Mwenye kumbukumbu ya ajali ya moto shule ya Shauri Tanga

reuben kombe

Member
Jul 8, 2016
53
54
Kwa yeyote yule mwenya historia ya tukio hilo lililotokea zaidi ya miaka 20 iliyopita atupe japo dondoo kazaa,
 
Ilikuwa ajali mbaya sana kupata tokea Tanzania.
Ilihusishwa na mauza uza na pia masuala ya kiufundi hasa mambo ya umeme.
Kipindi hicho Waziri mkuu akiwa ni mshua wake Le Mutuz mzee Malecela John .

Ilitokea mnano 18 June 1994. Wapelelezi wa scotland yard toka Uingereza walifanya
kazi kubwa sana ya kutoa ripoti ya kilichosababisha janga lile la moto ambalo liliondoa
roho za wanafunzi wengi sana ( wanafunzi 42) huko wilayani Rombo , mkoani Kilimnajaro.

Moto mkubwa ulizuka Bwenini na kusababisha vifo vyote hivyo, kwa sasa wamejengewa mnara kama kumbukumbu ya kutokatishwa tamaa na majanga pindi yanapotokea.

Hule hiyo kwa sasa ina milikiwa na Jumuia ya wazazi wa CCM na muanzilishi wa shule hiyo
alikuwa ni Padre (Father) aliyeitwa Padre Aloyce Shauritanga

Bweni husika

upload_2017-5-8_14-24-27.jpeg

kaburi lao la pamoja hili hapa baada ya kukarabatiwa upa.

upload_2017-5-8_14-19-56.jpeg


Hapa ni picha ya kaburi lao kabla ya ukarabati.

upload_2017-5-8_14-22-6.jpeg

upload_2017-5-8_14-12-33.jpeg
 
Walikufa wanafunzi 32.
Walikufa wanfunzi 42 wote waliungua moto na maiti hazikutambuliwa kabisa mimi nilikuwa form three ,lakini lilikuwa tukio la kushutua nakumbuka wakuu wa shule mkoani Kilimanjaro walikaa kikao wakatoka na maazimio kuwa kila mwanafunzi hawe mlinzi wa mwenzake sisi shuleni tuliweka sungusungu tulikuwa tunalinda kwa zamu masaa matatu wengine wanaendelea
 
Walikufa wanfunzi 42 wote waliungua moto na maiti hazikutambuliwa kabisa mimi nilikuwa form three ,lakini lilikuwa tukio la kushutua nakumbuka wakuu wa shule mkoani Kilimanjaro walikaa kikao wakatoka na maazimio kuwa kila mwanafunzi hawe mlinzi wa mwenzake sisi shuleni tuliweka sungusungu tulikuwa tunalinda kwa zamu masaa matatu wengine wanaendelea
Mkuu wakati bweni linawaka moto hawakuwepo waokoaji? Liliteketea usiku au mchana?
 
"Shauritanga tukabaki na matanga,
waliua wasichana vijana wenzetu,
walikosa nini maskini?
mapea kama vile kuwapeleka kaburini!
mi nasikitika, nahangaika napita huku kule mambo yamerabika
namkumbuka sokoine,
mpaka hii awamu ya tano nani mwingine afanane?
ni wapi tunakwenda?

II Proud
 
Wapumzike kwa amani Dada zetu hawa. Kila nafsi itaonja mauti
 
Usiku wa manane, wakiwa wamelala, moto mkubwa ulizuka. Mabinti wale walipiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa walinzi hawakufanikiwa hadi wakafa wakiwa wamejikusanya sehemu ya mlango uliokuwa umefungwa na walinzi kwa nje.

Viongozi wa Serikali walikimbia haraka sana, wakatoa kauli nzito za kulaani kilichoonekana kuwa kama hujuma na wakaahidi kwamba tukio hilo halitajirudia tena. Kinachosikitisha ni kwamba miaka 22 baadaye, bado shule zinateketea kwa sababu huenda zinazofanana na tukio la Shauritanga
 
Back
Top Bottom