no one like you
Member
- Aug 27, 2014
- 43
- 11
kwa kweli nilipigwa na butwa kuona mazingira yale,najiri aliligundua hilo,kwa sauti ya upole najiri akaniuliza'unashangaa nini mume wangu wa ndoa'?kwa kweli ni maneno ambayo yaliushtua moyo wangu kuniita mume wake,kwani ni ajabu dini kuolewa na binadamu,nilitaka kumhoji maswali kadhaa najiri,kwa kweli kabla hata sijamuuliza akadakia kwa sauti tamu kama asali akisema'najua unachotaka kuuliza mume wangu,nakuita mume kwa sababu nilikupenda hata kabla hujazaliwa ,na ujio wako duniani umenifanya niwe mtumwa wa kukutembelea kila siku,usiyashangae sana haya mazingira ,kiukwel leo ni siku muhimu sana kwetu na hutaisahau,leo ni tofauti na siku zote kwani nimewaarika wazaz wangu katika siku hii,siku hiyo ndo ilikua mara ya kwanza kusikia kama majini wana wazazi.Najiri akaendelea kwa kusema'baada ya kukaa kwa muda mrefu katika urafiki na wewe wazazi wangu walinishauri tufunge pingu za maisha,kwa hyo leo ndo siku yenyewe,'maneno hayo yalifanya miguu yangu kufa ganzi na mapigo ya moyo kuongezeka,fuatilia mwendelezo