Mwenendo wa Siasa Ndani ya NEC na Unafiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenendo wa Siasa Ndani ya NEC na Unafiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KING COBRA, Nov 26, 2011.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]
  HIVI NCHI INAKWENDA WAPI????
  Wakati Lowassa anamushambulia Kikwete Rais Mkapa alikuwa anafurahia
  Hivi Mkapa ni Msafi kuliko Kikwete??
  Lowassa alimuweka Kikwete Madarakani , Kati ya Kikwete na Lowassa nani alijilimbizia Mali kabla??
  Rais Mkapa ndiye anatajwa katika kipindi Chake Kuiba fedha nyingi Serikalini na Mgogoro wa EPA Ulikuja Kipindi Chake[/FONT]

  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Rais Mkapa , Mkewe ndiye Walipora Nchi na Kujimilikisha mgodi wa Kiwira kama Familia ambapo Mkwe Wake Marehemu Joseph Mbuna ndiye aliye kuwa Kinara[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Sasa mimi nimeshangaa kidogo kuona kwamba Rais Mkapa anaungana na Fredrick Sumaye Kumusakama Rais Kikwete Wakati wote ni Wezi.[/FONT]
  [FONT=&quot]Ukiangalia ukweli ni kwamba Lowassa anasema suala la Richmond alifanya kwa maelekezo yake lakini Lowassa huyo huyo anasahau kuwa Baba wa Taifa alisema Lowassa ni Mwizi na Kikwete bado ni Mtoto Mdogo kuongoza nchi . sasa hebu angalia kati ya Lowassa na kikwete yupi ni Mtoto???[/FONT]
  [FONT=&quot]Utagundua kuwa Lowassa ni motto isipokuwa ni Mwizi ??[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Malalamiko ya Lowassa ni kwamba yeye na Rostam ndio waliomuweka Kikwete Madarakani kwa uwezo wao wa pesa !!![/FONT]
  [FONT=&quot]Sasa Hapo tunapata hoja kwamba Nyerere alikuwa sahihi kwani hizo pesa ambazo Lowassa aliyumia kumuweka KIKWETE madarakani yeye(Lowassa ) alipata wapi???[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Hivi Lowassa kama asingekuwa Mwizi kwa nini asinge mpinga Kikwete wakati wanapanga kuibia Nchi lakini wakakubaliana ajiuzulu ili aje awe Rais Waendelee Kutuibia!!![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Hivi hapa ni kweli kwamba Lowassa kasema ukweli , ni kwa nini hajaeleza mipango yao ya yeye kujiuzulu ili anusuru serikali kwa maslahi ya nani???[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Nini mipango baada ya Lowasa kujiuzuru??[/FONT]
  [FONT=&quot]Hapa Kikwete naye aseme Lowassa amekosea nini mpaka mipango hiyo imepoteza Mwelekeo???[/FONT]
  [FONT=&quot]Hivi Jambazi akimutaja mwezake anasameheka??[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Ni Kwa nini Lowassa aseme Mambo hayo sasa hivi tunapokaribia Uchaguzi???[/FONT]
  [FONT=&quot]Kwani Lowassa lazima awe Rais 2015 hakuna watu wengine??[/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa nini Watu wenye kashifa za Wizi ndio wagombea wa Urais na ndio waliopora fedha na kutumia kuwahonga Wananchi??[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mimi natoa Rai kwa Kikwete naye asimame kama Major wa Jeshi kupambana na Jeshi la uasi wa Lowassa ambalo linatka kupindua nchi .[/FONT]
  [FONT=&quot]Tanzania[/FONT][FONT=&quot] haiwezi kuongozwa na watu wenye Kashifa Kama Lowassa eti kwa sababu tu Kasema kwamba suala la Richmond ni Kikwete alimtuma je Wakati Nyerere anasema Lowassa ni Mwizi nani alimutuma Lowassa kwenda kuiba???[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Hivi Lowassa anakashifa moja tu!!![/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Fredy Lowassa anamambo kadhaa Mabaya !!!!!!!!!![/FONT]
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,790
  Trophy Points: 280
  Sielewi CCM wanafikiri nini. But I suspect some big guys are up for something to end once and for all,this political puzzle
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  naona bado mnaweweseka ukweli ndo huo Lowassa is the man na Kikwete hamfanyi kitu sababu ye ndo mbovu, fisadi, mwizi na mnafki
   
 4. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #4
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot] UTETEZI HUU WA LOWASSA UNAONYESHA KWAMBA YEYE NI MZALENDO???
  MBONA DAVID JAIRO ALIJITETE HIVYO LAKINI BADO HAKUSAMEHEWA??

  Neville Meena na Habel Chidawali, Dodoma[/FONT]
  [FONT=&quot]
  MAWAZIRI Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, jana walishambulia kwa maneno makali wajumbe wawili wa Sekretarieti ya CCM kwamba wamekuwa wakikivuruga chama na kusababisha mgawanyiko uliopo.Lowassa aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu, kutokana na kashfa ya Richmond ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzungumzia suala hilo wakati wa mjadala wa hali ya siasa, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kilichomazika jana mjini Dodoma.

  Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao hicho zinasema Lowassa alianza kubwaga moyo wake baada ya NEC kuridhia ombi la Kamati Kuu ya chama hicho (CC) kwamba suala la mageuzi ndani ya CCM maarufu kama kujivua gamba lirejeshwe katika kamati hiyo ili lifanyiwe kazi kwa taratibu za kawaida za kinidhamu baada ya wahusika kukataa kuachia nafasi zao.

  "Mwenyekiti kwanza napongeza uamuzi huu wa kurejesha jambo hili katika taratibu za kawaida, lakini napenda kufahamu kwa miezi saba nimetukanwa nikiitwa fisadi, watu wamezunguka nchi nzima kwa fedha za chama wakinitukana, hivi hatukujua kwamba kuna kamati hizo za maadili,"Lowassa alinukuliwa akihoji.

  Lowassa alinukuliwa akiwataja Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Tanzania Bara, John Chiligati kwamba wamekuwa wakitukana watu ovyo kwa fedha wanazopewa na CCM.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, Lowassa alitumia dakika saba kumshambulia Nape kwamba amekuwa akifanya mambo nje ya utaratibu na kwamba mwenendo huo umekuwa ukikibomoa chama badala ya kukijenga.

  Baada ya maneno ya Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Sumaye alisimama na kuhoji sababu za chama hicho kunyamazia ukiukwaji wa taratibu ambao umekuwa ukifanywa na watendaji hao.

  "Mwenyekiti huyu bwana (Lowassa) amesema kwamba amechafuliwa kwa miezi saba, sasa kama leo tunasema kwamba tunarudi kwenye utaratibu wa kamati za maadili, hao waliomchafua watafanywaje?"Sumaye alinukuliwa akihoji.
  Hata hivyo, taarifa za ndani ya kikao hicho zilimnukuu Kikwete akisema kwamba viongozi hao watakuchukuliwa hatua za kinidhamu kama watakuwa wamefanya hivyo.
  Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete aliwasihi wajumbe kuachana na suala hilo na badala yake kuchangia maeneo mengine ya taarifa hiyo ya hali ya siasa iliyowasilishwa na Katibu wa Siasa na Mambo ya Nje ya CCM, January Makamba.

  Kikwete alinukuliwa akihitimisha hoja hiyo kwa kusema kwamba: "Jamani hapa tunajenga chama, watu wanasubiri kusikia tukimaliza kikao chetu kwa ugomvi, naomba tumalize kwa amani na twendeni tukajenge chama chetu".

  [/FONT][FONT=&quot]RICHMOND[/FONT][FONT=&quot] YATAJWA[/FONT][FONT=&quot]
  Vyanzo vyetu vilimnukuu Lowassa akizungumzia suala la Kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond kwamba yeye aliamua kuvunja mkataba baina ya kampuni hiyo, lakini Rais KIkwete alimwambia subiri baada ya kuwa amepata ushauri wa Makatibu Wakuu.

  Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), alinukuliwa akisema: "Mwenyekiti utakumbuka kwamba mimi nilishaamua kuvunja mkataba wa Richmond mapema, lakini baada ya kukupigia simu ukiwa katika safari nje ya nchi ulisema tusubiri kwani ulikuwa umepata ushauri wa makatibu wakuu wa wizara, sasa leo hii ninahukumiwa nakuitwa fisadi kwanini?".

  "Nilijiuzulu kuwajibika kwa ajili ya kuilinda Serikali yangu na kwa heshima ya chama changu, sasa kwanini leo nahukumiwa kwa jambo hili, tena natukanwa na wana CCM wenzangu na siyo wapinzani nchi nzima kwamba mimi eti fisadi?,"alinukuliwa akihoji Lowassa.

  Kadhalika kada huyo wa CCM alinukuliwa akimkumbusha Rais Kikwete kwamba: "Mwenyekiti nikukumbushe mwaka 1997 kule Zanzibar, kina Mzee Daudi Mwakawago walikuja na mafaili yakiwa na tuhuma dhidi ya mtizamo hasi wa jamii dhidi yako, kwa hiyo wakati ule kama si busara za kina Mzee Mkapa (Benjamin) leo usingekuwa hapo ulipo".

  Lowassa alisema kama alivyozungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa walipokutana jijini Dar es Salaam, tatizo kubwa analolifahamu la vita ya sasa ni urais wa 2015.

  "Mwenyekiti nikukumbushe jambo jingine, kule Zanzibar mwaka 1997 walipoleta tuhuma za mtizamo wa umma dhidi yako, ulisema kwamba kuwa Rais ni mipango ya Mungu,"alinukuliwa Lowassa katika maelezo yake ndani ya NEC

  Alisema kwa kuzingatia mazingira hayo, hii leo si sahihi hata yeye (Lowassa) kuhukumiwa kwa kuzingatia kile kinachodaiwa kuwa ni mtizamo wa umma dhidi yake unaompa sura ya ufisadi, jambo ambalo alidai kwamba siyo la kweli.
  Baada ya Lowassa na Sumaye kuongoa, kada maarufu wa chama hicho, Kingunge Ngombale Mwiru alisimama akitaka kuongelea dhana ya gamba ndipo Mkapa alipomshtua Kikwete kwamba hoja hiyo ifikie mwisho.
  Baadhi ya wajumbe waliiambia Mwananchi kwamba wakati Lowassa akiongea Mkapa alionekana kufurahi.


  [/FONT]
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Nov 26, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Full masarakasi tu!! They are good in staging up scene areas!!!
   
 6. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #6
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kwamba Rais Kikwete ndiye aliyemtuma Lowassa kwa kila alilofanya Wakati Wa Richmond na sisi tunataka kujua kwa kuwa Lowassa anasema yeye alitaka kuvunja Mkataba lakini Kikwete akamkataza , Sasa hivi kuna kesi ya kuwa Richmond ni Hewa na kwamba kampuni hiyo ni mali ya Lowassa sasa Lowasa inaonekana anawafahamu Wamiliki Wa Richmond na ndio maana Alitaka kuvunja Mkataba nao !!!

  Sasa kama Bunge limesema Richmond ni Matapeli mimi nataka kujua Hivi Lowassa alikuwa anataka kuvunja Mkataba na Matapeli???

  Na kama kweli yeye ni Mzalendo kwa nini asijiuzulu Wakati Ule Kikwete amekataa kuvunja mkataba na matapeli??
  Mbona Augustino Mrema aliachia Ngazi baada ya kutofautina na Rasi Mwinyi??
  Hapa inaonyesha Lowassa alikuwa Mwizi Sambamba na Richmondi(RICHARD MONDULI)!!!

  Kumbuka Lowassa ndiye aliunda Gvt Negotiating Team sasa alikuwa anaogea na Nani ???

  Kumbuka Mpaka juzi Ndipo tunajua wamiliki Wa Dowons ambao bado ni Utata !!! Je Lowassa kwa nini anaficha Wamiliki Wa Dowans na Richmond???

  Kwa nini ajitokeze sasa wakati Nchi imeliwa imebaki mifupa mitupu!!!

  Lowassa atuambia kweli ni nani Mumiliki wa Richmon na Nina Mumiliki wa Dowons , Na ni nani aliyetushitaki ICC kudai 111blns
   
 7. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #7
  Nov 26, 2011
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Tatizo lako unajichanganya... unataka kumtetea JK lakini unajikuta kuwa hateteki :biggrin:. Tafuta njia nyingine maana Rais wako ameshachafuka!
   
 8. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #8
  Nov 26, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145

  Sina Mawazo ya kumutetea Rais Lakini pia Kitendo cha Lowassa kumtaja Kikwete kuwa ndio richmond Kisimpe Lowassa Uhalali wa Kututawala !!!
  Ni kwa nini Watu waseme kuwa Lowassa anafaa kuwa Rais baada ya kumutaja Jk kuwa ndiye aliyempa maelekezo kuhusu Richmond??

  Hivi Upinzani hawana haki ya kuongoza Urais Mpaka Watu Wamupigie Debe Mtu Mwizi??
  Chadema Walisha taja Orodha ya Mafisadi akiwemo Kikwete na Lowassa Hapo nani Muuadilifu??

  Pia nani asiyejua kuwa Kikwete ndiye aliyekuwa anatoa maelekezo kwa Lowassa kama PM??
  Hapo hakuna jipya , Kazi ya PM ni kupewa Maelekezo na Rais , Kazi ya Chief Secretary Luhanjo pia inafahamika!!!

  Mbona Luhanjo Kahukumiwa kwa wizi wake , lakini
  alikuwa amepewa maaelekezo yote na Kikwete!!!
  Hapa tunaopata kujua kwamba yapo Mambo ambayo Kikwete alimuelekeza Lowassa kuyafanya lakini si yote ambayo Lowassa alrtekel;eza kwa uaminifu kama Luhanjo alivyo fanya !!!

  Ukweli ni Kwamba Lowassa kasema kuwa Yeye na Kikwete ni Marafiki ni kwa nini Waendeshe Nchi Kirafiki harafu wanatia umasikini ,harafu Watu wanasema Lowassa anafaa kuwa Rais Huu ni Upuuzi!!!

  kazi iliyopo ni bora nchi iongozwe na Upinzani ili CCM ijute na Wezi Wote akiwemo Lowassa ,Wapelekwe Mahakamani!!!
   
 9. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Binafsi i admire a brave and a hard working president 2015.
   
Loading...