Mwenyekiti Kikwete, Dr. Magufuli anakuhitaji

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Ile timu ya makada nguli wa chama 32 kumpigia kampeni Dr. Magufuli na Samia S. Hassan imekumbwa na kanyamazongo. Haiko pamoja na haimsaidii Dr. Magufuli kama ilivyotarajia. Hata kilichotokea leo ni aibu hata kukiandika hapa. Natunza heshima ya chama changu.

Mwenyekiti Kikwete,unahitajika kwenye kampeni. Tayari Dr. Magufuli ameshajionesha kuwa anaweza kujisimamia. Tayari amejitangaza vya kutosha. Tayari amesikika ingawa shati wanamshika. Lakini,Mwenyekiti Kikwete yakupasa uingia kampenini. Timiza ahadi yako ya Lumumba kuongoza ngoma ya ushindi. Uko wapi?

Mwenyekiti,wanatimu uliowaamini hawaaminiki. Wanamimina matusi,kashfa zisizo na afya,kejeli za jeuri na maigizo. Wamemfanya hata Dr. Magufuli kuwa tapeli na muigizaji wa kisiasa. Usijitenge Mwenyekiti. Ingia ngomani. Mazuri yako yatambeba huyu. Hali inatisha kwenye kampeni. Si vutizi. Wenzetu watatupiga overtake na teke.

Mwenyekiti Kikwete,tafadhali okoa jahazi na hadhi ya CCM!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
Yupo na Sophia Simba kwa Obama kama mtu hajasalitiwa hapa sijui!!!
 
Kikwete Ana mambo meng mtoa maada mwache huyo wakaz apige kazi,,,,,,, mbona shein anajitoshereza Bila jazba wala kejeri,,,,.. Poleni ccm hata mm niliwapenda cna stress na m4c yang,,,
 
Wana macho ya kuona lakini hawataona, wana masikio ya kusikia lakini hawatasikia wana akili ya kutafakari lakini hawatafikiria, laiti wangekuwa wanasikia ujumbe wako mda mrefu sana wangekuwa angalau wamebadili upepo. ila ndio hivyo sikio la kufa halisikii dawa. acha wafu wazikane mzee Vuta Nkuvute.
 
Ila ccm waliaribu walipoanza
1. Kampeni za matusi(nape, kibajaji)
2.Kuongelea afya ya mtu badala ya sera
3. Kuwekeza sana kwawasanii
4. Kutumia wasaliti- pole pole nk
5. Kutumia wasanii kuvuta watu
6. Kuleta maigizo- push up nk
7.kupika tafiti za uongo
Hatari wanaoifanya sasahivi ni kuplankuiba kura. Hii wataifikisha nchi pabaya
 
Kikwete ndiyo ataharibu mambo. Tutamuuliza ahadi zake ambazo mpaka leo hakuna utekelezaji. Mfano tunataka meli kubwa Ziwa Victoria, iko wapi. Hospitali hazina madawa, rushwa tupu kwenye ofisi za Serikali. yeye ndiyo atapata aibu ya mwaka.
 
Kikwete ndiyo ataharibu mambo. Tutamuuliza ahadi zake ambazo mpaka leo hakuna utekelezaji. Mfano tunataka meli kubwa Ziwa Victoria, iko wapi. Hospitali hazina madawa, rushwa tupu kwenye ofisi za Serikali. yeye ndiyo atapata aibu ya mwaka.

Si ametekeleza kwa asilimia 80?
 
Yupo na Sophia Simba kwa Obama kama mtu hajasalitiwa hapa sijui!!!

Kwa hiyo Sofia na Kikwete, viongozi wa ccm wanamsaliti mgombea wao Magufuli kwa Obama?

Kama ni kunyume chake we hujui hata maana ya usaliti wala tofauti kati ya usaliti na unafiki.
 
Back
Top Bottom