Mwenyekiti Bodi ya Parole kulikoni?

mafutamingi

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
2,772
2,171
Mara baada ya Mh Agustino Mrema kuteuliwa wadhifa wa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, alianza kazi kwa mbwembwe nyingi.

Kwa hamasa kubwa aliyokuwa nayo na wadhifa huo mara kwa mara alijikuta ana-overstep mandate yake. Lakini siku za hivi karibuni Mzee Mrema amekuwa kimya sana. Hatumsikii akifanya hiki wala kile.

Hatumuoni akitembelea magereza na mahabusu katika vituo vya polisi na kutoa matamko. Swali langu: nini kimempata huyu Mzee mpaka kupoa kiasi hiki? Au alitumbuliwa kimya kimya na wadhifa huo hanao tena?

Kwa namna alivyo mtu wa vituko, ni vigumu kuelewa kwa nini yuko kimya kama kweli wadhifa huo bado anao. Mwenye fununu atujuze
 
Mrema "Mzee wa Parole" amemsaidia sana Mbowe wakati akiwa magereza hasa kwenye issue ya diet!
 
Serekali haina pesa, na hicho cheo alipewa kama kuhadaa umma kwamba awamu hii imewapa nafasi mpaka wapinzani. Hivyo hicho cheo chake kwa ukata huu ni kama kuwa na bunduki isiyo na risasi. Ikitokea hitaji la propaganda atapewa fungu kisha atalishwa maneno ya kuja kutapika hadharani. Kwa sasa yeye ni bigG iliyoisha utamu.
 
Mara baada ya Mh Agustino Mrema kuteuliwa wadhifa wa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, alianza kazi kwa mbwembwe nyingi.

Kwa hamasa kubwa aliyokuwa nayo na wadhifa huo mara kwa mara alijikuta ana-overstep mandate yake. Lakini siku za hivi karibuni Mzee Mrema amekuwa kimya sana. Hatumsikii akifanya hiki wala kile.

Hatumuoni akitembelea magereza na mahabusu katika vituo vya polisi na kutoa matamko. Swali langu: nini kimempata huyu Mzee mpaka kupoa kiasi hiki? Au alitumbuliwa kimya kimya na wadhifa huo hanao tena?

Kwa namna alivyo mtu wa vituko, ni vigumu kuelewa kwa nini yuko kimya kama kweli wadhifa huo bado anao. Mwenye fununu atujuze
Nae yupo Gerezani
 
Nafikiri tangu alipotamka hadharani kwamba anatarajia kutumia bajeti ya parole kuendeshea chama chake cha TLP, naona fungu lilikatwa gafulale, Mzee wa kiraracha akazimika gafula!
 
Hivi wale Mrema ‘bashers’ wa Mzalendo zama zile wameishia wapi? Au ndio hawa Mbowe bashers wa awamu hii?
 
Back
Top Bottom