Mwenyekiti uda na jeuri ya ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti uda na jeuri ya ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by jambotemuv, Mar 6, 2012.

 1. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mwenyekiti Uda awashukia wabunge Dar
  Na Mwandishi wetu
  5th March 2012B-pepeChapaMaoni
  Meya Dk. Didas MasaburiMwenyekiti Mtendaji wa Kampuni Simon Group, Simon Kisena, amewashukia wabunge wa Dar es Salaam, kwa kuwataka waache kupiga kelele kuhusu uuzwaji wa shirika la usafiri Dar es Salaam (UDA ) wakati yeye anatoa fedha zake mfukoni kuwalipa wafanyakazi wa shirika hilo tangu Juni 10, mwaka jana.

  Akizungumza na NIPASHE mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, Kisena alisema anawashangaa wabunge hao kupiga kelele kuhususiana na uuzwaji wa shirika hilo na badala yake wajiulize anapata wapi fedha za kuwalipa mishahara wafanya kazi wa shirika hilo.

  Alisema kila mwezi anatoa mfukoni kwake shilingi milioni 70 kuwalipa wafanyakazi wapatao 98 mishahara pamoja na makato mbalimbali yanayotakiwa, hivyo wabunge hao waache kupiga kelele.

  "Jamani hawa wabunge na wengine wanaopiga kelele kuhusiana na shirika la Uda kwa nini wasijiulize kila mwezi napata wapi shilingi milioni 70 kuwalipa wafanyakazi? Fedha zote hizo natoa mfukoni kwangu," alisema Kisena.

  Kwa muda mrefu kumekuwepo na msuguano kati ya wabunge wa Dar es Salaam na Meya Dk. Didas Masaburi, baada ya wabunge hao kudai ubinafsishaji wa shirika hilo umefanyika kifisadi na ukiukwaji wa sheria.


  Nadhani swala halali zaidi ni M/kitu kutujulisha mfuko wake umepata wapi uwezo wa milioni 70 za kugawa kila mwezi. Wakishalewa ufisadi aibu zote huondoka.
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hawa mafisadi wawili Didas Masaburi na mwenzie wanafanya mambo haya wakijua fika kuwa nyuma yao wako viongozi wa nchi ; ama sivyo jeuri hii wasingekuwa nayo!! Nchi haiwezi kuendelea wakati viongozi wake ndio vinara wa kuiba mali zake. Mali zinaibiwa lakini kiongozi wa nchi anakaa kimya tu, maana yake nini?Nani asiyejua kuwa Riz1 ni mbia wa huyo jamaa aliyekwapua hiyo kampuni ya UDA? Msiwafanye wadanganyika wote kuwa wajinga.One day not in the distant future you will answer for your sins.
   
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  nadhani wako wengi wasiojua hili,tafadhali tujuze kwa kina!
  :A S-coffee:
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa aliyekwapua UDA aligombea ubunge jimbo moja lule Maswa akishindana na Shibuda,wakati wa kampeni Riz1 alikuwa kule kumsaidia ili awe mbunge na pia walishirikiana kwenye biashara ya pamba na jamaa ndio maana alifanikiwa kufisadi TIB zile fedha za STIMULUS package ambazo mpaka leo hajalipa!! Ukisoma kwenye magazeti ya mwaka 2010 wakati wa uchaguzi kule Maswa yaliyosababisha hata dereva mmoja kuuawa na purukushani zote zilizotokea mpaka Shibuda akawekwa ndani utapata taarifa zote hizi!!
   
 5. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu huyo jamaa anayesema anatoa hela zake mfukoni ana-interest ipi? Je ni kwa kuwa yeye ni mzalendo sana, ama kwa kuwa anawaonea huruma hao wafanyakazi wasikose chakula majumbani mwao, au kwa kuwa naye pia ananufaika na utendaji mbovu wa UDA?
   
 6. jambotemuv

  jambotemuv JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Swali kubwa labaki. Chanzo chake halali cha mapato kinachohalalisha uwezo wake wa kugawa milioni 70 kwa mwezi ni kipi? Anakusudiaje kuzirudisha pesa hizo bila kulazimisha kujiuzia shirika la uma na hivyo kuwapora wadanganyika chao?
   
Loading...