Mwenyekiti chipukizi taifa atema cheche

Mwenyekiti chipukizi taifa atema cheche

MASIGA

Senior Member
Joined
Aug 29, 2015
Posts
130
Reaction score
281
Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa Ndugu Nimka Lameck leo tarehe 21/10/2018 ametembelea uchaguzi wa chipukizi unaoendelea katika wilaya za Kinondoni, Ubungo na Temeke ambapo amepata fursa ya kuzungumza na wajumbe wa mkutano mkuu katika wilaya hizo.

Akizungumza na wajumbe hao kwa nyakati tofauti Ndg Nimka amewataka wachague viongozi kutokana na sifa na uwezo wa kuwawakilisha na kuwasemea changamoto zinazowakabili watoto. Pia alikemea vikali suala la rushwa katika uchaguzi huo

"Naomba tumuunge mkono Mwenyekiti wetu wa CCM na Rais wa Tanzania katika kuipiga vita Rushwa kwa kutokubali kushawishiwa kwa vitu ili kumchagua kiongozi atakayetuongoza. Wote watakaobainika kuwashawishi kwa vitu tutawachukulia hatua kali kwa mujibu wa taratibu za Chama ili kulinda maadili yetu."

#KulindaNaKujengaUjamaa
#TukutaneKazini
IMG-20181021-WA0069.jpeg
IMG-20181021-WA0072.jpeg
IMG-20181021-WA0073.jpeg
 
Watoto wa mafisadi wakifurahia fedha za kifisadi wanazopewa na baba zao mafisadi
 
Huyo ni chipukizi au mama mzazi wa chipukizi? Umechanganya picha wewe
 
Huku wanaandaa viongozi kule wanasema tumtoe Mboyo atuongoze nani yaan hakuna kama yeye daah
 
..Duh!!

..hata uchaguzi wa chipukizi wa ccm una rushwa?

..au huyo mtoto anajisemea tu mambo aliyokaririshwa?

..watoto ktk mataifa yaliyo makini wanajishughulisha na masuala ya STEAM, yaani Science, Technology, Engineering, Arts, Mathematics.

..kwamba watoto wa Tz wanajishughulisha na Chipukizi badala ya hayo niliyoyaeleza hapo juu wanaopaswa kulaumiwa ni WAZAZI.
 
Back
Top Bottom