Mwenyekiti wa NEC: "CCM Ng'oeni Mabango ya Kikwete!" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti wa NEC: "CCM Ng'oeni Mabango ya Kikwete!"

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Buchanan, Sep 14, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Sep 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  UME ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imeitaka CCM) kung’oa mabango ya picha za mgombea wake wa urais, Jakaya Kikwete zilizopigwa kwenye maeneo ya Ikulu.

  Mwenyekiti wa Nec, Jaji Lewis Makame aliliambia gazeti hili jana kuwa agizo hilo pia linavihusu vyama vyote vilivyotumia mabango ambayo hayakuthibitishwa na tume hiyo.

  “Tumeshaviagiza vyama vyote vinavyotumia mabango ambayo hayakupitishwa na Nec viache mara moja,” alisema Jaji Makame ambaye tume yake ilikutana kwa siku mbili mwishoni mwa wiki kujadili suala hilo lililoibuliwa na Baraza la Ushauri la Vyama vya Siasa.

  “Lakini agizo hilo si kwa CCM tu, bali vyama vyote vinavyotumia bango ambalo halikuhakikiwa na tume.”

  Mwananchi iliripoti mwishoni mwa wiki kuwa Nec ilijadili suala hilo kwa siku mbili mfululizo na kuwahoji wawakilishi wa CCM kuhusu baadhi ya mabango yanayomuonyesha mgombea wake wa urais akiwa Ikulu.

  Gazeti moja la kila siku la Kiingereza liliripoti jana kuwa chama hicho tawala kilianza kuondoa mabango mawili makubwa ya barabarani yaliyowekwa mkoani Kagera, ikitii sheria za nchi baada ya mabango hayo kutopitishwa na Nec.

  Gazeti hilo linamkariri katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba akisema kuwa chama chake kinaheshimu sheria za nchi. Makamba alionekana kwenye kituo cha televisheni cha TBC akisema kuwa mabango yote ya CCM yalishapitishwa na Nec na kwamba wanafanya kazi kwa makini.

  Lakini baada ya vikao vya siku mbili mfululizo, CCM ilianza kuondoa mabango hayo hata kabla ya taarifa rasmi ya Nec jana.

  Jana, Makamba hakutaka kuzungumzia suala hilo baada ya Mwananchi kumpigia simu kutaka ufafanuzi.

  "Mimi niko Bumbuli kwenye mikutano ya kampeni za mwenyekiti. Kama taarifa hiyo ipo nitaikuta ofisini, nisubiri," alisema Makamba.

  Sakata la mabango lilianza Septemba 6 mwaka huu wakati Baraza la Ushauri wa Vyama vya Siasa lilipoitaka CCM kutotumia picha zilizopigwa Ikulu katika mabango ya mgombea wake wa urais.

  “Picha za kampeni za CCM zinazoonyesha Ikulu zisitumike, ukitumia hizo picha halafu chini yake ukasema chagua chama fulani, hiyo itakuwa siyo demokrasia kwa sababu hata aliyepiga hizo picha ni mfanyakazi wa Ikulu,” alisema Tendwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mkutano wa baraza hilo.

  Kwa mujibu wa Tendwa, picha hizo pia zinawashawishi wananchi kukipigia kura chama hicho wakati vyama vingine haviwezi kupata fursa ya kutumia maeneo hayo kwa kuwa havijashika dola.

  Tendwa aliwaeleza waandishi wa habari kuwa mabango hayo ni yale yanayoonyesha picha za majengo ya ofisi na makazi hayo ya mkuu wa nchi.

  Hivi karibuni, Naibu katibu wa elimu ya mpigakura na habari wa Nec, Ruth Masham alilieleza gazeti hili kuwa suala hilo lilijadiliwa na Nec kwa kwa siku mbili kabla ya kupata muafaka ambao Makame aliubainisha jana.


  Source: MWANANCHI.
   
 2. S

  Sylver Senior Member

  #2
  Sep 14, 2010
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nice
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Sep 14, 2010
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,850
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280
  ..haya ni mafanikio ya jamii forums....kwani hili la mabango tulianza kulipigia kelele hapa tangu tu walipoyabandakika.........mabango yanayoondolewa ni yale yenye link na ikulu.

  Pia mabango ambayo ametumia picha za viongozi wa nje lazima pia yatolewe ....kwanza ni ukoloni mamboleo kutumia picha za viongozi wa nje kujiuza kwenye chaguzi za ndani...zaidi ya kuwa haipendezi kidiplomasia....

  sasa pia wajiandae kuwalipa pesa zao .....watanzania ambao picha zao zimetumika kwenye mabango...kwani pale ni biashara ile .....waliopewa hiyo kazi wamelipwa mamilioni na sio busara kutumia bure picha za walalahoi ...watoto ,walemavu hadi vikongwe bila kuwalipa stahili yao au kutokuwa na mktaba nao.....

  ndio maana tunasema tupo makini ...
   
Loading...