jjs2017
JF-Expert Member
- May 25, 2019
- 2,023
- 4,213
Habari ya asubuhi ndugu zangu.
Mimi ni kijana wenu mwenye umri wa miaka 30+, sijaoa wala sina familia na pia sina mwanamke yeyote wa kudumu,nakuja hapa kuomba kwenu ushauri wa kina juu ya haya mazingira ninayo ya pitia maana yamekua tishio kwa maisha yangu sasa na siku za usoni ndugu zangu, nisaidie kijana wenu
NIMEKUA NIKIKUMBANA NA MAZINGIRA HAYA NDUGU ZANGU
1: kuhisi upweke sana moyoni kiasi cha kujiona siyo binadamu wa kawaida
2: Napatwa na hisia za uchungu na hasira hali inayo pelekea kuhisi kama nataka kulipuka flani hivi. ( Yani kunakua na kitu kama natakiwa nikitapike au ni kipasue ndani ya moyo wangu kitoke niwe salama)
3: Mwili wangu na akili umechoka sana mpaka na jihisi mwili hauna energy ya kutosha na akili kuzimia
4: Nimekua ni kihema sana na kutoa hewa kwa nguvu ili mwili urelax
5: Nimekua mtu wakukosa amani moyoni kabisa ndugu zangu niwe kazini, niwe nyumbani au hata kwenye mikusanyiko ya watu
6: Sina marafiki wa kudumu hata mmoja kwa sasa na kuchangamana na watu najikuta tuu automatically hata nikiwa na watu bado nakuwa mpweke sana.
7: Sina furaha kabisa , japo na fake sana furaha ila kiukweli mimi sinaga furaha hata kidogo tuu
8: Nime kuwa ni mtu wa kuhisi na kuona imagination za matukio ya kutisha tisha na ya hatari tupu ndugu zangu kama ajali, vifo, mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu na manyanyaso makali , pamoja na vitendo vya kikatili sana kwa binadamu na wanyama
9: Nimekua ni mtu wa kukosa usingizi kabisa, japo mwili unataka muda wote uwe umelala tuu
10: Macho yangu ya mekua angavu sana inafika mahali nakua kama mtu mwenye kusinzia sana
HATUA NILIZO JITAHIDI KUZICHUKUA KUKABILIANA NA MAZINGIRA HAYO ILA ZIKAGONGA MWAMBA
1: Nilienda hospitali ya Rufaa nikakutana na wataalamu wa afya ya mwili nikawaelezea jinsi nilivyo, wakanielekeza kwa wataalamu wa afya ya akili ila niliishiwa kupewa dawa kama "amitrilia" na zikagonga mwamba baadae nilihamishiwa kwa specialist mmoja na kunipa dozi ya vidonge vya "phenobabiton"
2: Dawa zao ziligonga mwamba zote na madaktari wakanionyesha kukata tamaa na mimi japo hawakuniambia ila mazungumzo yao yalionyesha hivyo, waliingia mpaka library zaidi ya madaktari tano ila waliishia kuniambia katumie hizo dawa tuu na uombe sana.
3: Nimejitahidi kwenda kwenye maombi ila naona huko wananichanganya sana , kila mtumishi anaongea lake .
4: Nimejitahidi kujichanganya kwenye gym na viwanja vya mazoezi , pamoja na kupiga mazoezi makali sana ila hakuna badiliko chanya bado nipo hivyo hivyo
Ndugu zangu naombeni ushauri na msaada wenu nifanyaje ndugu zangu.
Asanteni
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app