Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Ruvuma kupeleka orodha ya watumishi wala rushwa kwa Rais Magufuli

BongeMwepesi

Senior Member
Aug 13, 2013
125
83
Mwenyekiti huyo wa UVCCM Raymund Mhenga ameyasema hayo kwenye mahafali ya 10 ya Wahitimu wa Chuo Cha Ufundi Top One College.Mhenga amesema anapeleka majina ya watumishi wa Serikali ambao wanakwamisha wawekezaji na mabingwa wa Kuomba Rushwa kwa wananchi kwa Rais Magufuli kupitia kwa Mkuu wa Mkoa,maana hali hiyo ya watumishi kupenda Rushwa inachelewesha maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma.

"Hawa wapenda Rushwa ndio wanaochelewesha maendeleo ya Mkoa wetu na wanawaumiza wananchi wetu na wanatupa wakati mgumu chama chetu kuaminiwa na wanamchonganisha Rais Magufuli na Serikali yake kwa Wananchi".

Mwenyekiti pia aliwaeleza wahitimu wa chuo hicho namna bora za kujiajiri na kwamba serikali imetoa fursa nyingi za uwezeshaji kwa Vijana hasa za Mikopo kwenye Vijana wenye ujuzi hivyo wasisubiri tu ajira ila wajiunge vikundi hili kupatiwa Mikopo na kuwa kama sehemu ya mtaji kutimiza malengo yao.
 
Wala rushwa peleka kwa PCCB Mkoa wa Ruvuma, unapeleka kwa Rais, rais atashughulika na mangapi!?. Sema tu umeanza kuunyemelea ubunge hapo Songea mjini sasa unatafuta utoke vipi!!
 
Huyu naye ana matatizo kwani Mkoani kwake hakuna Kamanda wa TAKUKURU? Mwisho Mwalimu Mkuu naye atataka kupeleka orodha ya watoro shuleni kwa Magufuli!
Haya mambo mara zote huibuka kwenye tawala za kidikteta. Wanapoona mambo yanaharibika, hutafutwa wachawi wa kutupiwa lawama kuficha tatizo halisi.

Utawala huu unapiga vita uwekezaji na private sector. Mambo yanapoharibika, ni lazima tuone vituko. Watasingiziwa hata watu wasiokuwa na ajira popote kuwa ndio wanaharibu nchi.

Yetu macho.
 
Kwa hiyo viongozi wa Serikali mkoa wameshindwa kazi, huu ndiyo ujumbe anaompelekea JPM
 
Dah yani ufunge safari Songea to State house kumpelekea rais majina ya wala rushwa? Who are you by then, unataka kutuambia kwamba Kamanda wa takukuru Ruvuma, RSO wameshindwa kazi, au ndio majungu style?
 
huwezi kuzichukulia kwa uzito kauli za UVCCM au CCM kwa ujumla, umbumbumbu wao unastaajabisha!
 
Kwa nini asifanye hivyo wakati ameaminishwa hivyo? kwamba yuko mtu mmoja tu anayeweza kutatua shida zote kubwa na ndogo.
Huyu naye ana matatizo kwani Mkoani kwake hakuna Kamanda wa TAKUKURU? Mwisho Mwalimu Mkuu naye atataka kupeleka orodha ya watoro shuleni kwa Magufuli!
 
Na asisahau kupeleka list ya watumishi ambao hawajaonja nyongeza ya mshahara tangu Magufuli aingie madarakani.
Mwehu sana huyo UVCCM.
 
Huyu kijana ni nashindwa kumuelewa kabisa,Ila nasikia ni mtu Wa system na kila anachokifanya kinamaana na inawezekana analenga kitu.Kwa waliosoma naye chuo kikuu cha dar es salaam wanasema anaitumikia system muda mrefu na inawezekana kuna jambo bwana mkuu anataka kulifanya kwa viongozi wa huko Songea na yeye katangulizwa kuchokoza.
 
Huenda jina la Mkuu wa Mkoa lipo kwenye hiyo orodha ndio sababu hataki kupeleka hiyo orodha ngazi ya Mkoa
 
Huyu kijana ni nashindwa kumuelewa kabisa,Ila nasikia ni mtu Wa system na kila anachokifanya kinamaana na inawezekana analenga kitu.Kwa waliosoma naye chuo kikuu cha dar es salaam wanasema anaitumikia system muda mrefu na inawezekana kuna jambo bwana mkuu anataka kulifanya kwa viongozi wa huko Songea na yeye katangulizwa kuchokoza.
Hakuna cha System yoyote kwa Ray. Sio Songea Boys,Sio Minaki,Sio UD, Sio pale Clouds na wala sio kwenye kugombea Ubunge Songea sio popote.....

Ni mwanasiasa tu kama wanasiasa wengine. Analitaka jimbo kwa udi na uvumba
 
Mwenyekiti huyo wa UVCCM Raymund Mhenga ameyasema hayo kwenye mahafali ya 10 ya Wahitimu wa Chuo Cha Ufundi Top One College.Mhenga amesema anapeleka majina ya watumishi wa Serikali ambao wanakwamisha wawekezaji na mabingwa wa Kuomba Rushwa kwa wananchi kwa Rais Magufuli kupitia kwa Mkuu wa Mkoa,maana hali hiyo ya watumishi kupenda Rushwa inachelewesha maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma.

"Hawa wapenda Rushwa ndio wanaochelewesha maendeleo ya Mkoa wetu na wanawaumiza wananchi wetu na wanatupa wakati mgumu chama chetu kuaminiwa na wanamchonganisha Rais Magufuli na Serikali yake kwa Wananchi".

Mwenyekiti pia aliwaeleza wahitimu wa chuo hicho namna bora za kujiajiri na kwamba serikali imetoa fursa nyingi za uwezeshaji kwa Vijana hasa za Mikopo kwenye Vijana wenye ujuzi hivyo wasisubiri tu ajira ila wajiunge vikundi hili kupatiwa Mikopo na kuwa kama sehemu ya mtaji kutimiza malengo yao.

Nani kakudanganya kuwa rais hujui wala rushwa? Taarifa ya Mzee Warioba kuhusu rushwa iko Ikulu. Umewahi kusikia akizungumzia? Wakati wa kampeni Mzee Warioba iliwekwa mstari wa mbele ili kuaminisha umma kuwa katiba mpya itapatikana na rushwa itadhibitiwa! Pia watu wapate imani kuwa serikali ijayo itatumia busara za huyu mzee.Tume ya Warioba ilibainisha taasisi za umma zinazoongoza kwa rushwa na kila mtu anazijua. Taasisi hizo ndizo zinazotumika sasa kushamirisha ukandamizaji wa raia na kuvunja haki za raia.
 
Huyu naye ana matatizo kwani Mkoani kwake hakuna Kamanda wa TAKUKURU? Mwisho Mwalimu Mkuu naye atataka kupeleka orodha ya watoro shuleni kwa Magufuli!
Nadhani mkuu hapa umesahau kuwa rais ndiye mwajiri mkuu. Acha aende hata mwalimu mkuu naye apeleke hao watoro wafutwe shule na rais. Si ulisikia kilichowakuta wanafunzi mbeya.
 
Back
Top Bottom