mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,789
- 7,185
Ni tukio la kusikitisha sana mwenye nyumba Ndugu Ali Mbonde amenitapeli yeye na dada yake Tatu Mbonde,
Ilikuwa hivi, niliona frem za biashara pale Tegeta Kibaoni stand ya zamani ya magari yatokayo Bunju na Bagamoyo, frem hizo zilikuwa ndio zinajengwa msingi, nilimfuata mwenye frem na kuuliza kama kuna frem za biashara alinieleza zimebaki mbili miongoni mwa frem tano, aliniambia zitachelewa kumalizika kwani nimepanga zianze rasmi mwezi wa saba, hapo ilikuwa mwezi wa tano kama kawaida nikaenda benki yangu ya Akiba C. nikamtolea million 1.8 kwani frem ni 150, huyu tapeli aliniomba nilipe miaka miwili ili apate fedha za kumaliza haraka,
Nikamshauri kama hana fedha akakope benki tena wanampa fasta, sijui kama alienda au la, huyu tapeli alijenga kwa kasi na akashauriana na mafundi wake waongezee wafanye hiyo nyumba iwe ghorofa, basi ikaanza kubadilishwa kuwa ghorofa,
Frem za chini zilimalizika mwezi wa tisa, nikamwambia basi niwekee frem na umeme nianze biashara, akanieleza nivute subira mpaka wa kumi, wakumi hakuna kitu, nikaanza kumdai kila baada ya wiki, ilipofika wiki zaidi ya mbili, watu wakaanza kuvamia frem na kuweka milango nilipomuuliza mbona wangu uniwekei akadai watu hawa wamevamia frem zao nitazingoa ili niweke zangu nilishachongesha.
Nilimfuta mpangaji mwezangu kumuuliza kulikoni akaniambia huyu mwenye nyumba ni tapeli sana hivyo sisi tumeshindwa kumvumilia kwani hizi frem zina zaidi ya watu 12. Hivyo nawe weka frem (Mlango) ufunge mpaka akuwekee umeme. wkati najiandaa kuweka frem hivyo ananiita akaniambia frem hiyo siyo yako nilikosea frem yako iko juu ya ghorofa.
Nikamwambia haiwezekani kwani nilikuambia biashara zangu nitauza spea za magari na pikipiki akaniambia kama hutaki kuchukua juu basi nikurudishie fedha zako. Niliamua kumpeleka kwa mwanasheria wangu akatuita mwanasheria akambana arudishe pesa, akahahidi tarehe 7/02/2013 siku ilipofika akaja na maneno na kuomba siku kumi na nne, mpaka sasa amezima simu mara ya mwisho alituma message kuwa amefiwa na mama mkwe.
Kama kuna ushauri nishauri nifanyeje?