GE2025 Mwenyekiti wa ADC Shaban Itutu: Tumeamua mwaka huu kila tunapotembea tutakuwa tunachinja Ng`ombe, tunataka tutoke draw na waliopeleka baiskeli

GE2025 Mwenyekiti wa ADC Shaban Itutu: Tumeamua mwaka huu kila tunapotembea tutakuwa tunachinja Ng`ombe, tunataka tutoke draw na waliopeleka baiskeli

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Shaban Itutu, amehoji uwiano wa mamlaka kati ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Tume Huru ya Uchaguzi, akisema kuna mgongano unaoweza kuathiri haki na uwazi wa uchaguzi.

Akizungumza Agosti 18, 2025, katika Mafunzo kuhusu Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vya Siasa kwenye Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Itutu amesema kuwa mgongano huo wa kisheria unajitokeza pale ambapo Msajili ana mamlaka ya kupokea pingamizi dhidi ya wagombea huku Tume nayo ikiwa na nguvu ya kuwaondoa wagombea.

"Suala la rushwa na misukosuko ya kisheria limekuwa likiwatoa wanasiasa kwenye mtiririko mzuri wa ushindani wa haki. Kwa sasa Msajili ndiye mwenye mamlaka ya pingamizi, wakati Tume nayo inaweza kuwaondoa wagombea. Hali hii inaleta mkanganyiko mkubwa," amesema Itutu

Aidha, Itutu amelalamikia kile alichodai ni unyanyasaji wa Polisi dhidi ya wagombea wa upinzani wakati wa kampeni, akisema baadhi yao hukamatwa bila sababu za msingi

"Polisi wamekuwa wakitusumbua kwenye kampeni. Wakiona mgombea ambaye hatokani na dola, mara moja anakamatwa. Tulishaomba hata kwenye mikutano kama hii na wao wawepo ili wajifunze kuwa kazi yao si kuwatisha wanasiasa," ameongeza

Akizungumzia Sheria ya Gharama za Uchaguzi, Itutu amesema haipaswi kuibana ADC, kwa kuwa chama hicho kimejipanga kwa kampeni za kipekee zenye muonekano wa kitamaduni na kisherehe

"Sisi ADC tumepanga kila tutakapotembea, kila kituo tutachinja ng'ombe. Mimi nikienda kuchukua fomu Jimbo la Ilemela, tutaanzia Dar es Salaam hadi Mwanza tukifanya ngoma na droo. Wengine wamepeleka baiskeli, sisi lazima twendane na droo yetu," amesema Itutu

Mafunzo hayo yamekusudiwa kuongeza uelewa wa viongozi wa vyama juu ya utekelezaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, sambamba na maandalizi va kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025




Chanzo: Habari digital
 
Hakika ng'ombe watapata tabu sana uchaguzi huu...
 
Back
Top Bottom