VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Mwenyekiti wangu wa CCM Taifa na Rais wangu, Dr. John Pombe Magufuli naomba nikupe ujumbe huu mfupi. Mimi nipo huku Arusha kuhudhuria mkutano wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS). Nimeshaamua kuwa katika uchaguzi wa TLS, nitamchagua Wakili Msomi Tundu Lissu kuwa Rais wetu wa TLS. Nina sababu, nia na ari ya kumchagua Lissu.
Mwenyekiti, sikuja Dodoma ingawa mimi ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu na vikao vinginevyo vya kitaifa. Sikuja kwakuwa nilijua kila ambacho kitatokea kule Dodoma kikiwekwa kwenye mwamvuli wa 'mabadiliko ndani ya chama'. Mimi nayaita ni 'machafuko ndani ya chama' badala ya mabadiliko. Mambo yale hayakufanyika inavyopasa.
Mwenyekiti, makada si watumishi wa umma. Makada si watu wa kupigwa mkwara, kuambiwa maneno makalimakali na kupondwapondwa. Ukada hauna mshahara kama ulivyo utumishi wa umma. Ukada upo kwenye hiari zaidi ya maslahi. Makada wanapaswa kushawishiwa badala ya kutishiwa; kuombwa badala ya kusombwa.
Hakukuwa na haja ya kujaza mapolisi kule Dodoma. Hakukuwa na haja ya kukamata makada, tena waandamizi, na kuwashikilia. Hakukuwa na haja ya kutisha kihotuba na hata kusema chochote bila ya hoja ya kimajadiliano. CCM, na vyama vingine haviongozwi kama jeshi. Vyamani, wanachama hujadiliana na kukubaliana. Nasema tena, makada si watumishi wa umma.
Mabadiliko ni kupunguza vikao? Kwanini mabadiliko yasingekuwa ya Mwenyekiti wa CCM kuwa mwingine na Rais wa Jamhuri kuwa mwingine? Mabadiliko ndiyo kukichora chama kama chama cha watu wachache kuamua na kufanya watakalo halafu makada wote waliosalia kuambiwa na kuambiwa wamepitisha kwa kishindo?
Mwafaaaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Arusha kumchagua Lissu kuwa Rais wa TLS)