Mwenyekiti wa UVCCM Arusha awasaliti UVCCM

Mwenyekiti wa UVCCM Arusha awasaliti UVCCM

Joined
Feb 26, 2014
Posts
22
Reaction score
17
Taarifa za kuaminika Mwenyekiti wa UVCCM Arusha pamoja na aliekuwa mgombea udiwani kata ya Sombetini Arusha wameshiriki katika kikao cha awali cha chama kipya cha Alliance for Change and Transparency (ACT).

Munisi pamoja na David wameonekana mara mbili katika vikao tofauti huku Munis akitaka kupata ridha ya chama hicho kugombea ubunge jijini Arusha,tayari Munis anawashawishi wanachama wa UVCCM kujiunga.

Kikao hicho kiliudhuriwa na wafanya biashara wakubwa Arusha wa chama cha CCM wakiongozwa na Munis na Mwenyekiti wa Mondoli.

Kikao cha siri kinaendelea muda huu katika moja ya hoteli kubwa hapa Arusha chini ya Jonas Nanyaro.
 
Taarifa za kuaminika Mwenyekiti wa UVCCM Arusha pamoja na aliekuwa mgombea udiwani kata ya Sombetini Arusha wameshiriki katika kikao cha awali cha chama kipya cha Alliance for Change and Transparency (ACT)
Munisi pamoja na David wameonekana mara mbili katika vikao tofauti huku Munis akitaka kupata ridha ya chama hicho kugombea ubunge jijini Arusha,tayari Munis anawashawishi wanachama wa UVCCM kujiunga'
Kikao hicho kiliudhuriwa na wafanya biashara wakubwa Arusha wa chama cha CCM wakiongozwa na Munis na Mwenyekiti wa Mondoli.
Kikao cha siri kinaendelea muda huu katika moja ya hoteli kubwa hapa Arusha chini ya Jonas Nanyaro.

Ufipa kweli imefilisika kisiasa huyu punguani sijui wamemtoa wapi?
 
Kweli CCM hadaa CDM shujaa. Kwani yote haya mwenyekiti wao aliyatabiri kuwa rushwa ndani ya chama Ikizidi 2015 watakuwa wao ndio wapinzani.
 
Nimeisikia hiyo habari hapa mjini kati. Tatizo CCM walikuwa wanakishabikia hiki chama wakidhani ni mwiba kwa wahasimu wao CDM, kumbe nao wanapita njia hiyohiyo angali hawajavaa viatu. Naamini lolote linaweza kutokea kuhusu hiki chama kupata kuimarika ghafla na kuonyesha upinzani mkubwa kwa CCM na CDM.
 
Lyimo kaka hadi sasa chama hiki kinawanunuwa watu kwa pesa jana tulipatiwa shilingi 30,000 kwa mwanachama na 68,000 ukipeleka mtu mmojaakikubali tu kuwa mwanachama.
 
Lyimo kaka hadi sasa chama hiki kinawanunuwa watu kwa pesa jana tulipatiwa shilingi 30,000 kwa mwanachama na 68,000 ukipeleka mtu mmojaakikubali tu kuwa mwanachama.

Basi kama ndiyo hivi, ni dhahiri hiki chama kitaibuka ghafla na kufa baada ya muda mfupi. Vilevile kitaharibu siasa za Tanzania, wananchi watategemea kupewa hongo ili kutimiza haki zao za kikatiba na kisheria. Huko baadaye itakuwa hata kama unataka kuhamasisha wananchi kwaajili ya maendeleo yao, basi itahitajika kwanza uwape hongo. Tumeshafika pabaya sana....
 
Lyimo kaka hadi sasa chama hiki kinawanunuwa watu kwa pesa jana tulipatiwa shilingi 30,000 kwa mwanachama na 68,000 ukipeleka mtu mmojaakikubali tu kuwa mwanachama.

Mkuu, sidhani kama taarifa yako ina ukweli.
Hizo elfu 30, kama zipo, ebu tuelekeze na sisi tukazichukue
 
Mfinanga Oroliani 0753156350 mtafute,huyo alikuwa kamanda wa Chadema Kata yaOroliani na kwa sasa ni mwanaACT na nimratibu wa ACT arusha anaorodha ya majina ya watu kila siku anaandikisha'
 
Back
Top Bottom