Amba Samedi
Senior Member
- Apr 5, 2024
- 193
- 326
Habari wanaJF,
Ni jioni nyingine tena nakuja hapa kumalizia siku hii. Nikiwa hapa, nilipiga picha ya kumbuukumbu za maisha ya hapo nyuma. Nikagundua cycles fulani zinazojirudia rudia. Na cycle (mzunguko) unapoisha, huna budi kuanza tena.
Mwanzo huwa ni mgumu. Maisha sio rahisi baada ya kupoteza vyote. Lakini if this is your case, endelea kusoma. Kuna kitu fulani nimeakuandalia kukutia moyo unapokabiliana na wiki hii mpya.
Nakuletea "the 3Ts You Must Know if You're Starting from Scratch" (Vitu 3 vya kuvifahamu endapo utakuwa unaanza upya).
Muda sio tu masaa 24—ni namna unavyoutumia. Utahitaji muda wa kujifunza, wa kufikia watu, wa kutoa huduma, na wa kujenga kitu ambacho kitabadilisha maisha yako na ya jamii yako. Utahitaji muda wa kuvumilia ukimya, kusubiri dalili za mvua, na kuendelea hata pale juhudi zako zinapoonekana kugonga mwamba.
Fahamu kuwa Mohammed Dewji (Mo) hakurithi utajiri mkubwa kama wengi wanavyodhani. Alianza na biashara ya familia iliyokuwa ndogo, lakini alitumia muda mwingi kujifunza, kupanua mtandao wake, na kuweka mikakati ya muda mrefu. Leo, anajulikana kama mmoja wa wafanyabiashara wakubwa Afrika (na anaongoza Afrika Mashariki, kwa mujibu wa Forbes List 2024). Lakini ilikuwa ni safari ya muda mrefu—yenye kazi kwelikweli.
"Muda ni mtaji wa maskini mwenye ndoto kubwa."
Kila mtu ana kitu kimoja anachokifanya vizuri zaidi ya 90% ya watu wanaomzunguka. Hicho ndicho silaha yako. Kitafute. Kikuze. Kikamilishe. Kama hujui talanta yako, waulize wanaokufahamu. Halafu jifunze kitu kipya kinachohusiana na talanta/kipaji chako kila siku, hata kama ni kwa dakika 15 tu. Kipaji hukua. Baada ya mwaka mmoja utakuwa mbele ya asilimia 90 ya watu.
Angalia Nandy—aliyekulia katika mazingira ya kawaida mkoani Moshi. Alijua kuwa ana kipaji cha kuimba, akakikuza kupitia mashindano kama Tecno Own the Stage. Alijitahidi, akaendelea, na leo ni miongoni mwa wanamuziki wakubwa Afrika Mashariki. Kipaji kilichofanyiwa kazi kiliweka historia. Konde Boy, Joel Nanauka na wengine kama hao ni mifano ya kuichunguza vizuri.
"Kipaji ni zawadi; lakini mafanikio ni kazi."
Wasanii wengi waliofanikiwa walipiga mbio kwa mgongo wa mtu mwingine. Ambaye alikuwa na watu, na access, na platform. Rais Samia hangekuwepo kama mwamba hangemwona na kumpa nafasi. Christiano Ronaldo (CR7) alishine kwa sababu ya rafiki yake aliyemwamini na kumpasia mpira akafunga, na kupata nafasi kujiunga na Lisbon Footbal academy. Trust, my friend, is the currency of starters.
"Uaminifu hujengwa na matendo, si maneno."
Endapo umelazimika kuanza na hakuna kinachoenda, kama kila kitu ni kigumu—shikilia. Mwanzo ni mgumu. Ndivyo ilivyo. Lakini mchakato huo unakutengeneza kuwa mtu ambaye usingekuwa endapo changamoto hazingekuwepo.
Signed,
Amba Jnr.
Ni jioni nyingine tena nakuja hapa kumalizia siku hii. Nikiwa hapa, nilipiga picha ya kumbuukumbu za maisha ya hapo nyuma. Nikagundua cycles fulani zinazojirudia rudia. Na cycle (mzunguko) unapoisha, huna budi kuanza tena.
Mwanzo huwa ni mgumu. Maisha sio rahisi baada ya kupoteza vyote. Lakini if this is your case, endelea kusoma. Kuna kitu fulani nimeakuandalia kukutia moyo unapokabiliana na wiki hii mpya.
Nakuletea "the 3Ts You Must Know if You're Starting from Scratch" (Vitu 3 vya kuvifahamu endapo utakuwa unaanza upya).
1. Muda (Time)
Muda sio tu masaa 24—ni namna unavyoutumia. Utahitaji muda wa kujifunza, wa kufikia watu, wa kutoa huduma, na wa kujenga kitu ambacho kitabadilisha maisha yako na ya jamii yako. Utahitaji muda wa kuvumilia ukimya, kusubiri dalili za mvua, na kuendelea hata pale juhudi zako zinapoonekana kugonga mwamba.
Fahamu kuwa Mohammed Dewji (Mo) hakurithi utajiri mkubwa kama wengi wanavyodhani. Alianza na biashara ya familia iliyokuwa ndogo, lakini alitumia muda mwingi kujifunza, kupanua mtandao wake, na kuweka mikakati ya muda mrefu. Leo, anajulikana kama mmoja wa wafanyabiashara wakubwa Afrika (na anaongoza Afrika Mashariki, kwa mujibu wa Forbes List 2024). Lakini ilikuwa ni safari ya muda mrefu—yenye kazi kwelikweli.
"Muda ni mtaji wa maskini mwenye ndoto kubwa."
2. Kipaji (Talent)
Kila mtu ana kitu kimoja anachokifanya vizuri zaidi ya 90% ya watu wanaomzunguka. Hicho ndicho silaha yako. Kitafute. Kikuze. Kikamilishe. Kama hujui talanta yako, waulize wanaokufahamu. Halafu jifunze kitu kipya kinachohusiana na talanta/kipaji chako kila siku, hata kama ni kwa dakika 15 tu. Kipaji hukua. Baada ya mwaka mmoja utakuwa mbele ya asilimia 90 ya watu.
Angalia Nandy—aliyekulia katika mazingira ya kawaida mkoani Moshi. Alijua kuwa ana kipaji cha kuimba, akakikuza kupitia mashindano kama Tecno Own the Stage. Alijitahidi, akaendelea, na leo ni miongoni mwa wanamuziki wakubwa Afrika Mashariki. Kipaji kilichofanyiwa kazi kiliweka historia. Konde Boy, Joel Nanauka na wengine kama hao ni mifano ya kuichunguza vizuri.
"Kipaji ni zawadi; lakini mafanikio ni kazi."
3. Uaminifu (Trust)
Unapokuwa huna kitu, uaminifu wako ndiyo mtaji wako wa kwanza. Ukiukosa, unaharibu msingi wa kila kitu. Ukikopa, lipa kwa wakati. Ukipewa nafasi, shine. Ukiaminiwa na mtu, usiache doa. Uaminifu unafungua milango ambayo hata pesa haiwezi kufungua.Wasanii wengi waliofanikiwa walipiga mbio kwa mgongo wa mtu mwingine. Ambaye alikuwa na watu, na access, na platform. Rais Samia hangekuwepo kama mwamba hangemwona na kumpa nafasi. Christiano Ronaldo (CR7) alishine kwa sababu ya rafiki yake aliyemwamini na kumpasia mpira akafunga, na kupata nafasi kujiunga na Lisbon Footbal academy. Trust, my friend, is the currency of starters.