28. Ulinzi wa taifa Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6 (1) Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, ardhi na umoja wa taifa.
(2) Bunge laweza kutunga Sheria zinazofaa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kutumikia katika majeshi na katika ulinzi wa taifa.
(3) Mtu yeyote hatakuwa na haki ya kutia sahihi kwenye mkataba wa kukubali kushindwa vita na kulitoa taifa kwa mshindi, wala kuridhia au kutambua kitendo cha uvamizi au mgawanyiko wa Jamhuri ya Muungano au wa sehemu yoyote ya ardhi ya eneo la taifa na, bila ya kuathiri Katiba hii na sheria zilizowekwa, hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi.
(4) Uhaini kama unavyofafanuliwa na sheria utakuwa ni kosa la juu kabisa dhidi ya Jamhuri ya Muungano.
Nimejiuliza sana maana ya hiki kipengele nakosa jibu.Jeshi la polisi wamewekwa tayari kupambana na raia wanaodhamiria kumwondoa mvamizi.Nijuavyo ni kwamba mvamizi anaweza kuja kwa mbinu nyingi ikiwemo ya mikataba ya ulaghai lakini azma yake ni kuikalia nchi ama kipande cha nchi kwa manufaa anayoyajua yeye.Tufike mahala tuwashinikize wabunge kuchukua hatua ya kuhoji madudu kama haya bila kusubiri raia waamue...28. Ulinzi wa taifa Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6....hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi.
Mkuu hata katiba imeonesha njia endapo kuna wahuni watadhani wanaweza kuuza nchi bila kuhojiwa ...hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi....NI kweli mwarabu alimilikishwa Loliondo na kutokana na juhudi za wabunge kama kina Philp Marmo na mwandishi Stan Katabaro walizuia akaendelea kuwinda kimya kimya huku akifanya kila kitu kama Dubai. Leo Serikali hasa IKULU inammilikisha Mwarabu eneo la Loliondo. Wanafanya hesabu ili kutumia vipengele vya sheria ya ardhi ya kuhaulisha ardhi ya vijiji na kuwa ya hifadhi. Wanadai ni kwa madhumuni ya hifadhi huku mwarabu inasemekana amewinda takriban wanyama 50,000 hadi sasa, amejenga chanzo kikuu cha maji ameweka mtambo wake wa mawasiliano. Halafu leo IKULU inataka kuwaondoa Wamasai. Kwa sababu Serikali haitambui tena sheria isipokua zile za kujinufaisha, TUWAUNGE MKONO wamasai wa Loliondo. WOTE KWA UMOJA WETU TUSIKUBALI
Wadau,
Nakumbuka wengi wetu bado tunamkumbuka mwandishi wa habari za kiuchunguzi Marehemu Stan Katabalo aliyeibua mchakato wa kimya kimya wa Ikulu kumuuzia Mtawala wa UAE ardhi yetu yenye rasilimali ya Loliondo. Kifo chake kilikuwa cha kutatanisha, na ikichukuliwa enzi zile ambapo uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa ndani ya kikombe hivyo hakukuwa na wa kuibana serikali kuhusiana na utata mwingi uliogubika habari ile na kifo chake.
Leo tunashuhudia mwendelezo wa serikali kushinikiza kuwaondoa wananchi wa Loliondo ili kupanua kitalu cha uwindaji kwa mwarabu ambaye kipande alichopewa kimeshamalizika wanyama na anataka ZAIDI. Kinachotia mashaka ni namna ambavyo mwekezaji huyo alivyoweza kujijengea himaya yake ambapo hata mtu anapokaribia ama kuingia eneo lile anakutana na ujumbe KARIBU KATIKA FALME YA NCHI ZA KIARABU ambapo kwa ujumbe huo ni dhahiri kipande ile ni milki ya mfalme wa uarabuni.
Katiba imekiukwa na wanaotakiwa kuijibu hii ni IKULU kwa sababu ndiyo tuliowapa mamlaka ya kuilinda Katiba chini ya Rais. Nanukuu hapa chini kipengele kilichokiukwa, soma kwenye bold
Tuhuma hizi zimekuwa zinakiukwa kwa makusudi kutolewa ufafanuzi na wahusika (Ikulu).
Nchi imemegwa na kupewa asiyestahili. Nini kifanyike?
Nina uhakika mkuu. Uthibitisho wake ni haya tunayoyashuhudia leo.Una uhakika na hapo kwa red? au unataka kupotosha umma wa watanzania!
Nyie semeni wazi tu kwamba mnachotaka ni malisho na maji kwa ajili ya ng'ombe wenu (wanyamapori siyo priority kwenu), haya mengine ni uzushi mtupu!!
mnataka wazungu na wadenmark pekee ndio waje wawekeze??? pili hii habari ni ya kizushi tu
Nina uhakika mkuu. Uthibitisho wake ni haya tunayoyashuhudia leo.
Tatizo lako na wenzako huko juu ni kujaribu kutumia hadaa ya kutumia wanyama pori ili mkamilishe mpango wenu wa uovu.
Wanyama walikuwepo hata kabla ya mjerumani kuja, na Wamaasai waliishi na wanyama hao huku wakifuga bila matatizo yeyote. Lakini tangu mlipokubali kuishi kwenye mifuko ya majambazi ya nje ndo mmejivua hata uraia.
Una uhakika na hapo kwa red? au unataka kupotosha umma wa watanzania!
Nyie semeni wazi tu kwamba mnachotaka ni malisho na maji kwa ajili ya ng'ombe wenu (wanyamapori siyo priority kwenu), haya mengine ni uzushi mtupu!!