GE2025 Mwenezi wa CCM Arusha aahidi kuwalipia nauli abiria wakapige kura

GE2025 Mwenezi wa CCM Arusha aahidi kuwalipia nauli abiria wakapige kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Saipulan Ramsey, amewaasa maafisa usafirishaji (bodaboda) kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upigaji kura linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Ramsey amesema baada ya bodaboda kupiga kura, wanapaswa kuendelea na shughuli zao huku wakihamasisha abiria wanaowabeba kwenda kupiga kura, ambapo aliahidi kuwalipia nauli abiria hao akisema “Ukirudi ukakutana na abiria ambaye hajapiga kura mpeleke akapige kura na umwambie mwenezi ameshakulipia nauli.”

Kauli hiyo ya Ramsey inakuja ikiwa zimesalia saa chache kabla ya kufanyika kwa zoezi la upigaji kura, ambapo ametoa wito kwa vijana na wananchi wote wa Arusha kujitokeza kwa amani na utulivu kushiriki katika mchakato huo muhimu kwa mustakabali wa nchi.
 
  • Fire
Reactions: Tui
Back
Top Bottom