hii ila ntabakiza cha kuvalia mayenu! Kama pouwa twende kazi.
 
ishu ya dini bana inafanya nikukose. Can't u think otherwise kuhusu hiyo ishu ya dini?
Hizo degree mbili ni za nini, I mean specialization i.e sociology, education, economics...
 
Habari zenu wanajamii.
Jamani maisha ni safari ndefu na inahitaji uvumilivu na ujasiri. Nimetumia ujasiri wangu kwa kujitokeza katika jukwaa hili ili kuweza kupata mwenza ambae atakuwa mume kama Muumba akibariki. Kwa aliye na nia ya dhati haswa naomba tuwasiliane kwa private message.

Sifa zangu
Umri: Miaka 30
Umbo:Ni wa kawaida sana, na kwa wale wanopenda makalio makubwa, mimi sina jamani, ni bora kuwa mkweli!
Urefu: Centimeter158
Rangi: Maji ya maharage
Elimu: Degree mbili
Kazi: Muajiriwa wa serikali
Dini:Islam

Sifa za Mtarajiwa
Umbo: asiwe na kitambi kwa kweli
Urefu: itakuwa vyema kama akinizidi maana isije leta zahma
Rangi: yeyote
Elimu: Degree
Kazi: Ni muhim maana maisha ni magumu sana
Dini: Islam, ila uwe hujaoa!

Najua kunawatakoleta mzaha, ni kawaida sana kwenye jamii. Nipo tayari kwa maswali mtakayoyauliza. Karibuni!

Nasreem, mimi nimefurahishwa na namna unavyojibu maswali, nimevutiwa na nina sifa zote kasoro nimeoa. Ila ningeomba tuwe marafiki tu.. kwani nimevutiwa kuwa na rafiki kama wewe.Kama huna tatizo na hili ni PM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom