Mwenyeki CCM Wilaya ya Bagamoyo atimuliwa

Mwenyeki CCM Wilaya ya Bagamoyo atimuliwa

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Pwani, kimewasimamisha uongozi viongozi wake kadhaa wa Wilaya ya Bagamoyo, kutokana na madai ya kuuza kwa mwekezaji eneo linalosemekana kuwa ni mali ya chama hicho.

Waliosimamishwa uongozi ni mwenyekiti, katibu na katibu mwenezi wa chama hicho wilayani humo na habari zinasema uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Utendaji ya CCM, Mkoa wa Pwani.

Hata hivyo baadhi ya wafuasi wa chama hicho wamelalamikia hatua hiyo waliyoielezea kuwa ni ya uonevu.

Chanzo: Mwananchi.
 
Wanaofaidika na miradi mikubwa mikubwa wapo tu
 
Of course, hawawezi kuuza ardhi ya bagamoyo hasa iliyomikononi mwa chama bila kuiconsult loyal family.
 
Kwani aliyeuziwa naye si ni wa Chama Cha Zamani au?
 
Sasa wamewafukuza wanni,wakati uwezi kuwa mwanachama wa ccm bila kuwa na nyota ya PANYA?Kuingia ccm lazma uwe mwizi.
 
Wawafukuze pia na walioanzisha kampuni ya Jitegemee ili kuuza eneo kwa TPA!mi ccm yote majambazi.Kapt Komba mali zote za TOT kauza na kufanya zake binafsi.
 
Kama ni kweli , watakuwa wameonewa bhana ! Mbona Kinana hakusimamishwa ?
 
Back
Top Bottom