Mwingereza
JF-Expert Member
- Jan 21, 2014
- 1,115
- 2,771
Picha ya Zamani kumuonyesha mamba tatu. Samwel Kiboye
Mwenyekiti wa CCM wilaya Rorya Samwel Kiboye "Almaarufu kama namba tatu" leo akiwa kwenye kijiji cha Ryagoro alipokutanana wakereketwa wa CCM, amesema kwamba wanaokiua CCM ni viongozi wa CCM taifa. Mtu anapewa nafasi ya kuongoza, anageuka kuleta udikteta, kutishia watu kila segemu. Ikiwa kuna watu wasafi, basi tunataka kujua nyumba za serikali zilivyouzwa. Wengine wanaamua kuzuia bunge kuonyeshwa moja kwa moja kwa manufaa yao.
Hao wanaojiita viongozi wa kitaifa inabidi watafakari ni jinsi gani tulivyohangaika kufanikisha CCM kushinda uchaguzi mkuu. Tumeuza hadi nyumba zetu kwa ajili ya chama. Huyu kijana anayeropoka kila kona ya nchi inabidi chama imdhibiti, yeye ndiye anayetuvuruga na wananchi. Afukuzwe uwaziri na ndani ya chama. Kwenye vikao vyetu vya kitaifa, tutahakikisha anan'golewa. Chama kwanza watu bade.
Tumesikia wanamtishia Lakairo, wajaribu. Hawakumchagua ni sisi wana Rorya ndio tulimchagua. Hakuna anayeweza kumtishia Sibuor Simba, na wiki Ijayo ujumbe maalum tutaelekea Dodoma tukakutana naye mbunge wetu ili asimame kupigania Bunge Kuonyeshwa moja kwa moja. alisema samba tatu
Huyo Namba Tatu ni bonge la Tapeli Fulani hivi wa Siasa pia huwa ni mnafiki mkubwa yupo after money kazi yake kubwa ni upambe kwa mjumbe wa NEC Gachuma rafiki mkubwa wa Lowasa, Namba Tatu a.k.a Gerad tupo naye chadema kifikra ingawa kimwili yupo ccm lakini tatizo lake ni mtu asiyekuwa na msimamo pia ni Tapeli mkubwa kwa kivuli cha ikulu, huwatapeli wengi kwa kisingizio cha kuwafikisha ikulu kumaliza shida zao.anakuja sana Uganda kwa ndugu zake hapa yeye Asili yake ni mjaluo wa hapa Uganda sasa mda mwingi hufanya mambo yake hufanyia hapa.
Gerard a.k.a namba tatu ni mtu Tapeli mkubwa mali zake zote zikichunguzwa na Takukuru nina hakika watamkuta na hatia maana anamiliki mali nyingi kinyume na kipato chake. Utapeli namgendo na ujambazi. Huyu mtu kakalia kuti kavu....Magufuli huyu mtu anatumia jina la Ikulu kutapeli, wakati ni Lowassa CHADEMA Damu damu. Nape jipu hilo tunaona anakuponda
Aache kunywa viroba kabla ya kuongea ili aeleweke anakusudia kusema nini. Kwa sababu kama anamsema Magufuli lazima ajue matatizo ya kumsema Rais.
Hawa ndio mafisadi mnaowasikia. Mara Nyingi sana huyu mtu na Lameck Airo wanatishia watu, tena kwa kufyatuliwa bastola bila polisi kuchukua hatua wakati wapo. Miradi yote ya almashauri ya Rorya wanamiliki wao. Kwa mfano miradi yote ya Barabara wanamiliki wao. Watu watasema majungu lakini picha ndio hizo hapo
La-Kairo ni yule jamaa aliyekuwa Team Lowassa (mfadhili mkuu) kanda ya Ziwa, Lameck Airo, mbunge wa Rorya. Namba tatu alikuwa ni kama Katibu wa Mipango ya Lowassa