tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Wakati ambao mchakato wa kampeni za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29 mwaka huu ukiendelea, Mgombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kivule, lilipo Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam, Ndugu Massaburi Dougras Didas ameungwa mkono na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Msongola katika kukinadi Chama cha Mapinduzi.
Soma pia: Mgombea ubunge CHAUMMA amnadi Samia jukwaani akipiga kampeni
Akiwa katika kuzisaka kura za viongozi wa CCM kwenye kata hiyo ya Msongola iliyopo jimbo la Kivule, Ndugu Massaburi alimuomba Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Kata ya Msongola aliyekuwa amejitokeza kwenye kampeni hizo, kukinadi Chama cha Mapinduzi.
Tukio hilo lililotokea jana Septemba 11, 2025 liliibua mshangao miongoni mwa wananchi, kutokana na nafasi ya mwenyekiti huyo ambaye kikatiba anatakiwa kuhamasisha sera za chama chake.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo alisema uamuzi wake umetokana na kutaka kuunga mkono mtu anayejali maendeleo ya wananchi badala ya kuzingatia mipaka ya kisiasa pekee.
Kwa upande wake Ndugu Massaburi aliwashukuru wananchi wa Msongola kwa mwitikio mkubwa na kuahidi kuendelea kufanya siasa za kistaarabu zenye lengo la kuwaletea wananchi maendeleo huku akisisitiza kuwa uchaguzi huu ni nafasi ya wananchi kuchagua viongozi watakaoweza kusimamia vema rasilimali za taifa na kuhakikisha huduma za kijamii zinaboreshwa.