Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kibamba, Dar es Salaam Ernest Mgawe anashikiliwa na Jeshi la Polisi ikielezwa kuwa anatuhumiwa kutenda makosa mawili (2) ambayo ni kuhamasisha maandamano, na kuhamasisha watu kufanya fujo kwenye vituo na magari ya mwendokasi
Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 02.2025 na Wakili wake Dickson Matata imeeleza kuwa baada ya Mgawe kukamatwa jana, Oktoba 01.2025 mteja wake alipelekwa kwenye Kituo cha Polisi Oysterbay, ambapo akiwa kituoni hapo aliandika maelezo
Soma zaidi > Kamanda Muliro: Watatu wakamata kwa kuharibu Mabasi ya Mwendokasi, wengine wasakwa katika fujo Magomeni
Wakili Matata, anasema ilipofika majira ya Saa 06:30 usiku maafisa wa Jeshi la Polisi wakiambatana na mtuhumiwa na Wakili wake walielekea nyumbani kwa mtuhumiwa Kibamba kwa ajili ya kufanya upekuzi katika makazi yake
"Muda huu Saa 11:21 alfajiri ndio tumetoka Kibamba na kufika Oysterbay Police baada ya kumaliza zoezi la upekuzi ambalo (Polisi) hawajapata kitu chochote kinachohusiana na tuhuma zinazomkabili" -Wakili Matata
Katika maelezo yake, Wakili Matata amebainisha kuwa zoezi hilo lilikuwa linasimamiwa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Gogoni ASP Yahaya M. Omary aliyekuwa anatekeleza maelekezo ya RCO wa Kinondoni
Kuhusu suala la dhamana ya mteja wake, wakati anaandika taarifa hiyo alfajiri ya leo Wakili huyo alitoa wito wa subira, huku akiahidi kuendelea kufuatilia mchakato huo wa dhamana siku ya leo
Chanzo Jambo TV
CHADEMA ambao wamezuiwa kufanya shughuli zote za kisiasa!