Mwendokasi: Tuungane kupinga huu wizi

Mwendokasi: Tuungane kupinga huu wizi

Kaisari

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2012
Posts
3,636
Reaction score
3,045
Jamani nimeweka 5,000/= kwenye kadi ya mwendokasi nimepanda gari mara nne tuu. Inaniambia ' insufficient balance'
Tuungane kupinga huu wizi.
 
Ee bwana tunaibiwa mbaya kabisa. Kuna siku niliweka elfu kumi nikaenda mara sita hela ikakata sikujali sana ila leo nimethibitisha. Tunaibiwa sana.

Kuna wakati mtu unapanda bus unashuka kituoni unakuta mashine za kusoma kadi kuwa abiria ametoka hazifanyi kazi na wao husema kama usipo sign off systems inalamba fedha.

Usishangae kusikia wakati mwingine wanakorofisha mashine zisisome ili unaposhuka kituoni usi sign out na kwa maana hiyo salio lako linaendelea kulambwa.

Hiyo Maxi malipo yao imeniingiza hasara mara nyingi hata kwenye ununuzi wa vocha za simu, siiamini kamwe
 
Imebidi nirudi kutumia tickets,
Hivi na kwanini hawa wadai nauli ya 650 zaidi ya dala dala ya kawaida 400, kwani hii siyo daladala kwanini wao wanachaji zaidi.
Huduma zao jinsi siku zinavyozidi kusonga zinazidi kuwa mbaya, unakaa kituoni dk 40, hakuna gari na likija limejaa hamna pa kusimama,
Walipoanza walitangaza kila baada ya dk 5 patapita gari. Sasa mwendo kasi imeshakuwa hovyoo, watu wanakaa kituoni saa nzima wamefungiwa kwenye mabanda hayo hamna gari.
 
na hili lisaa uwe mzima kama mgonjwa utajuta, sijui kwanini viti waliweka kimara mwisho, kivukoni na gerezani.
 
Eidha umesahau baadhi ya ruti zako au umepigwa na keshia sababu ya kutokuwa makini!
 
Jamani nimeweka 5,000/= kwenye kadi ya mwendokasi nimepanda gari mara nne tuu. Inaniambia ' insufficient balance'
Tuungane kupinga huu wizi.
....sisi Wengine tuligundua kitambo Wizi wa hao jamaa tukaachana nazo....kwahiyo kama nawe unapinga Wizi Ungana nami kutumia Tiket kila unatumia Mwendokasi kama hutaki basi achakulalamika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani nimeweka 5,000/= kwenye kadi ya mwendokasi nimepanda gari mara nne tuu. Inaniambia ' insufficient balance'
Tuungane kupinga huu wizi.
Hakikisha kabla hujaondoka soma vizuri kwenye risiti wameweka sh ngapi na salio lako sh ngapi
 
Imebidi nirudi kutumia tickets,
Hivi na kwanini hawa wadai nauli ya 650 zaidi ya dala dala ya kawaida 400, kwani hii siyo daladala kwanini wao wanachaji zaidi.
Huduma zao jinsi siku zinavyozidi kusonga zinazidi kuwa mbaya, unakaa kituoni dk 40, hakuna gari na likija limejaa hamna pa kusimama,
Walipoanza walitangaza kila baada ya dk 5 patapita gari. Sasa mwendo kasi imeshakuwa hovyoo, watu wanakaa kituoni saa nzima wamefungiwa kwenye mabanda hayo hamna gari.
Kunapoendea utazikumbuka dalala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafanyabiashara wezi huwa hawanyooki mpaka wapate kesi. Inatakiwa muungane muishtaki Udart vinginevyo mtaendelea kunyonywa. mnachofanyiwa ni ufisaidi wa kimtandao. Hiyo ni JINAI
 
Back
Top Bottom