PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Abdulaziz Said Sakala, leo Julai 3, 2025, amerejesha rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Mjini kupitia CCM, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Sakala amewasilisha fomu hiyo katika Ofisi za CCM zilizopo Kata ya Mjini, Shinyanga, huku akipokelewa na viongozi wa Chama na wanachama mbalimbali walioungana naye katika hatua hiyo muhimu ya kisiasa.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu, Sakala amesema iwapo atapewa ridhaa na chama chake na baadaye kuchaguliwa kuwa Diwani, atahakikisha anasimamia maendeleo ya wananchi wa Kata ya Mjini kwa vitendo. Hata hivyo, amesema ataweka wazi mipango yake kwa wananchi endapo jina lake litapitishwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi ujao.
"Katika uchaguzi huu nafarijika kuona vijana wengi wamejitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kama Udiwani na Ubunge. Hii ni ishara ya kuimarika kwa demokrasia ndani ya chama chetu, na nashukuru CCM kwa kulinda na kudumisha misingi hiyo," Amesema Sakala.
Hatua hiyo ya Sakala inakuja wakati mchakato wa ndani ya chama cha CCM wa kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali ukiendelea kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini.