Mwenyekiti wa Halmashauri Karagwe ang'ang'aniwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti wa Halmashauri Karagwe ang'ang'aniwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jul 30, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  [​IMG]


  PIUS Msekwa, makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), anatuhumiwa kumkingia kifua Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karagwe mkoani Kagera, Kashunju Runyogote.

  Msekwa anatuhumiwa kuamuru, kuwatisha na kuwashawishi kwa njia ya rushwa madiwani wa Karagwe wanaotokana na chama chake ili kumlinda Runyogote ambaye wenzake hawamtaki.

  Hata hivyo, Msekwa harakaharaka anakana madai hayo.

  Akizungumza na MwanaHALISI kwa njia ya simu Jumatatu iliyopita, Msekwa alisema "Kwanza niseme jambo moja. Nashukuru kwa kunipigia kwa sababu watu wanapenda sana kuzusha mambo. Kwa hiyo, huo ni uzushi kijana wangu."

  Alipobanwa kwamba alikuwa mkoani Kagera mapema mwezi huu na jambo hilo alilishughulikia kwa nguvu zote tena ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kwa madiwani, alisema;

  "Ndiyo maana nasema ni uzushi."

  "Ni kweli, nilikuwa Kagera si kwenye kesi hiyo. Nilikwenda na kuhudhuria mkutano wa kamati ya siasa ya mkoa. Sasa tukiwa kwenye mkutano, ndipo ikaibuka taarifa hiyo ya madiwani wa Karagwe.

  "Nikamwambia katibu wa CCM mkoa afuatilie siku inayofuata na anipe majibu. Nikamwambia kwamba awaambie madiwani waangalie maslahi ya chama juu ya uamuzi wao."

  Anasema kwamba katibu huyo wa CCM ambaye hakumtaja jina, alikwenda Karagwe na aliporeja alimweleza Msekwa kuwa amemaliza mgogoro huo na haupo tena."Si kwamba nilihonga au kwenda Karagwe. Watu wazushi sana mwanangu," anasisitiza

  Msekwa ambaye ni katibu mkuu wa kwanza wa CCM ilipozaliwa kutokana na muungano wa vyama vya TANU na ASP.

  Msekwa anadaiwa kujitosa katika mgogoro huo baada ya kupata taarifa kuwa madiwani 29 wa Karagwe, wamemwandika barua Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Bosco Ndunguru kuitisha mkutano maalumu kujadili tuhuma dhidi ya Runyogote. Madiwani waliosaini barua hiyo ni kutoka CCM na upinzani.

  "Huyu Msekwa alipoelezwa jambo hilo na viongozi wa CCM mkoani Kagera, haraka alisikika akisema, ‘nashangazwa na hatua ya madiwani wa CCM waliomweka mwenyekiti wao, kushirikiana na madiwani wa upinzani kumfukuza,'" ameeleza kiongozi mmoja wa CCM mkoani hapa.

  Taarifa zinasema Msekwa alianza kutafuta suluhu kwa kufanya kikao na madiwani hao, 6 Julai 2012, kwenye hoteli ya St. Francis iliyoko Bukoba mjini.

  Baadhi ya tuhuma zinazomkabili Runyogote, ni matumizi mabaya ya madaraka; wizi na ufujaji wa rasilimali za taifa kwani katika kipindi cha miezi 18, tayari Runyogote amelipwa kinyume na taratibu, kiasi cha Sh. 90 milioni.

  Nyaraka zinaonyesha Runyogote amelipwa Sh. 620,000 kupitia hundi Na. 141077 yenye maelezo ya mkutano wa madiwani huko Mwanza na kiasi kingine cha Sh. 5,880,000 alilipwa kwa hundi Na. 141221 kwa maelezo ya matumizi ya kikao cha kamati za vyama uliofanyika Agosti 2011.

  Aidha, Runyogote amelipwa kiasi cha Sh. 9.3 milioni kwa hundi Na. 141139 yenye maelezo mikutano ya madiwani iliyofanyika Mwanza (Tanzania) na Kisumu, nchini Kenya.

  Pia amelipwa Sh. 3,591,000 kupitia hundi Na. 000293 yenye maelezo ya safari ya Rwanda na kiasi kingine ni Sh. 14.7 milioni kwa hundi Na. 141220 kwa mkutano wa Baraza wa Agosti 2011.

  Malipo mengine ni ya hundi namba 146449 ya Sh. 21,725,000 yenye maelezo ya Kamati za Vyama na Baraza iliyofanya kikao chake Oktoba 2011; hundi Na. 000654 ya Sh 5,910,000 yenye maelezo ya Kamati za Vyama mwezi Januari 2012.

  Vilevile, kuna malipo ya hundi Na. 000653 ya Sh 15,295,000 yenye maelezo ya Baraza la madiwani katika kikao cha Januari 2012; mengine ni ya hundi Na. 001828 ya Sh 7,132,320 yenye maelezo ya safari ya Rwanda Mei, 2012. Malipo mengine ni ya hundi Na. 000050 ya Sh 5,795,000 yenye maelezo ya ukaguzi miradi Mei, 2012.

  Alipoulizwa Runyogote kuhusiana na tuhuma dhidi yake na kupingwa na madiwani amesema,

  "Kwanza mimi mambo hayo siyajui."

  Akaendelea kusema huku aking'aka kwa sauti kali kwamba, "Pili, nani amekupa namba yangu? nakuuliza nani amekupa namba yangu?"

  Alipoambiwa kwamba yeye ni kiongozi wa umma kwamba anaweza kutafutwa wakati wowote kwa jambo linalohusiana na wilaya yake, akatulia na kujibu, "Sasa kaka kama watu wana mipango yao kama hii ya kukuondoa watashindwa? Kaka mimi sijui lolote. Hakuna ninalolijua juu ya tuhuma hizo."

  Naye, Ndunguru ambaye ameandikiwa waraka na madiwani wakimtaka kuitisha kikao kumjadili Runyogote, hakupatikana. Awali simu yake iliita bila majibu kabla ya kufungwa kwani kila alipopigiwa kuanzia saa 5.15 asubuhi juzi Jumatatu hakupatikana.

  Nakala ya barua hiyo ya madiwani kwenda kwa mkurugenzi ya 30 Mei 2012 ambayo gazeti hili imeona nakala yake, imepelekwa pia kwa mkuu wa Usalama wa Taifa mkoani Kagera (RSO), mkuu wa TAKUKURU mkoani humo na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai (RCO).

  Madiwani, katika barua hiyo iliyoandikwa kwa mkono na kusainiwa, wamesema kwamba wanataka mkutano huo kwa kwa mujibu wa kanuni za kudumu za halmashauri ya wilaya ya Karagwe. Kanuni hiyo ni namba 80 (i).

  Tuhuma dhidi ya Runyogote zinasema amekuwa akipewa mafuta pamoja na gari la halmashauri kumpeleka kijijini Rukuraijo na kumrudisha Kayanga wakati vikao vya baraza vikiendelea.

  "Baraza la madiwani halijawahi kuidhinisha mafuta ya mwenyekiti ya kumsafirisha wakati vikao vikiendelea isipokuwa posho ya kujikimu na hali hii imeisababishia halmashauri yetu hasara kubwa," inasema sehemu ya barua hiyo.

  Runyogote pia anatuhumiwa kuhudhuria sherehe za kusimikwa na kuwekwa wakfu Askofu Rugambwa wa jimbo Katoliki la Kigoma kwa kutumia gari ambalo ni mali ya TASAF lenye namba za usajili STK 2098 kwa gharama za halmashauri bila idhini ya madiwani.

  Tuhuma nyingine ni kupokea posho kwa siku nyingi zaidi ya zile zilizotajwa kwenye mwaliko mbali ya siku za njiani.Mwenyekiti huyo alihudhuria mkutano wa maendeleo ya mazingira Kisumu. Wakati barua ya mwaliko inataja siku tatu, Runyogote amedai posho ya siku saba. Amedai posho ya njiani.

  Barua inasema Runyogote amekuwa akishinikiza uanzishaji wa miradi mbalimbali kwa maslahi binafsi na kwa kukiuka taratibu za halmashauri.

  Miradi hiyo ni pamoja na kitega uchumi kilichopo stendi ya Kayanga kinachodaiwa kutofuata taratibu ikiwamo kupitisha kwenye kamati ya wataalamu (CMT), kamati ya ujenzi, uchumi na mazingira.Runyogote anatuhumiwa kulazimisha ununuzi wa vifaa vya mradi wa maji wa Rukurajio vilivyonunuliwa na kusafirishwa moja kwa moja hadi kwenye kata yake bila kufuata taratibu za manunuzi.

  Aidha, madiwani wa Karagwe wanamtuhumu Runyogote kupokea malipo zaidi ya mara moja. Alipokea fedha ya ziara ya kwenda nchini Rwanda na wakati huo akachukua nyingine za safari ya kukagua miradi.

  Hata hivyo, alipogundua kwamba anashutumiwa kuchukua posho mbili, alimwagiza mtumishi wa halmashauri aliyetajwa kwa jina la Ashura Kajuna kurejesha kiasi cha Sh. 270,000.

  Fedha hizo zilipokewa 6 Juni 2012 na ofisa malipo wa halmashauri ya wilaya aliyefahamika kwa jina moja la Jack na kukatiwa risiti.

  Mmoja wa madiwani hao anasema, "Baada ya kurejesha fedha hizo, Runyogote ametumia viongozi wa mkoa kutuziba midomo ili tuhuma dhidi yake zisichunguzwe na kikao kisiitishwe, madiwani wote wa CCM tumeitwa na kutishwa 7 Juni 2012."

  Tuhuma nyingine ambazo wadiwani wameporomosha, ni Runyogote kuingiza halmashauri kwenye mikataba yenye utata. Wanataja mkataba wa matengenezo ya madirisha ya chuma ya shule za sekondari na ule wa ununuzi wa saruji.

  Runyogote anatuhumiwa kushindwa kusimamia maazimio halali ya vikao vya baraza la madiwani kwa kushindwa kuwa na ushirikishaji na ushirikishwaji wa wajumbe wa baraza la madiwani.

  Barua ya madiwani 29 inasema, ni "pamoja na kulipwa gharama za usafiri na posho kwenda Dar es Salaam kushughulikia gari yenye Na. STK 4891 ambalo lililokaa muda mrefu na bila taarifa zake kukweka hadharani."

  Katika barua hiyo, madiwani wanasema Runyogote amekuwa akiwashambulia madiwani kwa maneno yenye vitisho na matusi wale anaotofautiana nao kwenye hoja za msingi katika vikao.

  Anatuhumiwa pia kulidhalilisha baraza kwa kauli zake alizozitoa katika Radio Fadeco ambazo zimelenga kuonyesha umma kuwa wajumbe wa baraza hilo hawana upeo wa kuona mbali na wameingiliwa na virusi kwa kukataa kupitisha mradi wa kitega uchumi.

  Mradi huo unaotajwa, ndiyo unaolalamikiwa na madiwani kutofuata taratibu.  CHANZO: MwanaHalisi
   
 2. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Ndugu madiwani wa Karagwe, nashukuru kwani mmeamka, hapo mliposhika ni patamu sana msipaachie, endelezeni kibano chenu na kuminya kwa sana, tena kwa nguvu zenu zote mpaka ajijambie. Mkamueni kende nunda huyu choo kimbane, mbaneni korodani kisawasawa mpaka ujogoo umtoke.

  Baada ya kumvua kanzuu yake, mpelekeni kwa pilato ajibu mashitaka, hawa ndo mafisadi wadogo na wenye njaa kaa mchwa.

  Nawapa pongezi, hongera na heko zenu, kwa ujasiri wenu mkuu, naiheshimu kazi yenu, nawapa five.
   
 3. Yakuza

  Yakuza Senior Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Kama hayo madai ni kweli:

  1. Avuliwe madaraka
  2. Afikishwe mbele ya sheria
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hii nchi, majitu hata woga hayana. Tutabadilika lini?
   
 5. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Alipita kwa hongo na Mbunge wa Kyerwa anahusika maana ndiye aliyempa hela ya kumweka madarakani ili hari uwezo wake kielimu na utendaji ni mdogo.
  Wabunge wetu hasa kata za Isingiro, Rutunguru, Kaisho,kibingo Mabira,kyerwa,Rwabere,Nkwendana karagwe nzima tuondolee huyu takataka. Nimefuraishwa na wananchi wa kihanga-Isingiro kwa kukataa mradi wa machine ya kusaga na kukoboa ambayo ilifungwa kihuni kwa gharama za x10. Najua karagwe tunaweza najua tunaweza sasa tuwaondoe hawa maana hata mnyauko wa migomba unakuja kwa sababu ya watu kama hawa kuwepo madarakani.
   
 6. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Huu ndio wakati wa Watanzania kubadilika tumechoka kutishwa na kuvumilia mafisadi, nawapa hongera madiwani wa Karagwe somo limeeleweka!!! Kuna mbunge juzi kakili kuwa upinzani sio vita ni kuwaeleza watu udhaifu na maovu ya serikali na kutafuta njia ya kuyatatua!! Naona Karagwe kumekucha, Tanzania amkeni wakati wa kuonewa umekwisha sasa!!!

   
 7. B

  Byera1 Member

  #7
  Jul 30, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli hizi siasa zisizokuwa na tija kwa mwendo huu naamin zitafika mwisho na hakika wana karagwe tutamkumbuka Mh Salvatory Kalabamu, na walaaniwe waliomshawishi agombee ubunge na wakaja kumuangusha na kumpa Blandes ambaye amewekwa kwa nguvu za Sir George Kahama mbunge ambaye ameiongoza karagwe kwa siku nyingi bila hata kuiletea maendeleo
   
Loading...