Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete akutana na waandishi wa habari Lumumba

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akutana na waandishi wa habari asubuhi ya leo katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ndogo ya CCM Lumumba Jijiji Dar es salaam.

Mheshimiwa Kikwete ametembelewa ofisini kwake na mwanasoka bora Afrika kwa wachezaji wa ndani Mbwana Samata asubuhi hii na kufanya nae mazungumzo ikiwa ni sehemu ya kumpongeza kwa mafanikio hayo makubwa ambayo Mbwana ameyapata na heshima kubwa aliyoiletea Taifa kwa ujumla.

Baada ya mazungumzo hayo Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete, Mbwana Samata pamoja na Muenezi wa CCM ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Nape Nnauye walikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia mafanikio ya Samata na Kama Chama wamepokea vipi mafanikio hayo.

CYbU-0vUMAAiX1u.jpg

Nape Nnauye akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Lumumba.

CYbUo_zUMAEihY4.jpg

Waandishi wakifuatilia kwa makini Mazungumzo ya Samata na Mhe Jakaya Kikwete.

CYbUH81UMAEp5Xi.jpg

Mhe Jakaya Kikwete akizungumzo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Lumumba Asubuhi hii.

CYbTRVgWQAAeJyk.jpg

Mbwana Samata akiwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.
 
CCM na michezo wapi na wapi?viwanja vingi vya soka walivyovitaifisha wameshindwa kuviendeleza,Leo ndio wanamwona Samatta bidhaa yenye thamani kisiasa?Wamemtumia Diamond weee leo wamemgeukia huyu bwana mdogo.
 
Nimekimbilia huu Uzi nikifikiri anazungumzia maswala ya Zanzibar kumbe samata,
Samata na ccm wapi na wapi bora hata angemtembelea kikwete nyumbani kwake ingeleta maana kuliko kiingiza itikadi kwa mambo ya kitaifa.
 
Back
Top Bottom