Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
MWANZILISHI WA WAZO LA UKAWA NI NANI?
Mwanzilishi na muasisi wa idea ya UKAWA ni Deogratius Kisandu wakati akiwa Katibu Mwenezi kitengo cha Vijana wa NCCR Mageuzi Taifa.
Kisandu alifanya mahojiano na gazeti la FAHAMU linalotoka Mara Moja kwa wiki. Na makala hiyo ya mahojiano ilitoka mwezi wa February 2013 kama sijakosea na kama nimekosea itakuwa ni mwishoni mwa mwezi Januari 2013.
Katika makala hiyo iliyokuwa na takribani ya maswali 12 niliulizwa wapinzani wafanye nini ili waweze kuchukua mamlaka ya kuongoza nchi. Majibu yangu yalikuwa ni wapinzani waache ubinafsi wakubali kuungana na kuachiana majimbo ya ubunge na kusapotiana bila kinyongo.
Na pia kuwa na mgombea mmoja wa Urais, na kwa kufanya hivyo tutashinda Urais na kuwa na majimbo mengi ya kushinda ya wabunge.
Wazo hili nililiweka hapa Jamiiforums na pia lilileta mjadala kwa wenyeviti wa vyama vya Siasa vya upinzani na kukubaliana kupitia bunge la Katiba kuanzisha UKAWA ambao baadae ukaja kutumika kama muungano wa vyama vya upinzani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
NCCR mageuzi wazo hili lilichukua mjadala sana na kufanyiwa kazi. Na kabla bunge la katiba halijaanza tulikutana Mwanza na Said Kubenea kwenye kongamano la Katiba, akanikumbusha kuwakumbusha viongozi wangu wa NCCR Mageuzi ili washauriane na upande wa pili wa Chadema ili kuwe na umoja siku ya uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Nilimuelewa nikamwambia wazo langu bado linaendelea. Nikamkumbusha tena aliyekuwa Katibu Mkuu wa NCCR Mageuzi ndg. Mosena Nyambabe juu ya muungano na akaniambia wazo lako limekwisha fanyiwa kazi Siku nyingi sana baada tu ya kutoa ile makala gazetini.
Ndugu zangu, aliyetoa wazo anaishi kama kapuku na alipotezewa. Lakini Mungu atanijibia.
Deogratius Nalimi Kisandu
Expected Chief chairman of ACA.