GE2025 Mwenyekiti wa ADC Shaban Itutu: Kauli ya Rais Mstaafu Kikwete ya 'Pumba na Mchele' inakejeli Upinzani na kuumiza Demokrasia, ajitokeze aombe radhi

GE2025 Mwenyekiti wa ADC Shaban Itutu: Kauli ya Rais Mstaafu Kikwete ya 'Pumba na Mchele' inakejeli Upinzani na kuumiza Demokrasia, ajitokeze aombe radhi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Taifa, Shaban Itutu, amemtaka Rais mstaafu wa Tanzania na Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuomba radhi kwa umma wa Watanzania kutokana na kauli yake kuhusu ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025

Itutu ametoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akihutubia mkutano wa kampeni wa chama hicho uliofanyika Buguruni, jijini Dar es Salaam, saa chache baada ya hotuba ya Kikwete

Kwa mujibu wa Itutu, kauli ya Kikwete kwamba “CCM hawapo tayari kuchanganya pumba na mchele” iliyotajwa kumaanisha kuwa wabunge wote wanatakiwa kuwa wa chama hicho, inaleta mashaka juu ya mustakabali wa demokrasia nchini.

"Sisi tukiwa tumejitoa kimasomaso kuionesha demokrasia ndani ya nchi yetu inatakiwa kuendelea kuwepo na kuilinda, leo Rais Mstaafu mbele ya wananchi wa Tanzania na vyombo vya habari anawaambia Watanzania kwamba CCM hawapo tayari kuchanganya pumba na mchele”, amesema Itutu

Katika mkutano wa kampeni wa CCM mkoani Pwani, Kikwete alisema Watanzania wana kila sababu ya kumchagua mgombea urais wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisisitiza kuwa amefanikisha kukabili changamoto nyingi zinazowakabili wananchi, hivyo ni muda wa kulipa wema huo

“Ninakuhakikishia kuwa wananchi wa Mkoa wa Pwani tutawachagua wabunge wote wa CCM, na ni imani yangu kuwa Tanzania nzima itakuwa hivyo. Hatuko tayari kuchanganya pumba na mchele,” alisema Kikwete

Itutu amesema angetarajia kauli za kuhamasisha ushindani wa kidemokrasia na siyo kuelekeza ushindi wa upande mmoja

“Mimi ningetegemea angesema tunakwenda kushindana na wenzetu, atakayeshinda atangazwe, atakayeshindwa abaki asitangazwe, hizo ndizo kauli za kidemokrasia na kauli za kidemokrasia za wanademokrasia waliokomaa kama Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete", ameeleza

Soma pia GE2025 - Kikwete: Wabunge wote wa Pwani bunge lijalo watatoka CCM, hatuko tayari kuchanganya pumba na mchele

 
20250929_093747.jpg
20250928_220449.png
 
Moja ya watu wa hovyo na wanaodharauliwa kwenye tasnia ya habari kwa sasa, huyo Balile nadhani anaongoza. Yaani akili yake yote kaitoa kichwani na kuihamishia tumboni.
 
Watu wengi hawamjui Kikwete. Kikwete ndiyo muasisi wa ushetani wote unaoendelra sasa:

1. Kikwete ndiye aliasisi utekaji. Kikwete ndiye aliamuru utekwaji wa Dr. Ulimboka.

2. Kikwete aliasisi mauaji ya wapinzani. Kikwete ndiye aliamrisha mauaji ya watu waliokwenda kwenye mkutano wa hadhara Arusha.

3. Kikwete ndiye muasisi wa mtandao wa ufisadi nchini.

Hivyo haishangazi kuona Kikwete anatoka hadharani na kuonesha sura yake halisi.
 
Back
Top Bottom