Mwenye taarifa za Justice Rwakibalira nijuzeni. Pia tujadili hatima ya wapigakura walomshitaki Lema

Chaimaharage

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
211
0
Miezi michache iliyopita nilisikia taarifa zisizo rasmi kuwa Justice Rwakibalira alikimbwizwa India kwa matibabu ya ugonjwa wa ajabu uliompata. Baada ya hapo sijapata habari zake tena. Binafsi napenda kujua taarifa za huyu bwana sababu mara nyingi katika jamii watu wanaofanya mambo mabaya au kujulikana kwa mabaya(notorious) hupenda kuwajua ili kujiepusha nao. Vile vile wanaofanya mema jamii hapenda kuwajua pia ili na wao wajifunze kutoka kwao.

Alicho kifanya Justice Rwakibalira kuweka taaluma pembeni na kutii matakwa ya wanasiasa hatima yake inakuja kugharimu taaluma yake maisha yake yote. Ilibidi ajue kuwa wanasiasa ni watu wa kupita tu bali taaluma yake hubakia mpaka anakwenda kuzimu. Hakuna mtuhumiwa atakuwa na imani naye tena kwa kesi zote atakazo ziendesha iwe kwa haki au mizengwe. Na nina imani hukumu zake zote watu watakuwa wanazikatia rufaa ili kujiridhisha kama kweli zilikidhi matakwa ya kisheria.

Suala la pili napenda kujua hatima ya wapiga kura 3 walio pinga ubunge wa Mh.Lema. Nauliza hivi kwa sababu wote tuna amini kuwa walitumwa kwenda kufungua mashitaka yale, lakini hatujui nani haswa aliwatuma, ama Batilda au CCM. Sasa issue inakuja hivi; Ni wazi gharama za kuendesha kesi ile ni kubwa,je, moja, iwapo Batilda akiwaruka kwamba yeye binafsi hakufungua kesi bali walifanya vile kwa matakwa yao kwa hiyo hahusiki na kulipa gharama watakimbilia kwa nani? Pili kama CCM ndiyo iliwatuma(na ndivyo ilivyo kwa asilimia 99.999) nao wakiwa ruka kwenye kulipa gharama watashitaki kwa nani?

Ni wazi sasa hivi watakuwa kwenye wakati mgumu wakimuomba(Shetani) kati ya pande mbili nilizo zieleza wasiwageuke.

Naomba michango yenu wanajamvi katika hili, tujadili pasipo ushabiki ili siku za usoni iwe fundisho kwa wapiga kura watakao shawishiwa kufungua mashitaka pasipo kuwa na uhakika hatima itakuwa nini. Ni wazi pasipo shaka kuwa pande zote mbili yaani CCM na Batilda wakiwatelekeza wapiga kura hao basi itabidi wengine wauze mali zao kufidia kesi. Tunaomba aliyewatuma asiwatelekeze.
 

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,236
1,500
Kuhusu gharama za kesi, nadhani utakuwa wakati mgumu kwa wale watu 3 waliofungua kesi. Ninawashauri CDM wasiwasamehe katika hilo ili iwe fundisho kwa watu wengine wasioweza kutumia akili zao bali kutumiwa na watu wengine. Nina mashaka kama CCM itakuwa tayari kuwasaidia kulipa gharama za kesi.

Mwaka 1995 (kama sikosei) katika jimbo la uchaguzi la Karatu, aliyekuwa mgombea wa CCM, Ndugu Patrick Qorro alifungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa jimbo hilo uliompa ushindi Dr. Slaa. Hukumu ilitupilia mbali madai ya mlalamikaji yaani Patrick Qorro. Inasemekana CCM walimponza kwa kumwambia Qorro kwamba afungue kesi na kwamba watamsaidia lakini baadaye wakamtelekeza. Kwa bahati Dr. Slaa akamsamehe gharama za kesi.

Ninashauri CDM wasitoe msamaha wa aina yoyote katika suala hili, hata kama hawana fedha za kulipa gharama za kesi wafilisiwe ili wasirudie upuuzi walioufanya.
 

Kanundu

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
889
0
Na kwa tabia hii ya kuwa samehe gharama za kesi, ndiyo kunaleta watu kujipendekeza na kujifanya wamenyimwa haki za kupiga kura na mambo mengine kedekede!

CHADEMA hakuna kusamehe kitu. Kumbukeni damu nyingi za waTanzania zimemwagika kutokana na dhuluma katika chaguzi mbalimbali hasa pale CHADEMA inapoonekana ni tishio.

Walipe gharama zote za kesi hii.
 

Babkey

JF-Expert Member
Dec 10, 2010
4,832
2,000
...ila inachekesha...wanadai matusi na kashfa ziliathiri watu kupiga kura...ajabu ya walimwengu washitaki wenyewe walipiga kura.
 

mchaichai

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
648
0
wakome washenzi wao! watu wenyewe wamepaukaa!hawana hata nguo za maana wanafungua kesi nyuso zao taabu tupu...ningekuwa na mamalaka kwa hasara ya time ningewashona risasi watu kama hao
 

bornagain

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
3,386
2,000
Waliotumwa chali, judge chali na waliotuma kisirisiri chali pia,chezeya nguvu ya UMMA wewe.CCM sasa wameamua kuchagua fungu la kukosa ili kuleta amani Arusha maana wangechemsha kingenuka tena
 

Kishalu

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,173
2,000
kwa mantiki ya kichwa cha habari huyu ndg Jaji Gabriel Rwakibalira alikuwa mgonjwa na alikuwa anatibiwa India lakini tangia mwezi wa kumi alikuwa amerudi na tayari alikuwa anafanya mazoezi huko kwake nyumbani Kimara Temboni mtaa wa Matosa ,kila jioni alikuwa anatoka na fimbo yake na kutembea kama umbali wa 2km na kurudi home kwa ujumla hali yake ilikuwa inaendelea vizuri toka alipotoka India sijui kwa sasa[h=2][/h]
 

james chapacha

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
939
195
walipe na zote tunanunua mashine za kufua mashuka ya wagonjwa mt.meru hosptl kufidia zile zilizo bebwa na msomali
 

majaar

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
1,356
1,195
Huyo jaji anaumwa ugonjwa wa lemafhobia ni ugonjwa mmbaya sana huo inabidi apate maombezi na kutubu makosa yake kanisani labda mungu anaweza kumsamehe.
 

Jallen

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
516
225
Rwakibarila anaendelea viuri lakini kiogo angekufa maana alipata stroke
 

DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,640
2,000
Nasikia Mfungua kesi Musa Mkanga ameanza kutuma ujumbe kwa Nape ili gharama zilipwe na ccm ila ametoswa.ANA MPANGO WA KUUZA NYUMBA.
 

Jangakuu

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
514
250
kwa mantiki ya kichwa cha habari huyu ndg Jaji Gabriel Rwakibalira alikuwa mgonjwa na alikuwa anatibiwa India lakini tangia mwezi wa kumi alikuwa amerudi na tayari alikuwa anafanya mazoezi huko kwake nyumbani Kimara Temboni mtaa wa Matosa ,kila jioni alikuwa anatoka na fimbo yake na kutembea kama umbali wa 2km na kurudi home kwa ujumla hali yake ilikuwa inaendelea vizuri toka alipotoka India sijui kwa sasa
juzi juzi kuna mwandishi wa habari alimtembelea na kumuuliza je kesi ya lema unaionje atashinda, akasema lema lazime ashinde!!!
 

yegella

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,113
1,250
kuna tetesi yuko hoi hasa baada ya huku yake kuonekana niushuzi mtupu..nilikuwa naomba asife kabla lema hajarudishiwa ubunge sasa lema ni mbunge kufa salama mubaka haki..
 

artorius

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
757
0
kama ulimwona tundu lissu leo kwenye eatv amesema,''gharama zote za uendeshaji wa kesi lazima wazilipe,ole wao washindwe kulipa,tutawafunga''
 

Nicholas

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
25,264
2,000
Wanaweza samehewa iwapo watapanda jukwaani siku inayofaa na wakiri jukwaani walitumwa na nani na kwanini>kama wachawi wakirivyo mbele ya kakobe na Joe David ili wapate msamaha huo n akuiabisha CCM.Watakuwamelipia kwa nguvu zao na watakauwa wamegeuza uovu kuwa ushindi kwa walio wa haki
 

cacasi

Senior Member
Dec 21, 2012
156
0
Na kwa tabia hii ya kuwa samehe gharama za kesi, ndiyo kunaleta watu kujipendekeza na kujifanya wamenyimwa haki za kupiga kura na mambo mengine kedekede!

CHADEMA hakuna kusamehe kitu. Kumbukeni damu nyingi za waTanzania zimemwagika kutokana na dhuluma katika chaguzi mbalimbali hasa pale CHADEMA inapoonekana ni tishio.

Walipe gharama zote za kesi hii.
mkubwa punguza uchungu na hasira, kwani watu wenyewe wanavyooneka hawa uwezo wa kulipa hizo gharama , ni bora mh Lema na CDM wakafikiria kuwasamehe hizo gharama za kesi, kwa mfano hata kama wakishindwa kulipa na wakafungwa jela si MH Lema hata CDM itakayokuwa kuwa imepata faida yoyote, kwani maandiko yana seme" samehe 7 x70"
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom