Mwenendo Wa mchakato Wa Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenendo Wa mchakato Wa Katiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwikumwiku, Nov 14, 2011.

 1. m

  mwikumwiku Senior Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa hali inavyokwenda kwa sasa juu ya majadiliano kuhusiana na Muswada wa Mapitio ya Katiba ni wazi kwamba kuna baadhi ya watu au vikundi vya watu, ama "wanasiasa", "wasomi" au "wanaharakati" wameteka mchakato mzima na wao kujifanya ndio wananchi. Hii inaweza ikapelekea katiba mpya itakayotungwa kuwa ya kikundi Fulani cha watu "elites" sote tunafahamu kuwa ni kwa kiasi gani katiba za nchi nyingi zimevurugwa na "elites".

  My take:
  Kama ningekuwa Rais ningesitisha mchakato wowote kuhusiana na Katiba mpya mpaka hapo watanzania wenyewe, na si kikundi au vikundi vya watu" watakapotaka katiba mpya. Mnatuchanganya akili zetu kwa masilahi yenu binafsi.
  k
   
 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Eti mjadala usitishwe hadi Watanzania wenyewe...
  Kwani hicho kikundi au hao elite ni raia wa wapi?
  Kwa hiyo tatizo lako ni kuwaona wanaharakati
  wakichangia mjadala wa katiba? kwani kuna watu
  wamezuiwa kuchangia? Hii kwangu ni hoja mfu...
   
 3. baina

  baina JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mleta mada sina shaka umetumwa na kama hujatumwa naomba ujibu swali hili
  JE ULIONA WAPI MWAJIRIWA ANAMPANGIA MWAJIRI KAZI ANAZOTAKA KUFANYA AU KWA MAANA NYINGINE NI KWAMBA ULIONA WAPI MWAJIRIWA AKIANDAA JOB DESCRIPTION NA KAMA SIO MWAJIRI ANAMUANDALIA MWAJIRIWA?
   
 4. k

  kizazi kipya JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  walewale....stupid
   
 5. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Nionavyo mimi huu ni mswada wa mabadiliko ya katiba, baadhi ya watu wanapendekeza uwe mswada wa kubadilisha katiba. Naona dhahiri kwa jinsi baadhi ya wanajamii wanavyoupinga ndivyo muda unavyokwenda mbele na ni manufaa kwa watawala, kwa mfano ikiwa hautapita kwa jina lake tu, inamaana mpaka kikao kingine cha bunge, hapo ndipio kitazungumziwa kilichomo ndani ya mswada wenyewe mpaka ukubalike ndipo utaanza mchakato wa kuandika hiyo tuseme ni katiba "mpya". Hapo itachukua mda gani?? Na wengine wameeanza kujadili katiba mpya iweje hata kabla ya huyo atakaepokea mapendekezo yao hajaundwa.

  Ukweli ni kwamba kila kundi linatazama maslahi yake kwanza kwenye katiba hiyo na baadae mengine kwa ajili ya kuzuga zuga tu. Sitegemei hata kidogo chama tawala kikubali kuwa na katiba itakayoweza kurahisisha kukiondoa madarakani.

  Na ndugu zangu wa upinzani nao wanajua wazi kule bungeni hawana uwakilishi utakaoweza kupitisha yale wanayopenda, hivyo wanajaribu kupenyeza kwa njia ya "peoples power'' kwa kuchukua advantage zinazojitokeza km. matatizo ya umeme, DOWANS,wananchi kuuwawa na vyombo vya dola, Machinga, wabunge kukamatwa na vyombo vya dola,uchaguzi wa mameya na lo lote litakalojitokeza (inaelekea wataandamana mpaka miguu miingie ndani ) angalau wajulikane kama na wao wapo.

  Nasubiri hawa wawakilishi wetu wataaamuaje kuhusu huu mswada unaowakilishwa leo...
   
 6. Relief

  Relief JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inaonyesha umechoka ndugu yangu, hebu pumzika waache watu wasio na usingizi waseme sawa eeh
   
 7. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #7
  Nov 14, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,847
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180

  Tunahitaji kama jamii tujiridhishe na mchakato si kuangalia muda tu.the process must be sorrounded by good governance and not other wise, kuandika katiba haichukui hata mwezi document inakamilika.kinachochukua muda ni ukusanyaji maoni ambao lazima uwe wazi kwa wananchi na si kwa kikundi cha mafisadi.
   
 8. m

  mwikumwiku Senior Member

  #8
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  As human being, we are normaly pleased to hear what we want to hear. But take ma word, endapo trend hii ya kupiga kelele bila kuwa na "more focused strategies" mchakato huu utakula kwa kwetu wananchi tusio tunaoruhusu watu wachache wawe wazungumzaji wetu "elites" wapige kelele zao kwa migongo yetu!

  Namna mambo yanavyoenda sioni possibility ya kuwa na katiba mpya kabla ya 2015 kwakuwa ni dhahiri kwamba hawa wanaojifanya "wasemaji wetu" hawataki zoezi hili likamilike. Ni vema tukafahamu kwamba kuna NGO na vikundi vingine vingi vimeanzishwa na vinaendelea ku-exist kwaajili kwa sababu ya mchakato huu! Kwa vyovyote vile NGO na vikundi kama hivi kamwe havitapenda mchakato huu ukamilike.

  Mfano kikundi kama Jukwaa la Katiba kuendelea kuwepo kwa mchakato ndo uhai wao! Tafadhali wenzangu na mimi tusije tukaondolewa kwenye malengo yetu yaani kuwa na katiba mpya kabla ya 2015 itusaidie kwenye Uchaguzi huo.
   
 9. m

  mwikumwiku Senior Member

  #9
  Nov 14, 2011
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tujifunze kuyasikia hata yale tusiyoyapenda kuyasikia! tunapoteza dira ya kile tunachokitaka!
   
 10. k

  kada1 Member

  #10
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naona hujamuelewa mtoa hoja, soma tena halafu critisise, naunga mkono hoja hii, hwa jamaa wote wanatuchanganya tu.
   
 11. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Katiba ni roho ya Taifa. Ni heri kuwa na katiba nzuri iliyochukua miaka 100 kuandaliwa kuliko kuwa na katiba bomu ambayo imechukua wiki moja kuandaliwa.
  Kwa hiyo acha hivi vikundi vifanye kazi zake, kwani wao ni dira tu ambapo wananchi wengi hawajui waanzie wapi waishie wapi katika kuandaa katiba itakayokuwa ya Wananchi na si ya Mafisadi na CCM yao.
   
 12. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Huyo unayemsemea hajachaguliwa na Watanzania wote, ila kikundi tu cha watu 5 kati ya milioni 40.
   
 13. Jacobus

  Jacobus JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 29, 2011
  Messages: 3,580
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Tu wepesi mno kusahau. Je anayehitaji KATIBA mpya ni nani?
  Jibu 1. Kama ni wananchi = Hii haiji kama kuagiza kahawa na tende, Kenya ni mfano mzuri tuu wa hivi karibuni.
  2. Kama ni watawala (si viongozi) = Hii ingepatikana ndani ya miezi sita tuu.
  Tafakari sana MWANANCHI.
   
Loading...