Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi Suleiman Mathew apewa dhamana, atoka Gerezani

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,281
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi Suleiman Mathew pamoja na Mwenyekiti wa Kata waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha miezi nane gerezani wamepata dhamana baada ya Mahakama Kuu kusikiliza maombi yao ya kuomba dhamana wakati rufaa yao ikisikilizwa.


January mwaka huu Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Lindi, Suleiman Mathew alihukumiwa na Mahakama ya Lindi kwenda jela miezi nane baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko bila ya kibali.

Mathew ambaye alikuwa mgombea ubunge katika jimbo la Mtama mkoani humo kupitia Chadema na kiongozi mwenzake wa kata wamehukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko bila ya kibali.

Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya Mkoa wa Lindi, mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhina.

Mahakama ilifikia uamuzi huo baada ya kusikiliza mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kujiridhisha kuwa ushahidi wao umethibitika bila kuacha shaka.

Waliotiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ni Mwenyekiti Chadema mkoani Lindi, Selemani Methew pamoja na Katibu wa Tawi la Kata ya Nyangamala, Ismail Kupilila.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mhina alisema, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Juma Maige uliwafikisha mahakamani hapo mashahidi sita.

Alisema kutokana na ushahidi ulitolewa na mashahidi hao, mahakama imeona upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao bila kuacha shaka yoyote na kuwatia hatiani.

Habari zaidi soma=>LINDI: M/kiti wa CHADEMA na Katibu wa tawi la Nyangamara wahukumiwa miezi 8 bila faini
 
Huyo jaji ni jipu na nitamtumbua muda wowote, haiwezekani watu wameshafungwa jela alafu mtu mmoja kutumia madaraka yake anawatoa badala ya kuwaacha wakalime huko gerezani
 
Breaking news...
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Lindi Suleiman Mathew pamoja na M.kiti wa Kata waliokuwa wamehukumiwa kifungo cha miezi nane gerezani wamepata dhamana baada ya Mahakama Kuu kusikiliza maombi yao ya kuomba dhamana wakati rufaa yao ikisikilizwa.
Hongera zao, this is the law on bail pending appeal:
 

Attachments

  • BAIL PENDING APPEAL.pdf
    164 KB · Views: 65
  • BAIL PENDING APPEAL UGANDA.docx
    28.7 KB · Views: 67
Lema umetoka, Mathew umetoka, bado Lijuakali. Dhuluma haikuwahi kuishinda haki hata siku moja na kutokea kwa haya kumetufunza mengi ambayo tusingeyajua.
Walioanza na Mungu kwa nia ya kweli na haki daima watamaliza na Mungu! Na fisi waliojivalisha ngozi za kondoo wataishia kulialia mbele ya wachungaji huku wasijue pa kwenda!
 
Natamani haki itendeke wakati wote jamani japo ni kitu kigumu maana hata Yesu alipokuwa anawaponya na kutenda miujiza bado walimtungia uwongo
 
Back
Top Bottom