Mwenye nyumba, Mpangaji, Dalali

Mwenye nyumba, Mpangaji, Dalali

Head current

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2013
Posts
479
Reaction score
128
Wakuu embu tusaidiane mawazo, eti nyie mnaonaje unatafuta nyumba ya kupanga yenye gharama ya sh 200,000 kwa mwezi kutokana na vigezo unavyohitaji, then baada ya kupata unamlipa mwenye mjengo kwa miezi mliokubaliana; na baada ya hapo eti inakubidi umlipe dalali aliyekutafutia, hiyo nyumba mwezi mmoja wa pesa unazolipa hapo; je? wakuu me najiuliza kwa upeo wangu kwa nn? dalali asilipwe na mwenye mjengo? na pili hivi mwenye shida ni mwenye mjengo kupata mpangaji? au mpangaji kupata mjengo? nisaidieni mawazo,,,
 
unadhani mwenye nyumba ndo ana shida na mahala pa kuishi?
 
BADILI TABIA;unadhani mwenye nyumba ndo ana shida na mahala pa kuishi? hpn mkuu ila upande wa pili wa shilingi asingejenga nyumba za wapangaji km hana shida na wapangaji; nachoona sio sahihi ni hilo swala la mpangaji kumlipa dalali pesa ya mwezi mmoja kwa kiwango mlichokubaliana; na kwa nini iwe ni ya mwezi mmoja kwa kiwango mlichokubaliana? na pili kwa nn? alipe mpangaji na sio mwenye nyumba? je sheria inasemaje kuusu hilo?
 
Wote wawili mpangaji na mpangishaji wanashida, na dalali inabidi alipwe, ila tatizo madalali wanataka pesa nyingi tena wanakula kote kote kwa mpangaji na mpangishaji.

Ifike wakati hawa madalali waaze kulipa kodi na wapangiwe viwango vya kuwatoza wateja wao, siyo kama sasa kila mtu analipisha anavyotaka.
 
Hakika nchi hii ni kama haina sheria,kuna watu wao wananeemeka kwa shida za wengine pasipo hata yone la jasho!Zaidi madalali ndoi wamekuwa wakipandisha kodi za nyumba kwa mwezi ili kipato chake kwa mwezi kiongezeke mathalani kodi ni 150,000 anaongeza kusudi utakavyolipa nyingi na yeye apate zaidi,mpangaji anajikuta anapigwa mara 2 zaidi,kuna haja ya kusajili kampuni binafsi za madalali ili walipe kodi na pia kuwe na mwongozo wa kiwango stahiki cha kodi!
 
Hakuna Sheria inayomtaka yeyote katika hao kuchukua cha juu zaidi ya Kodi ya chumba.
Kama umeridhika na chumba chukua anwani yake mwenye nyumba (simu yake au kuangalia anapokaa ) rudi usiku malizana nae wakati Dalali hayupo
Kwa kukomesha kabisa muandikiane
Mtu aliyeko Kisheria au mwenye Mamlaka ni yule anayesimamia mkataba wa upangaji ambaye zaidi huwa ni Mwanasheria ambapo km unahisi mnaweza shindwana katika upangaji hasa katika mambo ya kufukuzana kabla Mkataba haujaisha au kutokulipa Kodi ya chumba (Pango) kwa miezi 6 mfululizo ndio mnaweza kwenda kwake. Na huyo Mwanasheria atawachaji si zaidi ya 5% ya kodi au Gharama za Mkataba si zaidi ya 50,000/=) ambapo atasimamia mapatano yenu kwa mwaka huo wa Mkataba
Mimi yalishanitokea na huwa nawafukuza Mdalali na kumuita mwenye kuhitaji kupanga kwani huyo ni ndugu wakati wa kupanga na hata zaidi ya hapo
Uzuri wa Madalali ni kama nyumba yako haina soko au iko mbali na Mji na kumlipa na mapatano na mapenzi yenu (Asante)
 
Ukwaju acha ukauzu bana. hahahh.
Lakini nikweli hawa madalali ni kero,japo wanasaidia kurahisisha utafutaji wa huduma. Mimi nilibahatika wakati huo kupanga kwa Prof fulani, yeye alisema gharama ya tozo ya dalali mnaichangia nyote,yaani mwenye nymba na wewe mpangaji. Si sawa kutomlipa dalali aliyezunguka nawe kutafuta nyumba. Japo unapaswa umlipe kiasi..not necessarily kodi ya mwezi.
 
Last edited by a moderator:
madalali ulimwenguni kote wapo ki-commercial wanaitwa BROKERS, sema kwa hapa tz wengi hawana leseni pia hawalipi kodi serikalini. kiukweli huwezi kupata nyumba, gar, kiwanja, kazi n.k bila kupitia madalali!! hata hizi recruitment agencies ni madalal
 
hili ndo tatizo la kuwa na serikali isiyojenga apartments kwa wananchi wake, biashara ya nyumba ilitakiwa imilikiwe na serikali na hii ingeongeza kipato cha serikali, leo hii wenye nyumba hawalipi kodi na wanajipangia kodi wenyewe. very shame!
 
Ukwaju acha ukauzu bana. hahahh.
Si sawa kutomlipa dalali aliyezunguka nawe kutafuta nyumba. Japo unapaswa umlipe kiasi..not necessarily kodi ya mwezi.
Du wewe kauzu kwelikweli kumbe ni lazima utongozewe? huwezi tafuta mwenyewe?
uanweza tafutiwa Demu mpaka leo?
ok sorry km ni mgeni kwenye miji mikubwa kwa kutafuta Gari, nyumba nk mpaka upate mtu wa kuongea nao
Mm ni nyumba na ninapangisha hawa watu siwakubali kabisa, kuna siku nilitangaza kuuza shamba walikuwa wanawaleta wateja nikizunguka pembeni na Mteja baadae akiondoka nae wananisingizia Shamba linadaiwa na BENKI wateja hawarudi. Nilichoamua ni kulikata vipandevipande katika Farm 57 Msalato Dodoma mbona ndani ya wiki nilimaliza kuliuza lote
 
me nina nyumba ipo k,ndoni naipangisha ila sitaki dalali.
 
Hakika nchi hii ni kama haina sheria,kuna watu wao wananeemeka kwa shida za wengine pasipo hata yone la jasho!Zaidi madalali ndoi wamekuwa wakipandisha kodi za nyumba kwa mwezi ili kipato chake kwa mwezi kiongezeke mathalani kodi ni 150,000 anaongeza kusudi utakavyolipa nyingi na yeye apate zaidi,mpangaji anajikuta anapigwa mara 2 zaidi,kuna haja ya kusajili kampuni binafsi za madalali ili walipe kodi na pia kuwe na mwongozo wa kiwango stahiki cha kodi!

Hawa madalali ndo wamesababisha hapa dar nyumba kuwa ghali sana na maisha ya wapangaji kuwa magumu sana siwapendi kabisa na mimi nimejipangia kila wanapo nitafutia house pesa ya kuwapa nawapangia mimi mwenyewe wanaboa sana... Ziwekwe sheria kama naigeria ukijenga nyumba ya biashara hiyo siyo yako serikali ndo inakupangia kiwango cha kodi kulingana na uthamani wa nyumba.
 
Kama we ni dalali wa nyumba na Magari niandikie namba zako hapa Natafuta madalali kuna kazi nataka niwape
 
Pole ndg, hata kwangu ilisha nitokea, na hapa kwetu Tz imekuwa kawaida kama utaratibu halali!

Mkuu kutokana na uhaba wa Nyumba hapa Tz wapangaji wote wamekuwa wakinyanyasika sana, ikiwemo kulipishwa pango la miezi 6 au mwaka mzima (miezi 12) kwa kutanguliza ( in advance/prepayment).

Pesa kutorudishwa kutokana na kukiukwa kwa makubaliano baina ya pande zote 2. Nadhani ni muda muafaka wa kuomba wizara husika ikaleta sheria nzr ya kubana pande zote 2.

Nakumbuka Mhe: Mnyika aliwahi kusema Bungeni kuwa Tz ndio nchi pekee ambayo mpangaji analipa nyumba kwa miezi 12!!!!
 
Nyie wapumbav kweli. dalali halali ni yule aliyesajiliwa, na ana ofisi. unapomfuata na kumweleza shida zako mnakubaliana, unakuwa umempa kazi, LAZIMA UMLIPE KWA MUJIBU WA MAKUBALIANO. Wapangishaji walioko kibiashara anamkabidhi nyumba/vyumba/chumba dalali na kukubaliana naye atamlipa kiasi gani, akishapata mteja analipwa na mwenye nyumba wala hana shida na wewe. Elewa gharama mkubaliane kabla haujampa kazi mtu, mtu aungue jua kukutafutia nyumba wewe bure umekuwa babaake, ACHENI DHURMA!
 
Back
Top Bottom