security guard
JF-Expert Member
- Sep 27, 2011
- 799
- 603
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilula, Kata ya Hungumalwa Wilayani Kwimba ndugu Hamala Materemki amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) asubuhi ya leo baada ya hotuba ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahaman Kinana aliyoitoa kwa wananchi baada ya kushiriki mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Hungumalwa.
Mwenyekiti huyu, mwanachama wa CHADEMA amefikia uamuzi huo baada ya kukinai maneno ya kweli yenye ujumbe mzito aliyoyatoa Katibu Mkuu wa CCM kwa wananchi wa eneo hilo, akiwataka waache kuyumbishwa na Upinzani na waamue kwa dhati kujiletea maendeleo kwa kufanya Kazi.
Ndugu Hamala, ameshaandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Uenyekiti wa Kijiji, kwani amepoteza sifa kwa kuhama Chama alichokuwa anakiwakilisha na hivyo italazimika ufanyike uchaguzi mwingine wa kuunda upya Serikali ya Kijiji, ambapo Ndugu Hamala amesema atagombea tena nafasi hiyo kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana yuko Wilayani Kwimba akiendelea na Ziara yake ya Siku kumi katika Mkoa wa Mwanza, ambapo anategemea kumaliza Juni 30, 2015.