Chaimaharage
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 211
- 78
Miezi michache iliyopita nilisikia taarifa zisizo rasmi kuwa Justice Rwakibalira alikimbwizwa India kwa matibabu ya ugonjwa wa ajabu uliompata. Baada ya hapo sijapata habari zake tena. Binafsi napenda kujua taarifa za huyu bwana sababu mara nyingi katika jamii watu wanaofanya mambo mabaya au kujulikana kwa mabaya(notorious) hupenda kuwajua ili kujiepusha nao. Vile vile wanaofanya mema jamii hapenda kuwajua pia ili na wao wajifunze kutoka kwao.
Alicho kifanya Justice Rwakibalira kuweka taaluma pembeni na kutii matakwa ya wanasiasa hatima yake inakuja kugharimu taaluma yake maisha yake yote. Ilibidi ajue kuwa wanasiasa ni watu wa kupita tu bali taaluma yake hubakia mpaka anakwenda kuzimu. Hakuna mtuhumiwa atakuwa na imani naye tena kwa kesi zote atakazo ziendesha iwe kwa haki au mizengwe. Na nina imani hukumu zake zote watu watakuwa wanazikatia rufaa ili kujiridhisha kama kweli zilikidhi matakwa ya kisheria.
Suala la pili napenda kujua hatima ya wapiga kura 3 walio pinga ubunge wa Mh.Lema. Nauliza hivi kwa sababu wote tuna amini kuwa walitumwa kwenda kufungua mashitaka yale, lakini hatujui nani haswa aliwatuma, ama Batilda au CCM. Sasa issue inakuja hivi; Ni wazi gharama za kuendesha kesi ile ni kubwa,je, moja, iwapo Batilda akiwaruka kwamba yeye binafsi hakufungua kesi bali walifanya vile kwa matakwa yao kwa hiyo hahusiki na kulipa gharama watakimbilia kwa nani? Pili kama CCM ndiyo iliwatuma(na ndivyo ilivyo kwa asilimia 99.999) nao wakiwa ruka kwenye kulipa gharama watashitaki kwa nani?
Ni wazi sasa hivi watakuwa kwenye wakati mgumu wakimuomba(Shetani) kati ya pande mbili nilizo zieleza wasiwageuke.
Naomba michango yenu wanajamvi katika hili, tujadili pasipo ushabiki ili siku za usoni iwe fundisho kwa wapiga kura watakao shawishiwa kufungua mashitaka pasipo kuwa na uhakika hatima itakuwa nini. Ni wazi pasipo shaka kuwa pande zote mbili yaani CCM na Batilda wakiwatelekeza wapiga kura hao basi itabidi wengine wauze mali zao kufidia kesi. Tunaomba aliyewatuma asiwatelekeze.