Hata ikiwa uongo watu watahisi kweli, tatizo mnaharibu sana kuliko kujenga ndugu zangu.
mmarekani anaitwa mmarekani
mcanada anaitwa mcanada
muUAE anaitwa mwarabu
warabu mbona wanatoka nchi nyingi tu, moja wapo ni Tanzania, sasa hao wote ndio wamiliki? Acheni ubaguzi bana
mnataka wazungu na wadenmark pekee ndio waje wawekeze??? pili hii habari ni ya kizushi tu
NI kweli mwarabu alimilikishwa Loliondo na kutokana na juhudi za wabunge kama kina Philp Marmo na mwandishi Stan Katabaro walizuia akaendelea kuwinda kimya kimya huku akifanya kila kitu kama Dubai. Leo Serikali hasa IKULU inammilikisha Mwarabu eneo la Loliondo. Wanafanya hesabu ili kutumia vipengele vya sheria ya ardhi ya kuhaulisha ardhi ya vijiji na kuwa ya hifadhi. Wanadai ni kwa madhumuni ya hifadhi huku mwarabu inasemekana amewinda takriban wanyama 50,000 hadi sasa, amejenga chanzo kikuu cha maji ameweka mtambo wake wa mawasiliano. Halafu leo IKULU inataka kuwaondoa Wamasai. Kwa sababu Serikali haitambui tena sheria isipokua zile za kujinufaisha, TUWAUNGE MKONO wamasai wa Loliondo. WOTE KWA UMOJA WETU TUSIKUBALI
Mkuu waliopo ni wachache sana na kibaya wengi wao wananunulika.Sasa tunao waandishi wengi wa habari za kiuchunguzi,mitandao kama JF,na walau kidogo nafasi ya kusema tofauti na enzi za Stan Katabalo!
Kwanini hili swala tunalijadili kwa wepesi sana? Hivi kweli Stan Katabalo alipigana bila woga leo tuna puuza damu yake kwa faida ya vizazi vyetu?
Mimi nadhani waandishi wetu kama wana nia njema waanzishe Operation chukua Loliondo kwa faida ya Taifa hili na kuenzi juhudi binafsi za Stan Katabalo!