Mwenge wa uhuru unaposimamisha masomo

May 24, 2012
54
10
Mwenge wa uhuru ulipokuwa umekesha Mjini Mafinga Wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa siku ya Jumapili 20/05/2012 kuamkia jumatatu, siku ya jumatatu wanafunzi hawakwenda shule eti kwa sababu walimu wao walikesha na mwenge, hivyo shule zote za msingi za mjini Mafinga hawakwenda shule kwa agizo la viongozi wa HALMASHAURI ya Wilaya
 
Ukistaajabu ya Musa utaona ya firauni. Taarifa nilizopokea kutoka Njombe ni kuwa Madiwani wa Halmashauri ya Njombe ambao walikuwa kwenye msafara wa Mwenge wamesusia Mwenge huo kwa madai kuwa Mwenyekiti wa CCM (W) ya Njombe alizuiwa kuongoza Msafara wa Mwenge akiwa anapeperusha bendera ya Chama. Unaweza kuona walio uasisi Mwenge wenyewe wanaukana kwanza kwa kuingilia taratibu za itifaki ambazo waliziweka wenyewe na pili kwa kukana mtoto wao wenyewe. Nadhani ipo haja ya kuangalia upya taratibu za itifaki katika masuala mbalimbali hasa yanayohusu viongozi wetu wakuu. Iko siku Rais mwenyewe atasusiwa na viongozi wa Chama chake. Walioko Njombe watatujuza zaidi nini kimeendelea. karibu Mbeya.
 
Jamani ifike wakati tuseme ukweli huu mwenge usikimbizwe tena kwani unatumia pesa nyingi pasipo sababu ya msingi,sasa imetosha uwekwe jumba la makumbusho.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom