π
KERO MWENDOKASI MBAGALA
1. Mfumo wa kupanda π«
Mwendo kasi za Mbagala hairuhusiwi kugeuza. Ukifika mwisho, lazima ushuke halafu upange mstari upya ili upate siti.
π Hii inalazimisha baadhi ya watu
kulipa nauli mara mbili, hasa wazee na wenye changamoto za kusimama muda mrefu.
2. Nauli iko juu πΈ
Nauli za mwendo kasi bado ni kubwa ukilinganisha na umbali wa safari.
π Tukizingatia mabasi yanatumia
CNG na ni mradi wa serikali, wananchi wanategemea nafuu zaidi.
3. Kuondoa daladala = kuongeza kero β
Kuondoa daladala kumeongeza changamoto kwa wananchi:
π Nauli ya daladala ni nafuu zaidi
π Hakuna limit kubwa ya mizigo
π Mchana nauli hupungua
π Ilikuwa option mbadala muhimu kwa watu wengi
4. Usumbufu wa foleni Ilala π
Mofat imeshindwa kudhibiti matumizi ya njia ya Ilala.
π Magari mengine yanaingia kwenye njia za mwendo kasi na kusababisha
foleni kubwa, huduma inapoteza maana yake.
5. Express hazieleweki β
Express za Ilala Boma hazieleweki vituo vyake rasmi, tofauti na Kivukoni na Gerezani.
π Hii inaleta
mkanganyiko kwa abiria, hasa wanaotoka Mbagala kwenda Ilala.
π₯ HITIMISHO
Mwendo kasi ni mradi mzuri, lakini bado kuna changamoto zinazohitaji maboresho ili kuwahudumia wananchi kwa haki na ufanisi.