Mwenyekiti wangu wa CCM na Rais wa JMT, Dkt. Magufuli tafadhali mkemee haraka Cyprian Musiba

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,926
Nianze tu kwa Utangulizi wangu kwa kusema kwamba nimewahi kuishi sana na Wajita ambao watokao Mkoani Mara ( Musoma ) sehemu nyingi mno na sitosahau jinsi aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan na baadae akaenda kuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Marehemu Mufungo Silas Mujaya ( ambaye ni Mjita halisi ) alivyonilea vyema, Kiupendo na kuniongoza vyema Kimaadili na Kimaisha hasa nilipokuwa masomoni huko Uganda mwaka 1996 hadi 2002.

Kupitia Yeye ( Marehemu Balozi Mzee Mujaya R.I.P ) niliweza sana kuwajua Wajita kwani mara nyingi nikiwa likizo pale alipokuwa akiishi Kololo na baadae Muyenga jijini Kampala nilikuwa nikikutana mno na Wajita kadhaa na nakumbuka kuna muda hata alikuwa akipenda Kuongozana nami hadi Kijijini Kwake huko ' Ujitani ' Musoma kwakuwa alitokea kunikubali sana hivyo nilizidi kuwajua vyema Wajita.

Kilichonifanya nianze na utangulizi huo mdogo tu ni kwamba hadi hivi sasa najiuliza huyu Mtu aitwae Cyprian Musiba ni Mjita kweli au labda huyu atakuwa ni Mhutu? Kwa sifa zote ninazozijua za Wajita sijaona hata moja ambayo Cyprian Musiba anayo sana sana namuona kama ni Mtu mwenye utindio wa akili fulani hivi na anahitaji tiba ya haraka.

Wajita ni Watu makini, werevu, wastaarabu, wacha Mungu mno halafu hakuna kitu ambacho wanakichukia kama fujo au kuchochea chuki na majungu katika Jamii sifa ambazo tokea nianze kumjua Cyprian Musiba tokea alipokuwa Mtangazaji wa ' hovyo hovyo ' Magic FM na Channel Ten bado nazitafuta Kwake na mpaka leo sijabahatika kuziona labda Shetani anaweza akawa anazijua vyema.

Mheshimiwa Mwenyekiti wangu wa Chama changu ninachokishabikia cha CCM na pia Rais wangu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( JMT ) Dr. Magufuli nadhani kama kuna Mtu ambaye ndiyo ataweza kuzidisha ' chuki ' ya Wananchi ama Kwako au hata kwa Serikali yako hii ya awamu ya Tano basi ni huyu Cyprian Musiba.

Mheshimiwa Mwenyekiti na Rais wangu Mimi GENTAMYCINE sijawahi kuwa ' Mnafiki ' na desturi yangu siku zote huwa ni ' Kunyoosha ' tu maelezo bila Kupepesa macho, Kutikisa masikio na Kumung'unya maneno hata kama nitakayoyasema yanaweza yakawaudhi Watu wa Chama changu ninachokishabikia cha CCM.

Cyprian Musiba leo ametaja majina kama Kumi ( 10 ) hivi ya Watu ambao amedai kuwa ana uhakika nao kuwa Wao ndiyo ' Tishio ' kwa Usalama wa Taifa wa nchi hii na Mimi pia nadiriki kusema hadharani kuwa hao Watu wake Kumi ( 10 ) aliowataja hakuna hata mmoja ambaye ni ' Tishio ' kwa Usalama wa nchi ila kama nikiulizwa leo kuwa nadhani nani anaweza akawa si tu ' Tishio ' kwa Usalama wa Taifa wa nchi bali pia akawa ni ' Kirusi ' Kikubwa ndani ya Chama cha Mapinduzi basi kwa Vigezo vyangu haraka sana nitamtaja Cyprian Musiba.

Hapo juu nimesema kwamba moja ya sifa ' Mama ' ya Wajita wote huwa ni uwezo wao mkubwa wa akili waliobarikiwa ila kwa Kitendo cha Cyprian Musiba kusema kuwa kuna mmoja wa Watu katika kile ' Kikosi ' chake anatumika na FBI hakika nimetokea ' Kumdharau ' pengine hata ikitokea tu nikaonana nae Mbinguni pia nitajitahidi nimkwepe kwani ataweza kuniambukiza Ungumbaru / Ujinga wake hata tukiwa huko.

Hivi ina maana Cyprian Musiba pamoja na kujifanya amesoma, ana hela na Kampuni ameshindwa kujua tofauti ya Kimajukumu kati ya Federal Bureau of Investigation na Central Intelligence Agency? Tangia lini FBI wakaratibu ' machafuko ' ya nchi zingine? Angesema kuwa CIA inatumika kidogo ningemwona ana akili kwani katika ' machafuko ' mengi duniani ambayo Marekani inahusishwa moja kwa moja huwa yanaratibiwa 100% na CIA ambao mara nyingi hujikita na masuala ya nje ya Marekani na kamwe si FBI.

Huyu Cyprian Musiba wakati analishwa ' Sumu ' ya Kuwadanganya Watanzania ina maana hata Yeye tu alishindwa kuhakiki vyema ' data / facts ' zake ili basi angalau hata akiwa anaongea na Press awe ana uhakika na anachokisema? Na nimewashangaa mno pia na Waandishi wa Habari waliokuwepo kwa kushindwa hata tu ' Kumtega ' Jamaa na kumuuliza kwanini ameihusisha FBI na siyo CIA katika maelezo yake?

Mheshimiwa Mwenyekiti na Rais Dr. Magufuli hebu fuatilia vyema ni nani ambaye huwa anamtumia huyu Cyprian Musiba kuzungumzia mambo ya nchi / taifa kwa mgongo wa Chama chako cha CCM kwani unaweza kudhani anakusaidia lakini nikuhakikishie huyu ndiyo Kwanza anakuharibia na pia anatupa sana Kazi Sisi akina GENTAMYCINE ambao kutwa huwa tunakupigania na kukutetea humu na mitaani. Ikiwezekana apigwe ' stop ' mapema mno kuzungumza hovyo kwani hakuna anachokijua na sana sana anakiharibia Chama chetu cha CCM kwa kupenda Kwake ' Kukurupuka ' bila ya Kujipanda kwa ' Hoja ' zenye mantiki na mashiko.

Mwisho kabisa nimalizie tu kukuambia Mheshimiwa Mwenyekiti na Rais kuwa kama huyo Cyprian Musiba anadhani labda hao Watajwa wake Kumi ( 10 ) ndiyo threat to the National Security ya nchi hii basi atambue ya kwamba Watu ' Tishio ' halisi wa nchi hii na usalama wake na hata Kwako Wewe pia ( Mwenyekiti na Rais ) wapo ndani ya CCM yenyewe kama Chama na wengine wakiwa humo humo ndani ya Serikali yako unayoingoza sasa ila ' wanafichwa ' kwa mgongo wa ' Wapinzani ' wa nchi hii huku wakikujaza upepo ( namaanisha wakikudanganya ) kusudi uwaamini, uwapende na uzidi kuwapa madaraka na malengo yao yatimie.

Siko hapa kuwatetea hao Watajwa wake Kumi ( 10 ) japo nakiri kuwa karibia wote ni Watani zangu Kisiasa Wao wakiwa ni CHADEMA na Mimi nikiwa CCM ila ninachokitaka tu hapa ni haki na ukweli kusudi isije ikawa tunataka kutumia ' udhaifu ' au ' upole ' wa Wapinzani kuhalalisha ' Uonevu ' dhidi yao halafu mwisho wa Siku nchi hii aliyoiacha vyema Hayati Baba wa Taifa Nyerere na Mzee Karume ikatumbukia katika ' machafuko ' mabaya kisha tukajikuta pabaya na kuanza tena upya Kujijenga. Naomba ikiwezekana kuwe na majadiliano ya kina juu ya hali ya ' Kisiasa ' nchini Tanzania kwani kwa mwendo huu anaoenda nao Cyprian Musiba naogopa huko mbele tunaweza kuja ' Kutafutana ' na kuharibu kabisa taswira ya Mama Tanzania yetu.

GENTAMYCINE nimemaliza rasmi kutoa yangu ya moyoni na niseme tu Kwako Mwenyekiti wa Taifa na Rais wa JMT kwamba the ball is now in your court hivyo kuwa makini sana na Watu ambao wanajifanya wanakusaidia kumbe wanakuumiza na kukuharibia kabisa mipango yako mema uliyopanga kwa nchi hii unayoiongoza.

Nawasilisha.
 
Waandishi wa habari wa nchi hiii ni 'VILAZA' wanawezaje kumwacha mtu akiongea vitu kama hivi bila kuhoji maswali ya maana. Wao wanachowaza ni kuja kupost tu.

Yaani akili za Cyprian Musiba na hao Waandishi wa Habari aliowakusanya kama siyo kuwaita zote zinafanana hivyo sishangai sana kuwa na aina hii ya ' upungufu ' na naona Media ya Tanzania kila uchao tu inazidi kutafuta Kaburi la Kujizikia kwani haina tena ' Ueledi ' wala ' Ubunifu '.
 
Waandishi wetu ni wakuandika hawana taarifa za kiuchunguzi na wala si wasomaji wa vitabu na makala. Ni watu wa matukio kwaiyo kuwaambia waaulize maswali kwa ishu km hizo eti tofauti ya CIA na FBI ni kuwaonea maana ni mabubu.
 
WAANDISHI WETU NI WAKUANDIKA HAWANA TAARIFA ZA KIUCHUNGUZI NA WALA SI WASOMAJI WA VITABU NA MAKALA.NI WATU WA MATUKIO KWAIYO KUWAAMBIA WAALUZE MASWALI KWA ISHU KM HIZO ETI TOFAUT YA CIA NA FBI NI KUWAONEA MAANA NI MABUMBU.

Kweli Mkuu na wala hujakosea kwa ulichokiandika ila nadhani tukizidi kuwasema labda watajitathmini na kubadilika au?
 
yaan tena uyo musiba ni kilaza kwel kwel, anamjaza tu upepo no 1 pasipokujua kama watu hatar wapo ndan ya chama chake! kwa taarifa yako ww musiba watu wote hatar wapo ndan ya chama chako maana hao ndio wanaowapenyezea information wapinzan sasa inabid ujitathimi uone kama kwel ww una akil timam au mafuta?
 
genta nina wasiwasi katika yale majina aliyotaja yule kilaza mwenzio,moja ya jina ni lako.

bila shaka upo kwenye ile orodha. acha tuone hii vita vya vilaza kwa vilaza itaishaje.

ni hayo tu, povu ruksa.
 
Huyu Musiba ana akili sana ila huwezi kumwelewa haraka haraka, alichokifanya ni kinyume chake (vice versa) yaani ametumika kuleta ile agenda ya maandamano kutoka mitandaoni mpaka kweny vyombo vya habar.

Kiufupi ametumika kuchochea maandamano na anataja na tarehe ya maandamano (26/4/2018). Amemsaidia yule dada wa mitandaon kuhusu agenda yake. Jamaa ana akili sana yani amestua na raia wengine.
 
Back
Top Bottom